Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
Na Eleuteri Mangi na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewataka wadau wa habari na wananchi kwa ujumla kutoa maoni juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari wa mwaka 2016 uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni leo mjini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhairishwa Bunge, Waziri Nape amesema kuwa muswada huo unalengo la kuboresha tasnia ya habari ili kuweza kurahisha utendaji kazi wa wanahabari na kuifanya tasnia hiyo kuheshimika nchini.
“Ombi langu kwa wadau wa tasnia hii wausome vizuri muswada huo na kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni yao ili tuwe na sheria itakayoleta magezuzi na kukuza tasnia ya habari” amesema Waziri Nape.
Waziri Nape amewataka wadau wa habari kuendelea kusoma muswada huo ili kuweza kupata mapendekezo ya namna ya kuifanya sheria hiyo kuwa bora kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.
Aidha, Waziri Nape amewaahidi wadau wa habari kukutana nao mara kwa mara wakati wa kutoa maoni na mapendekezo yao yatakayosaidia kuboresha mazingira ya wanahabari nchini ili waweze kufanya kazi yao ipasavyo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma.
Vile vile, Waziri Nape amewapongeza waandishi wa habari kwa kushiriki vema katika kuhabarish umma kuhusu mkutano wa Bunge uliohitimishwa leo na kuahidi kuendelea kushirikiana nao wakati wote.
No comments:
Post a Comment