Ndugu zangu,
Mwaka huu haujaanza kwa mbwembwe kutokana na mambo mengi, kubwa zaidi ni ule utabiri ambao ulikuwa ukitolewa na mtabiri maarufu wa nyota Afrika Mashariki, marehemu Sheikh Yahya Hussein.
Pamoja na kutabiri mambo mengi wakati mwaka mpya unapoanza, lakini tunakumbuka tabiri zake nyingi katika matukio mbalimbali (wale wenye kuamini waliamini).
Tunakumbuka alivyotoa mkwara mzito wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 ambapo alisema yeyote (ndani ya CCM) atakayejitokeza kumpinga ama kupambana na Rais Jakaya Kikwete, lazima angekufa. Magare John Shibuda pekee ndiye aliyekuwa amejitokeza kutaka kuwania urais kupitia CCM, lakini akajitoa.
Tunakumbuka alivyotoa mkwara mzito wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 ambapo alisema yeyote (ndani ya CCM) atakayejitokeza kumpinga ama kupambana na Rais Jakaya Kikwete, lazima angekufa. Magare John Shibuda pekee ndiye aliyekuwa amejitokeza kutaka kuwania urais kupitia CCM, lakini akajitoa.
Wakati wa kampeni za CCM 2010, baada ya Rais Kikwete kuanguka jukwaani pale Jangwani, alijitokeza na kusema: ...Kikwete hana walinzi, maadui zake wanamwandama, hivyo angetoa ulinzi!
Pamoja na ukweli kwamba mwanawe, Hassan, amerithi mikoba na kutoa utabiri, lakini nguvu yake kwa wanaoamini nyota inaelekea kuwa bado ndogo.
Kwenu wadau.
Sunday, July 26, 2009
UTABIRI WA SHEIKH YAHYA HUSSEIN
Sheikh Yahya Hussein
ameibuka na utabiri wa mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ule unaodai kuwa
kuna rais wa nchi moja ya mashariki mwa Afrika atatekwa akiwa kwenye
ndege au kupinduliwa.
Sheikh Yahya amewaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo, litatokana na hali ya kupatwa kwa jua kulikotokea juzi nchini China na kwingineko barani Asia.
Ameendelea na kutabiri kuwa pia kutatokea matatizo katika mambo ya ulinzi na usalama kwa viongozi wa nchi mbalimbali za mashariki ya Afrika.
Hata hivyo, hakutaja nchi yoyote ambayo itakumbwa na tukio hilo.
"Pia natabiri baadhi ya wabunge kadhaa kufungwa na wengine kufa ghafla," akasema.
Akaongeza kuwa vilevile, baadhi ya maofisa wa ngazi za juu serikalini watafukuzwa kazi wakiwa nje ya nchi zao kwa kashfa mbalimbali.
Ameendelea kueleza kuwa vyama vya siasa vinavyotawala na vile vya upinzani vitakuwa na mabadiliko makubwa.
Aidha, akasema kuwa Muungano wa Tanzania utaendelea kudumu licha ya watu kulalamikia kasoro kadhaa kila kukicha.
Sheikh Yahya amewaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo, litatokana na hali ya kupatwa kwa jua kulikotokea juzi nchini China na kwingineko barani Asia.
Ameendelea na kutabiri kuwa pia kutatokea matatizo katika mambo ya ulinzi na usalama kwa viongozi wa nchi mbalimbali za mashariki ya Afrika.
Hata hivyo, hakutaja nchi yoyote ambayo itakumbwa na tukio hilo.
"Pia natabiri baadhi ya wabunge kadhaa kufungwa na wengine kufa ghafla," akasema.
Akaongeza kuwa vilevile, baadhi ya maofisa wa ngazi za juu serikalini watafukuzwa kazi wakiwa nje ya nchi zao kwa kashfa mbalimbali.
Ameendelea kueleza kuwa vyama vya siasa vinavyotawala na vile vya upinzani vitakuwa na mabadiliko makubwa.
Aidha, akasema kuwa Muungano wa Tanzania utaendelea kudumu licha ya watu kulalamikia kasoro kadhaa kila kukicha.
Mtoto wake naye akaanza kutabiri...
Saturday, January 14, 2012
UTABIRI WA MWAKA 2012
Kila
mwaka aliyekuwa mnajimu na mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati,
Sheikh Yahya Hussein alikuwa akifanya utabiri. Mwaka huu Januari 13,
mrithi wa kazi zake Maalim Hassan Yahya Hussein amechukua nafasi yake na
kufanya utabiri ambao umesambazwa katika vyombo vya habari na nasi
tunawaletea kama ifuatavyo:
Mwaka 2011 ulianzia siku ya Jumamosi ambayo inatawaliwa na Sayari ya Zohal na Nyota zake ni Mbuzi na Ndoo. Sayari hii Nyeusi na
inahusika na mambo mabaya, kama vile ndoa kuvunjika, vita, kuvunjika
kwa vitu au kuanguka kwa Serikali, fitina, magomvi, vifo vya waandishi
na watu maarufu, shida nyingi, maradhi mengi, hujuma, kuongezeka kwa
hofu mabalaa kwa wasafiri wa bara na baharini, mvua kubwa maafa na
majanga ya asili.
Katika utabiri wake alioutoa Februari mwaka jana miezi mitatu kabla hajafariki aliyekuwa Bingwa wa Utabiri hapa nchini Marehemu Sheikh Yahya Hussein alielezea
mambo mengi kuhusiana na hayo na mengi sana yametokea na bado
yanaendela kutokea, kubwa kabisa ni kuanguka kwa Serikali kadhaa za
Kiarabu, na kukimbia kwa viongozi wa nchi za Tunisia na Misri, kuuwawa
kwa kiongozi wa Libya Kanali Muamar Gaddafi, kiongozi wa Yemen kupata
matatizo na mpaka hivi sasa Syria bado kuna matatizo.
Alitabiri pia majanga ya asili na maafa kutokea sehemu mbali mbali za dunia, vifo vya Waandishi wa habari ambao mpaka sasa waliofariki na wanaofahamika hapa kwetu ni
- Hassan Mgenyi
- Juma Penza
- Dan Mwakiteleko
- David Wakati
- Maulid Hamad Maulid
- Adam Lusekelo
- Joseph Kaitani Asama
- Alfred Ngatezi
- Halima Mchuka
- John Ngahyoma
- Mwinyimvua Ahmed
Vile vile alitabiri kuhusu majanga kwa wasafiri wa bara yaani nchi kavu na baharini na tumeona maafa ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander, na ajali zilikuwa nyingi.
Alitabiri
pia kutokea kwa Mafuriko sehemu mbali mbali za dunia na mpaka hapa
kwetu Dar es Slaam tulikumbwa na mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya
Watanzania zaidi ya 40 na matabiri mengine mengi ambayo
hatujayaorodhesha yalitokea.
Kwa
ujumla mengi aliyoyatabiri kutokea katika mwaka 2011 yametokea na
mengine yanaendela kutokea mpaka Mwaka wa kinyota utakapomalizika mnamo Machi 20, mwaka huu (2012).
Mwaka huu wa 2012 umeanzia siku ya Jumapili, siku hii inatawaliwa na Sayari ya Jua ambayo nyota yake ni moja tu nayo ni nyota ya Simba.
Sayari hii inahusika na, kufanyiana kiburi, kutumia nguvu, ufahari, mambo yote yanayohusiana na Siasa, udereva, ufundi wa mambo ya moto na magari
Tarehe 20/5/2012 ambayo pia itakuwa siku ya Jumapili Jua
litapatwa kiasi (Partial Eclipse) kwa mara ya kwanza na kupatwa huku
kwa jua kutaonekana kwa upana wa kati ya kilometa 240 na 300 na sehemu
zitakazohusika ni Asia Mashariki, Kaskazini mwa bahari ya Pacific na
Magharibi ya Marekani.
Tokyo (Japani) ambayo iko kilometa 10 mwa mstari wa kati itashuhudia kupatwa huku kwa dakika 5 na sekunde 26.
Mwisho wa Mwaka huu tarehe 13/11/2012
ambayo itakuwa siku ya Jumatano ambayo inatawaliwa na sayari Mercury
jua litapatwa kamili (Total Eclipse) watu wanaoishi Australia na Bahari
ya Pacific ndio watakaokumbwa na kiza cha kupatwa na jua.
Kwa
sababu huu mwaka umeanzia na siku ya Jumapili na siku hiyo inatawaliwa
na sayari ya Jua, hatari za kupatwa huku zitaikumba Dunia moja kwa moja.
Mwaka huu una namba 12 (2012)
ambayo kinyota inaashiria, uadui wa kisiasa na kijamii, watu kulipizana
visasi na upinzani kupata nguvu, wanyonge kudai haki zao kwa nguvu na
mafanikio ya wataliwa dhidi ya watawala.
Vile
vile inaashiria kutokea kwa vimbunga, kusikika sana kwa habari za
Waandishi au Waandishi kupata madaraka makubwa katika siasa.
Pia ni mwaka ambao kutazuka Moto sehemu mbalimbali duniani na kuleta madhara makubwa na hiyo inaashiria kuzuka kwa magomvi baina ya viongozi wa kisiasa na wananchi.
Pamoja
na hayo tutasikia habari za kutokea matetemeko ya ardhi yatakayoleta
madhara makubwa, Wasanii kupata kwa kuchaguliwa au kuteuliwa kushika
nafasi za kisiasa na kutokea kashfa kubwa kwa viongozi zitakazohusiana
na masuala ya fedha au mambo ya ufisadi au wizi mkubwa utakaoshitua
watu.
Kutokana na hayo:-
Natabiri kutokea
shida kubwa za Majanga ya Asili na kuongezeka kwa maradhi au kufumuka
maradhi yasiyojulikana na kuiletea Dunia wasiwasi mkubwa.
Natabiri, Uadui
mkubwa kutokea kati ya viongozi wa nchi na wananchi kwa ujumla na
kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na viongozi kuvuliwa madaraka.
Natabiri kutokea vifo vya Mahakimu na Majaji na Wanasheria maarufu katika nchi za Mashariki, Tanzania ikiwemo
Natabiri kutokea vifo vya Mawaziri na Wizara zao kupatwa na matatizo.
Natabiri Kutokea kwa Njaa kali kutokana na Jua kuwa kali na ukame kukumba nchi.
Natabiri tutasikika habari za wanawake kuuwa waume zao na watumishi kuwauwa mabwana wanaowafanyia kazi.
Natabiri Mwaka huu ni mwaka ambao utatawaliwa na vifo vitakavyoshtua watu wengi.
Natabiri:
Huu ni mwaka wa vijana kushika nafasi za uongozi na kuchukua madaraka
na wazee wengi watapoteza nafasi zako hasa katika chaguzi mbali mbali
zitazofanyika.
Natabiri malumbano makubwa, vurugu na magomvi kwenye mabunge, wabunge watagombana bila kujali itikadi za vyama vyao.
Natabiri mivutano iliyopo hivi sasa katika vyama haitaharibu vyama husika hasa katika vyama vya CUF,NCCR na CCM.
Natabiri: Kutokea vifo vya ghafla kwa viongozi wa kisiasa waliopo madarakani au Serikalini.
Nashauri:- Serikali iwe makini katika utekelezaji wa shughuli zake kwa sababu kunaweza kuzuka mgogoro mkubwa utakaotikisa nchi.
Natabiri, Rais
Jakaya Kikwete kupata umaarufu mkubwa wa kisiasa mwaka huu na
atashirikisha wapinzani katika shughuli kadhaa za kiserikali hivyo nyota
yake kuzidi kung’aa kitaifa.
Natabiri baadhi ya viongozi wa dini kukumbwa na kashfa mbaya na za kutisha zitakazovunja hadhi zao.
Maalim Hassan Yahya Hussein
S.L.P 21250 Simu 0754672464
Monday, January 14, 2013
UTABIRI WA HASSAN YAHYA HUSSEIN 2013
Ndugu wanahabari wa vyombo vyote vya habari hapa nchini
Assalaam Aleykum,
Hassan Yahya Hussein |
UTANGULIZI:
Tarehe
kama ya leo, mwaka 2012 ambayo ilikuwa siku ya Ijumaa nilikuiteni hapa
kuzungumzia Utabiri wa mwaka 2012 ambao kinyota bado unaendelea. Utabiri
huo utakoma Machi 20, Mwaka huu 2013 kwa maana tarehe 21 Marchi ndio
mwaka mpya wa kinyota na ambapo ndipo Utabiri rasmi wa mwaka 2013
utakapoanza.
Wengi
wenu mmeona na Ni imani yangu na yetu kwamba asilimia 95 ya Utabiri
tulioutabiri Januari 13 mwaka 2012 umefanikiwa na yaliyotabiriwa
yametokea kama tulivyouweka hadharani. (Nakala ya Utabiri huo
nimeambatanisha)
Bila
kujisifu, hali hii inaoonesha wazi kuwa Muasisi wa kazi hizi katika
Afrika ya Mashariki na Kati na Dunia nzima kwa ujumla, Sheikh Yahya
Hussein ambaye kwa sasa ni Marehemu, alirithisha kazi zake hizi kwa mtu
Jadidi, Mweledi na Makini kama alivyokuwa akimuomba Mwenyezi Mungu siku
zote katika uhai wake.
Kabla sijatangaza rasmi Utabiri wa Mwaka huu, kwanza kabisa nitazungumzia namna mwaka 2013 Mwaka wa 2013 umeanzia siku yaJumanne, siku hii inatawaliwa
Na Sayari ya Mars au Mariikh ambayo nyota zake ni mbili nazo ni nyota ya Punda au Aries na Nge ambayo ni Kinyota hii nyota ya Punda ni nyota ya mwanzo ambayo ndio kichwa na kama nyumba ya Mwanzo na maana yake ni Mwanzo wa jambo, Anza jambo,Tangaza jambo au kupata mafanikio.
Nyota ya Pili ni NGE au Scorpio ambayo Kinyota ni nyota ya Nane au Nyumba ya Nane, nyota hi iinaashiria, Hasira, kupotea, Kuachana, kukimbiwa, Maziko,Vifo na Wasiwasi
Kwa
kawaida Mwaka ukianzia siku ya Jumanne unaashiria Matatizo makubwa,
ikiwa ni pamoja na kuongezeka Vita sehemu mbali mbali za dunia,
Viongozi wa kidini, kisiasa, na kijamii kuugua sana na wengine kufa,
kutokea moto katika miji mikubwa, ukame, ukosefu wa Maadili, wafanyakazi
kuwapiga mabosi wao, uongo kuwa mwingi kwa maana propaganda, umbeya,
masengenyo, mashujaa kufariki, mazao kupungua, ajali kuwa nyingi za bara
na baharini na angani, watu kuwa na khofu na watu wengi kuuwawa
Kwa upande mwingine inaashiria biashara kuongezeka na neema kuwa kubwa na watu kufaidika katika biashara
Pamoja
na hayo kutakuwa na Matatizo ya maradhi kwa watoto hasa kuugua vifua na
maradhi ya kichwa, wanawake wajawazito kupoteza maisha kwa wingi au
kuzaa kwa matatizo makubwa
Kwa
upande wa Siasa Mwaka ukianzia siku ya Jumanne basi hutokea kwamba
Viongozi wa Kidini na kisiasa kutoa matamshi ya utatanishi na
kusababisha khofu kubwa na hata watu kupigana lakini hali hiyo hudumu
kwa muda mfupi, baadhi ya viongozi hukaa pamoja na kukubaliana mambo
baina yao na kurejesha hali ya utulivu na amani
Mwaka
huu wa 2013 Mwezi utapatwa mara tatu tarehe 25/4/2013 ambayo itakuwa
siku ya Alkhamisi, tarehe 25/5/2013 ambayo itakuwa siku ya Jumapili na
tarehe 18/10/2013 siku ya Ijumaa
Jua
lenyewe nalo lipatwa mara mbili tarehe 10/5/2013 ambayo itakuwa siku ya
siku ya IJumaa na tarehe 3/11/2013 itakuwa siku ya jumapili
Siku
hizi za Alkhamisi Ijumaa na Jumapili ambazo Jua na Mwezi utapatwa zina
athari ya moja kwa moja kwa maisha yetu, Alkhamisi inatawaliwa na
Sayari ya Jupite r ambayo inahusika na Serikali, Wizara. Safari, na Magomvi,
Siku
ya Ijumaa inatawaliwa na Sayari ya Venus au Zuhura ambayo inahusika na
Muafaka, Urafiki,, Mapenzi, Ndoa, Masikilizano, Mapatano, Mambo ya
Muziki, Wasanii, na Michezo.
Siku
ya Jumapili inatawaliwa na Sayari ya Jua ambayo inahusika na Kiburi,
Nguvu, Ufahari, Kuona haya, wanasiasa, madereva, mafundi wa mambo ya
moto na magari.
Huu Mwaka wenyewe 2013 namba mbili za mwisho 13 ukizijumlisha unapata 4 ambayo ni nyota yaKaa au Cancer ambayo
inahusikana ,Kilimo, Mapenzi, Unyonge, Kufanya vitu kwa vishindo, Siri
na kuvumbuka kwake, Kuvunjika biashara na kutimia kwa haja, Mvua na
Mafuriko na Majanga ya asili.
KUTOKANA NA HAYO MAELEZO:-
Hali ya Kijamii:
Natabiri:
kwamba katika Mwaka huu wa 2013 Ndoa nyingi zitavunjika. Watu wengi,
wakiwemo Mawaziri na Viongozi Waandamizi wake kwa waume, watajikuta
katika kashfa ya Ngono, Kufumaniwa au kufumania na kupigana kiasi cha baadhi yao kuuawa.
Natabiri; Kuwa maisha katika mwaka huu yatakuwa mazuri, lakini kwa Watanzania watakaojifunga mikanda kuelekea katikati ya mwaka 2013.
Natabiri: Maradhi
ya watoto kuongezeka katika Mwaka huu wa 2013 na hasa ya kifua na
kichwa. Wanawake wengi wajawazito watapoteza maisha kwa kujifungua na au
kuzaa kwa matatizo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana.
Natabiri: Ajali zitakuwa nyingi, kuchafuka kwa bahari kutakuwako kwa wingi na kutakuwa na hofu ya watu wengi kuuawa.
Natabiri: Kutokea
kwa mioto mikubwa kwenye miji mikubwa, Njaa kuongezeka, ukosefu wa
maadili, wafanyakazi kuwapiga mabosi wao, uongo mwingi kwa maana ya
propaganda,
Natabiri: Umbeya utakua kwa kiwango kikubwa mwaka huu wa 2013, pamoja na masengenyo.
Natabiri vifo vya Mashujaa au wale watakojiona ni mashujaa.
Natabiri:
wingu zito la vifo vya ghafla kwa watunzi wa hadithi na vitabu,
Waandishi wa habari, Wanasiasa na Wasanii na muda huu itakuwa mbaya
zaidi ya mwaka jana.
Hali ya Kisiasa:
Natabiri: Viongozi
wengi wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wenyeviti wa vyama na
Makatibu wao watatoa matamshi ya utatanishi na kusababisha khofu na
mitafaruku mikubwa itakayowafanya watu kupigana.
Hata
hivyo, hali hiyo itadumu kwa muda mfupi. Kwani baadhi ya viongozi
watalazimika kukaa pamoja na kukubaliana mambo baina yao na kurejesha
hali ya utulivu na amani.
Natabiri: Wabunge
wengi katika Bunge la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania wataungana
katika masuala yatakayohusu Utaifa bila kujali itikadi zao za kivyama
au kimajimbo. Hata hivyo, nyota zinaonesdha kuna baadhi ya wabunge
wataanguka Bungeni wakati wa majadiliano.
Kinyota haionekani kuwa kutakuwa na athari lakini itapaswa kufanyika juhudi za ziada kuokoa maisha yao.
Natabiri Rais
Jakaya Kikwete maarufu kama “JK” kufanya mambo ya ajabu na
yasiyotabirika na ataungwa mkono kwa asilimia 100 na wananchi wote wa
Bara na Visiwani.
Natabiri JK atatenda maamuzi magumu katika mwaka 2013 kiasi cha dunia kushangaa.
Natabiri: JK
ataendelea kupata wasaidizi sadifu hasa kwa upande wa Uwaziri. Vile
vile nyota za Mawaziri Harrison Mwakyembe, John Pombe Magufuli na
Khamisi Kagasheki zitazidi kungara Mwaka huu na kuungwa Mkono na
Wananchi
Natabiri JK
ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa Utaifa kuliko
watangulizi wake. na atashirikiana zaidi na Wanasiasa na viongozi wa
dini kuondoa mtikisiko wa uvunjifu wa amani uliokuwapo nchini mwaka
jana.
Natabiri Chama
kimoja cha siasa hapa nchini kuchochea kujitenga na kuunda Taifa lake.
Hata hivyo, kusudio hilo halitafanikiwa. Kwani litapingwa na Watanzania
wote kwa kauli na vitendo.
Natabiri:. Natabiri Tanzania kushinda kwa kishindo kwenye mgogoro wake na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa bila kupigana vita.
Hali ya Kibiashara:
Natabiri: Mauzo
ya bidhaa yataongezeka na kuongeza neema na watu kufaidika katika
biashara. Pia mwisho wa mwaka huu wa 2013 mvua zitaongezeka na mazao
yatakuwa mengi.
Natabiri: Wafanyabiashara wengi na hasa wajasiriamali kufanikiwa katika kazi zao.
Natabiri: Neema itawaangukia wajasiriamali wa aina zote hapa nchini kwa mwaka huu.
Natabiri wawekezaji wengi zaidi mwaka huu watajikita kwenye biashara ndogondogo kuliko ilivyokuwa katika miaka iliyopita.
Natabiri: Sakata
la gesi ya Mtwara litatulia na kumalizika kwa amani katika mwaka huu wa
2013 kwa wananchi wote kuungana na kuunga mkono matumizi yake kwa faida
zaidi ya Taifa badala ya jimbo au majimbo
Natabiri: Nchini Kenya ambao ni Majirani zetu Muungano wa CORD ukiongozwa
na Raila Odinga kushinda uchaguzi wa Kenya ambao utakuwa wa amani na
utulivu na kuwashinda Kina uhuru Kenyatta na Ruto na Muungano wao wa JUBILEE na ule wa Musalia mudavadi unaoitwaAMANI
Maalim Hassan Yahya Hussein
13/1/2013 Jumapili
Ushindi wa Uhuru Kenyatta wamuumbua Maalimu Hassan Yahya Hussein
Utabiri wa Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mrithi wa aliyekuwa Mnajimu Mkuu Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein alioutoa tarehe 13/1/2013 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ushindi wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Mh. Raila Odinga katika uchaguzi mkuu uliofanyika march mwaka huu umeota mbawa kutokana na ushindi alioupata Uhuru Kenyatta katika uchaguzi huo.
Kati ya mambo aliyoyatabiri ni Nyota za utendaji kazi wenye ufanisi serikalini za mawaziri; Dk. Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), John Magufuli (Ujenzi) na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), zilimetabiriwa kuwa zitazidi kung’ara na kuungwa mkono na wananchi.Kadhalika, Rais Jakaya Kikwete, akitabiriwa pia kufanya maamuzi magumu yatakayoishangaza dunia, katika mwaka huu 2013.
Source: NIPASHE tarehe 14/1/2013.
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/414513-ushindi-wa-uhuru-kenyatta-wamuumbua-maalimu-hassan-yahya-hussein.html
No comments:
Post a Comment