Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 20 January 2014

CHEKA KIDOGO: IMEFUNGUKA!


Mchungaji alikuwa kanisani akihubiri. Mwanzoni kabisa wa mahubiri alisema: “Siku ya leo ni njema kabisa machoni pa Bwana, kwa sababu leo tunakwenda kufungua vifungo vyote vya shetani. Kwa hiyo, tutafumba macho na kila mmoja aanze kuomba, afungue kila kitu kinachomkwaza… Naamini Bwana atasikia na maombi yako yatajibiwa. Haya, tufumbe macho sasa tuombe…”

Baada ya hapo kila mtu akapaza sauti yake kuomba kwa kila hitaji lake. Mchungaji aliposema ‘AMEN’ na watu wote wakaitikia na kufumbua macho.

Mara ikasikika sauti kutoka katikati ya waumini: “Bwana asifiwe, Imefunguka! Nimeweza! Imefunguka!” Binti mmoja akainuka akishangilia huku kifua chake kikiwa wazi. Mchungaji akasema "Haleluya! Bwana Asifiwe! Nimewaambia Bwana anajibu kila hitaji lako! Haya, binti tueleze, nini kilichofunguka...!"

Akiendelea kuwa katika furaha ileile, binti huyo akasema: “Wiki sasa nahangaika na sidiria hii, nimejaribu kuifungua imeshindikana, mpenzi wangu naye amehangaika kuifungua imeshindikana. Lakini leo imefunguka…!”

Wakati huyo akieleza, kijana mwingine naye akainuka na kusema: “Hata mimi imefunguka…!”

Wenzake wakamuuliza: “Na wewe nini?” maana hawakumuona akihangaika sana.

Akajibu: “Zipu! Ni baada ya kuyaona matiti ya huyo dada…”

No comments:

Post a Comment