Meneja
mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy
akisisitiza jambo.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM
Mitandao ya kijamii ni mizuri katika kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana na madhumuni iliyotengenezwa, kwani ina nguvu ya kusambaza habari kwa haraka na kwa wakati hapa duniani.
Pamoja na umuhimu nwa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
Watu hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au wadukuzi, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali toka mitandaoni, kuna mbinu nyingi zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa mbalimbali kutoka kwenye takirishi (Computer) hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao(internet) na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.
Wezi wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares) zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta yake kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia na kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko, kutokana na hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani ndani ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.
Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo kwa kimombo kama ‘Phising’ ambapo ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website hutengenezwa kwa madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote kuhusiana na kitu chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti sana na njia ile yakey logging kwani katika njia hii kazi kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa halisi ya website fulani.
Ili tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa kwa njia ya mtandao kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo makini wakati wote tunapozitumia kompyuta zetu.
Kwaza kabiasa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na hackers (wadukuzi) ijulikanayo kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu kwa watu tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K vyote kwa pamoja ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika kompyuta na kama ikitokea kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza taarifa zako katika kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa kumtafuta mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.
Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall inasaidia kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers) ambao wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa zilizomo ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za baadhi ya taarifa zako.
Ili kujikinga na wizi wa taarifa zetu katika kompoyuta zetu, tunapaswa kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi virusi (Antivirus) mara kwa mara kwani vizuizi hivyo vimetengenezwa kwa ajili ya kuzuia virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze kuiingia ndani ya mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi cha namna yoyote ile, basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya kisiweze kudhuru kompyuta wakati wote.
Bila shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na tabia ya kuji-update vyenyewe.
Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi yaspyware huwa na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake kama ilivyo kwenye key-logging naPhising au huwa na tabia yakuweka matangazo yasiyo na ulazima katika kurasa Fulani iliyopo katika mtandao wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa usalama wa taarifa za mtu kwani hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi kuwa makini na baadhi ya matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi fulani pasipo malipo kwani mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine huwa na virusi vyenye kuweza kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi yako.
Katika hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya kijamii kuepuka kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa usumbufu wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo ni hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au unaposema (remember me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker kujua nenosiri lako kwa kufanya kitendo kijulikanacho kama(Inspect elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).
Katiko hilo, mharifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti (nyota) kisha anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha anafanya uhariri (editing) katika kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa rangi ya bluu kilichoandikwa neno‘passoword’, hapo anafuta na kuandika neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’ na akishamaliza kufanya hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda mfumo wa maneno badala ya doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo humuwezesha kujua tarakimu za nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii uliocha wazi.
Njia nyingine ya jinsi ya kujikinga na wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni hasa vibebaji (attachments) toka kwa watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua kwani hata hao hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa malengo yao binafsi.
Pia ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua katika mitandao mingi ya kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na mingineyo kwani baadhi ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names)kuomba urafiki kisha hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.
Kwa upande wa mabenki, ni vema kuachana na mifumo ya kizamani ya kuongozea kompyuta iliyounganishwa na Mashine za kutolea fedha maarufu kama (ATM) au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani hiyo ni hatarishi kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni mifumo ilikwishapitwa na wakati na hata Kampuni yenyewe ya Microsoft imewataka watumiaji kuwa makini nayo kwani haina-updates tena hali inayopelekea kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa mitandao kwa kutumia software za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba taarifa.
Katika matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards) tunapaswa kuwa makini kuepuka kushea namba za siri kwa marafiki au wapenzi na tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo kama nenosiri katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao wamekuwa watu wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.
Ili kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.
Pamoja na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga maendeleo.
Akitoa rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti kwa watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter, Instagram, BBM, LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na kuleta athari kwa jamii.
Alisema matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli, kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye uhalisia.
“Kuna utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi yakugombana kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani inayosababisha kuvunjika kwa amani na kusababisha matusi pande zote,” alisema Mungy.
Mungy aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha amani ya Tanzania.
“Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu iwapo siyo wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine atende kosa,” alisema.
Kwa mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba faini ya kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha miezi mitatu gerezani.
Kutokana na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si vibaya kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani ama kwa lengo la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu wengine, bali inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu mbalimbali duniani kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali japokuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na maelngo ya uwepo wake.
No comments:
Post a Comment