Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 24 January 2014

MTUHUMIWA AJIPAKA KINYESI KUWATOROKA POLISI

MTUHUMIWA AKIENDELEA KUZOA KINYESI CHINI YA ULINZI

NI HATARI AKIHAKIKISHA PANAKUWA SAFIII


DUUU AISEEEEE


HAPA AKIHITIMISHA KUZOA.
BAADA YA KUMALIZA KUZOA HAPA AKIPELEKWA MAHAKAMANI AKASOMEWA KOSA LA KUTOROKA NA KUPIGWA MIEZI SITA WAKATI KESI YAKE ALIYOMPELEKA 
IKIHAIRISHWA
.Mwandishi , Wiliam Bundara wa matukiodaima.com Mwanza
 ...................................................
UKIULIZA   kwanini  wapo  watakaosema kwa  sababu  ila ukihoji imefikaji wapo  watakaosema imefika ila kubwa kuwa mbinu  hukotea baada ya kubanwa na kutafuta  jinsi ya  kujinasua na hivi  ndivyo  ilivyo kuwa kwa Mahabusu mmoja aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa kioja cha mwaka kwa kujaribu kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.

Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi kilichokuwa kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na askari alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi.

Askari mwingine mwenye cheo cha sajenti, ambaye alikuwa akihushughulika na huduma nyingine mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa kupambana na mikasa na vioja kama hivyo vya mahabusu wanao kula njama za kutaka kutoroka aliamua kula naye sahani moja kwa kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata.


Baada ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo, kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha binadamu alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya kumaliza kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa la kula njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili awali ikiahirishwa.

CHANZO: Matukiodaima

No comments:

Post a Comment