Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 22 September 2016

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA STENDI KUU UBUNGO NA KIBAHA, AGUNDUA MABASI MABOVU, AYAZUIA KUSAFIRI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwauliza abiria wa Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, maswali mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wanaposafiri. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua mikanda katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akioneshwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora kwa ajili ya kusafirisha abiria. Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo lizuiwe kufanya safari na pia kuchukuliwa hatua kali kwa Mmiliki wa basi hilo pamoja na Dereva. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo ya mizigo yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo, madereva hao walilalamika kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi hiyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akishuhudia Dereva wa Basi la Tahmeed (kulia) akipimwa kilevi na Trafiki Nuru Mvungi kabla ya Basi lake kuruhusiwa na safari. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akihoji usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto wawili jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia wananchi wa Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani mara baada ya kumaliza ukaguzi wa mabasi mabovu pamoja na madereva ambao hawana leseni. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

*****************************************************************************

Na Mwandishi Wetu, MOHA
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amefanya ziara ya kushitukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Stendi ya Kibaha, mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo, alilizua basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF pamoja na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria.
Masauni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani akiwa na Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, aliwasili katika Stendi hiyo ya Ubungo saa 2:16 asubuhi na kuanza ziara hiyo ambayo aligundua baadhi ya mabasi yaendayo mikoani hayana viwango na ubora wa kusafirisha abiria.
Aidha, Masauni alitoa agizo kwa askari wa usalama barabrani pamoja na viongozi walioko katika kituo hicho, kuboresha mfumo wa ukaguzi wa mabasi hayo kuwa wa kiwango kinachoridhisha ili kuzidi kupunguza ajali za barabarani pamoja na kuzuia baadhi ya mabasi yaliyoonekana kuwa na ubovu zaidi kufanya safari ndefu lakini pia kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wamiliki wa mabasi hayo na madereva wake.
Katika ziara hiyo Masauni ametoa wito kwa abiria kutokua sehemu ya kusababisha ajali kwa kutaka dereva kukimbia sana lakini pia kutoa ushirikiano hasa katika kutoa taarifa polisi pamoja na Chana cha Kutetea Abiria (CHAKUA) juu ya madereva wanaoendesha kwa spidi ambayo ni hatari kwa maisha yao lakini pia kuepuka kupanda magari yasiyokuwa na mikanda, na viti vilivyolegea.
Lengo la Serikali na viongozi mbalimbali ni kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua ama kuisha kabisa hivyo haiwezi kufumbia macho makosa yanayoweza kusababisha ajali, “Pesa inatafutwa lakini roho haitafutwi hivyo ni vema kuwa makini barabarani, alisema masauni na kufafanua kuwa;
“Mkakati wa kuzuia ajali ni kuwa na mfumo endelevu wa kuzuia ajali za barabarani na si ya muda mfupi hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi havitakoma kuongeza nguvu ili kumaliza tatizo hilo na kuwachukulia hatua kali wamiliki na madereva wanaoendesha mabasi mabovu hivyo kuhatarisha usalama barabarani.”
Aidha, Masauni amewataka madereva wote pamoja na makondakta kuhakikisha abiria wote wamefunga mikanda kabla ya kuanza safari pia kuendesha kwa kuzingatia alama za barabarani ili kuzidi kupunguza ajali kwani dhamana ya maisha yao iko mikononi mwao.
Idadi kubwa ya abiria kwenye vituo hivyo vya mabasi wameonesha kuridhishwa na mwendo wa mabasi yanapokua barabarani lakini wameiomba Serikali iendelee kufuatilia madereva wanaokiuka sheria za usalama wa barabarani.


   

No comments:

Post a Comment