Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 13 January 2014

KAMATI KUU CCM YAWAPONGEZA WATANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Zanzibar leo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekuwa na kikao cha siku moja leo tarehe 13/01/2014 mjini Zanzibar chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.
Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa maandalizi mazuri na ya kufana ya sherehe hizo.
Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.
Aidha Kamati Kuu imemteua Ndg. Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Kiembesamaki kupitia CCM.
Kesho mgombea huyu wa CCM atachukua fomu za tume za kugombea. Uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Mohamed Gharib Bilal.
Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi.
Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili.
Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
13/01/2014

No comments:

Post a Comment