Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 2 January 2014

OFISA WA JESHI ADAIWA KUUWA WATU KWA RISASI


Na Joseph Zablon, Mwananchi

Dar es Salaam. Watu wawili inadaiwa wameuawa na mmoja kujeruhiwa eneo la Pugu Kinywamwezi baada ya kupigwa risasi na ofisa mmoja wa jeshi wakati walipopanda katika gari lake huku wakishangilia kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2014.
Habari kutoka katika eneo la tukio, zinadai ofisa huyo alipita eneo hilo na kukuta watu wakishangilia mwaka mpya na katika shamra shamra hizo baadhi ya  vijana walipanda katika gari lake wakati linakatiza katika umati wa watu.
Kutokana na hatua hiyo inasemekana ofisa huyo aliwataka watu hao kushuka lakini hawakumwelewa kutokana na kelele na zogo la kushangilia, jambo lililomfanya ofisa huyo kuchomoa bastola na kuwapiga watu watatu ambapo wawili walifariki  katika eneo la tukio.
“Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitimua mbio na gari lake na kuwaacha wananchi wakitaharuki,” kilisema chanzo chetu  katika eneo la tukio.
Katika vurugu hizo, gari ya Kampuni ya Mwananchi Communications  Limited (MCL), lilishambuliwa kwa mawe na kusababisha kioo cha nyuma, upande wa kulia kuvunjwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa  Ilala, Marietha Minangi alipotafutwa kwa njia ya simu ili kufafanua kuhusu tukio hilo, simu yake iliita bila kupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu.
Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya  Dar es Salaam, Suleiman Kova alitaka aulizwe kamanda Minangi kwa madai kuwa yupo hewani na anapatikana “Mtafute tu, mbona wenzako wamempata,” alisema Kova na kukata simu.
Kamanda wa Polisi wa Temeke, Englbert Kiondo alisema mwaka mpya ulisherehekewa vizuri.

CHANZO: Mwananchi

No comments:

Post a Comment