Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 September 2016

KUONA SERENGETI NA CONGO –BRAZZAVILLE BURE, VIJANA WAJAZWA NOTI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa ofa kwa wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016 katika mchezo wa mpira wa miguu utakaozikutanisha timu za vijana taifa za Tanzania na Congo-Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka. Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.

Nape alitoa ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi Septemba alipata kifungua kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako alitoa Sh 200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti Serengeti Boys ambao walichangia Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka kwa wadau wengine.
Nape ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”
Kuingia bure kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal Malinzi amemshukuru Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo imelenga kutoa hamasa kwa Watanzania kwenda kushangilia timu yao.

Katika mchezo huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema kwamba amemaliza kila kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani leo kuishangilia timu yao, utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako mpiga kipenga atakuwa Nelson Fred akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie wakati mwamuzi wa akiba akiwa Allister Barra. Kamishna wa mchezo atakuwa Gladmore Muzambi kutoka  Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment