Makampuni nchini China yameingia katika shutuma kali kua wanatengeza na kusafirisha vifaa vya mateso kwa vikosi vya polisi duniani.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetoa taarifa kuwa makampuni yapatayo mia moja na thelathini nchini humo,kati yao wamekiri kutengeneza
vifaa hivyo ikiwemo vibanio vya umeme,viti vya umeme,na pingu za vidole gumba.
Inasemekana vifaa vingi japo hutengenezwa na kusafirishwa,vingi matumizi yake ni katika kuleta maumivu mwilini na mateso.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu lina shaka na nchi zenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu hasa Africa na Kusini Mashariki mwa Asia wao ndio wateja wakuu wa vifaa hivyo.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment