London, England. Chelsea imepata hasara ya Pauni 49.4 milioni kwa mwaka ulioisha Juni 2013.
Mapato ya Pauni 255.8 milioni ni rekodi kwa klabu hiyo lakini kutolewa katika hatua za makundi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita kuliwaathiri.
Mapato hayo ukichanganya na faida ya Pauni 1.4 milioni waliyopata mwaka uliopita yanaangukia katika viwango viliyowekwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa).
Mapato yao ya kibishara yamepanda kutoka Pauni 67 milioni hadi Pauni 79.6 milioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.
Chelsea ilishinda Kombe la Ligi ya Europa mwaka 2013 lakini ilipata zawadi ndogo kulinganisha na ile iliyopata mwaka 2012 kwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“`Kwa Chelsea kupata rekodi ya mapato yake licha ya kutolewa katika hatua za makundi za Ligi ya Mabingwa Ulaya inaonyesha kuwa tumeweka biashara yetu vizuri na tuna mpango mzuri kwa maendeleo ya baadaye,” alisema Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ron Gourlay.
“Falsafa yetu ni kwamba tunajenga mafanikio yetu kwa kufanya vizuri uwanjani na kwa muundo wa kikosi chetu tutafaidika kwa miaka mingi ijayo”.
Faida kwa Chelsea ya mwaka uliopita ilikuwa ni ya kwanza tangu klabu hiyo imilikiwe na tajiri Roman Abramovich mwaka 2003.
Faida hiyo ilitokana na mauzo ya wachezaji na ya kampuni ya utangazaji ya BSkyB kuondoa hisa zake katika makubaliano ya kihabari na klabu.
Misimu miwili iliyopita ilikuwa ndiyo ya kwanza kupimwa nakungaliwa mapato ya klabu na Uefa.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bruce Buck alisema Uefa inafanya jambo zuri kwa utaratibu wake na wao wamejipanga ili kuhakikisha kwamba lengo lao la kunyakua vikombe linabaki palepale.
http://www.mwananchi.co.tz/Michezo/Chelsea-yapata-hasara-England/-/1597534/2132206/-/7492l1z/-/index.html
No comments:
Post a Comment