Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 13 January 2014

CRISTIANO RONALDO MWANASOKA BORA WA DUNIA

 Ronaldo akifuta machozi baada ya kukabidhiwa zawadi ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Fifa kutoka kwa Pele na Michel Platini.

Nadine Angerer

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameuvunja utawala wa miaka minne wa Lionel Messi wa Argentina anayechezea klabu pinzani ya Barcelona baada ya kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Fifa muda mfupi uliopita.
Ronaldo amemshinda pia Franck Rivery, Mfaransa anayechezea Bayern Munich.
Sherehe za tuzo hizo zilifanyika Zurich, Uswisi.
Kwa upande wa wanawake, kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Nadine Angerer ameibuka kinara mbele ya Marta (Brazil) na Abby Wambach (Marekani). Mdada huyo aliisaidia Ujerumani kutwaa taji ya Euro 2013 kwa wanawake akiokoa penati katika mechi yao ya fainali dhidi ya Norway waliyoshinda 1-0.

No comments:

Post a Comment