Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 30 September 2016

SERENGETI WAJIFUA ILI ‘KUIZIKA’ CONGO JUMAPILI

CONGO TUTAWAZIKA HAPA...
Ndivyo anavyoonekana kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.

Huyo ndiye Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kuonyesha uwezo wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa jahazi. Akikosa kufunga huwa ni kama bahati mbaya.
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Baadhi ya vigogo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, kutoka kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu, Pelegrinus Rutayuga na Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.

No comments:

Post a Comment