Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 22 September 2016

WAZIRI JAFO AHIMIZA SOMO LA HISABATI





Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akitizama vitabu wakati akitembelea  katika sehemu za maonyesho zilizoandaliwa kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.




Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akitizama moja ya maonyesho ya  mafunzo yanayotolela kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

 Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akizungumza katika  semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.




Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka CHAHITA kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Na Nasra Mwangamilo
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo amesema ni muhimu somo la hisabati likatiliwa mkazo na wazazi, wanafunzi na walimu ili kuwapata wataalamu wabobezi kwenye somo hilo.
Naibu Waziri aliyasema hayo wakati akitoa hotuba katika ufunguzi wa semina ya mafunzo ya hesabu iliyoandaliwa na chama hicho itakayoendelea kwa muda wa siku sita katika moja ya majengo ya ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma .
“Nimefarijika sana kwa ninyi kunipa fursa kuwa nanyi katika siku ya leo kwani najua lengo kubwa la semina yenu lakini pia lengo kubwa la chama chenu ni kuhakikisha taaluma ya hesabu inatamalaki katika nchi yetu ikiwa lengo kubwa ni kupata wataalamu wazuri waliobobea katika nyanja hii,” alisema Mh. Jafo.
Mh. Jafo aliongeza kuwa kwa sasa ni muhimu kufanya tathmini ni kwa namna gani wanaweza kuhakikisha ufaulu wa hesabu unaongezeka kwa wataalamu kuweza  kubuni mbinu tofautitofauti za ufundishaji wa somo hilo na kuhakikisha mbinu hizo zinatawanyika katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa katika kulisoma somo hilo.
Akiongea kwa niaba ya CHAHITA mwenyekiti wa chama hicho Dk. Said Sima alieleza malengo ya chama hicho kuwa ni kuwaendeleza na kuwapa mafunzo  walimu katika vijiji 489 na wilaya zote nchini ili kuhakikisha wanafundisha wanafunzi somo la hisabati kwa dhana ya nadharia na vitendo.
 Pia Dk. Sima alitoa mapendekezo kwa Mh. Naibu Waziri  ambayo ni kuongezewa malipo kwa walimu wa somo la hesabu, Serikali kubuni mpango kwa wanafunzi wa elimu ya juu ya ualimu wa somo la hesabu kuwa wanasaidia kufundisha katika shule za jirani na vyuo wanavyosoma na kubuni mpango wa walimu wa somo hilo kuwa wanapewa muda wa ziada wa kuwafundisha wanafunzi.
Chama hicho ambacho kwa sasa kina miaka 51 tangukilipo anzishwa tarehe 11 ya mwezi wa kwanza mwak 1966 kimeanza semina hiyo leo ikiwajumuisha walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka ndani nan je ya Dodoma, Walimu kutoka Vyuo vikuu, Wawakilishi kutoka NACTE  na NECTA na wawakiliski kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT). 

No comments:

Post a Comment