Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba
NA IDARA YA HABARI- MAELEZO
Mhashamu
Baba Askofu Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, amesema
Serikali ya Awamu ya Tano ina nidhamu ya kazi ya hali ya juu na udhibiti wa
matumizi ya fedha za serikali .
Hayo ameyasema askofu huyo wakati akifanya
mahojiano na Idara ya Habari Maelezo, kwa njia ya simu.
Askofu
Kilaini aliainisha maeneo kadhaa yanayoifanya Serikali ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuonekana ni ya kipekee, na kusisitiza kuwa ni yenye utendaji
wa kusema na kutenda, ambao umefuta utani kutoka kwa jirani zetu Malawi
na Kenya , kuwa ukitaka maneno nenda Tanzania, alisema Kilaini .
Aidha,
Askofu Kilaini alieleza kuwa utendaji WA Serikali ya awamu ya Tano umegawanyika
katika sehemu tatu ambazo ni nidhamu katika kazi, udhibiti wa fedha za
serikali, dhana ya kusema na kutenda na kuwajibika kwa watumishi wa serikali.
Kilaini
ameongeza ni dhahiri watumishi wa Serikali kuwajibika kuwahi makazini kufanya
kazi bila kulalamika. Akitoa mfano
Askofu Kilaini alisema hapa Tanzania nidhamu ya kazi ilikuwa enzi za serikali
ya awamu ya kwanza, nanukuu “angalia wakati wa Waziri Mkuu Marehemu Edward
Moringe Sokoine na hata Mheshimiwa Lyatonga Mrema alijaribu lakaini haikuwa endelevu.
Akisisitiza
juu ya nidhamu ya kazi Askofu Kilaini alieleza hali halisi ya shule za Msingi
na Sekondari Mkoani Kagera, kuwa sasa walimu wanawahi kazini bila kutoa
visingizio na kuingia darasani na kufundisha. Siku za nyuma walikuwa wakienda
shule kwa muda wanaopenda na hakuna aliyekuwa anawajibika kuwauliza au hata
kuwachukulia hatua.
Askofu
kilaini aliwashangaa wanaobeza fedha za ruzuku kutoka serikalini inayopelekwa
kwenye shule za Msingi na Sekondari akisema wanafanya makosa makubwa kubeza
kwani, ukiacha wale waliosoma enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,
shule hizo hazijawahi kuwa na ndoto ya kupata fedha kutoa serikalini, hivyo
hiyo fedha ambayo wengine wanaibeza ni mkombozi mkubwa kwa shule zetu na nina
uhakika kiwango cha elimu kitaboreka.
Muelekeo
wa serikali kudhibiti fedha za serikali njambo kubwa sana angalia suala zima la
watumishi hewa, fedha hizo zimepotea, zingeweza kufanya mambo makubwa kwa
wananchi wanyonge vijijini. Ni lazima tumshukuru kwa jambo hili limesaidia kuwa
makini kwa watumishi waliopewa dhamana na jambo husika.
Akiongezea
Askofu Kilaini alielezea dhana ya Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt John Pombe Magufuli ya kunena na kutenda imempa heshima kubwa sana hasa nje
ya mipaka ya Tanzania kama Kenya na Malawi ambao walikuwa wanaibeza Tanzania
kuwa nchi ya maneno maneno bila kutekeleza sasa dhana hiyo haipo. Anachosema
Rais anatenda na kusema hakika msemo wake wa HAPA KAZI TU ni dhana ya matendo.
Askofu
Kilaini aliwaasa vyama vya upinzani kufanya maandamano hasi na sio chanya,
alihoji wajiulize faida inayotokana na maamuzi wanayoyafanya kama yana tija kwa
Taifa. Aliongeza kwa kusema maandamano hasi ni kama kupinga mauaji ya Albino
unyanyasaji wa kijinsia na mambo kama hayo.
Mahojiano hayo
yaliyofanywa na Idara ya Habari – MAELEZO ilipata fursa ya kufamya mahojiano na
Mhashamu Baba Askofu Methodius Kilaini Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba yaliyofanyika
kwa njia ya simu tarehe 27/08/2016 Juu ya Utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano
ni kama yafuatavyo:
SWALI: Baba Askofu;
Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani tangu mwezi Novemba 2015 kwa sasa
takriban miezi kumi. Je, unalipi la kueleza wananchi juu ya utendaji wa
serikali hii?
JIBU: Mimi binafsi nadhani na
watu wengi wanafurahia utendaji wa Mheshimiwa Rais ambapo ni utendaji wenye upya
wenye kuelekea mahali papya kwa ufupi Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ana
muelekeo wake ambao utatufikisha mahali pazuri. Unajua kulikuwa na utani kutoka
kwa majirani zetu Kenya na Malawi wanatutania wakisema ukitaka maneno nenda
Tanzania ambao hawafanyi kazi, kwa sasa utani huo hauna nafasi.Utendaji huu
ninautazama katika maeneo ya fuatayo:
(a) Nidhamu katika kazi kwa
sasa inaonekana, siku za nyuma nidhamu ilipotea kabisa nidhamu hii
ninayoiongelea ilikuwepo wakati wa utawala wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, hapo katikati tulipoteza nidhamu hii akitoa mfano alisema
kwa sasa walimu wanawahi mashuleni na
kuingia darasani kufundisha,. Watumisi
wote kwa ujumla wanaenda kazini wanawahi na wanakaa kazini na kufanya kazi.
Hapo nyuma walimu wamekuwa wakienda
mashuleni wanavyotaka hawafundishi na hakuna mtu wa kuwawajibisha juu ya hilo,
ukiangalia wakati wa awamu ya kwanza Waziri Mkuu Marehemu Edward Sokoine
kulikuwa na nidhamu ya kazi ya hali ya juu. Hata nyakati za Mrema alijaribu
hata kuondoa viti kwa wale wanaochelewa maofisini lakini bahati mbaya
halikupata uungwaji mkono likaishia hivi hivi Bila kazi huwezi kupata maendeleo
hivyo ni lazima tufanye kazi kwa bidii na nidhamu.
(b)
Udhibiti
wa fedha ambazo zilikuwa nyingi mitaani, pia fedha hiyo ilipatikana kwa kazi za
kubabaisha. Napenda kukiri sasa ipo nidhamu ya fedha ya Serikali. Hapo nyuma
nidhamu ya fedha ilikuwa haipo mfano
Wizara, Taasisi na Idara za serikali zilikuwa zinatafuta njia za kula fedha ya
serikali bila tija kama kufanya semina , makongamano, warsha baada ya hapo
wanahalalisha kugawana fedha wanavyopenda. Semina siku moja wataandika siku tatu,
watakodi ukumbi wa hoteli wa bei ya juu sana bila sababu na matumizi mengine
yasiyo ya lazima.
Kwa Mheshimiwa Rais Magufuli ameweza kuziba mianya
yote kama vile kubaini watumishi hewa na kuelekeza fedha zilizookolewa kupelekwa
maeneo muhimu kwa maendeleo ya wananchi kama shule za kata ambao hawakuwahi
kufikiri katika maisha yao wanaweza kupata fedha za ruzuku ya serikali, watu
wamekuwa wakisema fedha hizo ni kidogo lakini wakumbuke shule hizo hazijawahi
kupata kitu kama hicho walikuwa wakilumbana na wazazi kutoa fedha na matokeo
yake wanafunzi wengi waliacha shule kwa sababu wazazi walishindwa kulipa karo
ya shule.
Nina
hakika kwa sasa elimu itaboreka na kujijenga kidogo kidogo, hakuna haja ya kubeza juu ya jambo hili. Wale
wanaobeza wanafanya dhambi kubwa wasubiri waone nini matokeo ya utaratibu huu.
(c) Dhana ya kusema na kutenda
Tanzania ilikuwa inabezwa na majirani zetu kama Kenya Malawi kuwa ni nchi ya
maneno maneno tu , lakini kwa sasa Mheshimiwa Rais amerudisha dhana ya kusema
na kutenda hapo hapo. Mfano lengo la kuhamia Dodoma ni la miaka mingi tangu
1973, lakini ametamka na kuanza kutenda na kutoa muda maalum wa kutekeleza
jambo hilo. Kama halijatekelezwa hatua zinachukuliwa na linaonekana na hata hao
majirani zetu wanaona na wamekubali kuwa sasa Tanzania ni Hapa Kazi tu .Lakini
nisieleweke vibaya kuwa labda awamu zilizopita hazikufanya kitu la hasha, kila
awamu ilifanya kazi yake na Mheshimiwa Magufuli anaendeleza kazi nzuri
iliyofanywa na watangulizi wake.
(d)Utendaji wa kazi kwa
watumishi wa serikali kama umeharibu unapaswa kuondoka sio kuhamishiwa mahala
pengine. Wasimuelewe vibaya Rais, bali ukiondolewa ridhika na toa fursa kwa
watu wengine, wapishe wengine watekeleze na wewe utapata nafasi ya kujifunza.
Watumishi
wa serikali kuendelea kung’ang’ania kukaa kwenye nafasi za madaraka hata pale
umri unapofikia. Tuna vijana wengi wapo mitaani hawana kazi wanahitaji ajira
hawa wazee wakiondoka kwa wakati na vijana watajaza nafasi zao, maendeleo
yataonekana na malalamiko yatapungua. Hii ni fursa pekee kwa vijana tofauti na
Ulaya vijana wakuchukua hizo nafasi hawapo ni wa kutafuta.
SWALI: Nini maoni yako
kuhusu mwelekeo wa nchi kwa sasa?
JIBU: Muelekeo wa nchi kwa sasa
ni mzuri, uongozi wowote ule wa nchi mara baada ya uchaguzi walioingia
madarakani hujipanga na kujaribu mambo mapya, ndio maana wanapewa awamu mbili
ili wajipange kisha waweze kutekeleza kile walichoahidi wananchi. Mheshimiwa Rais hataki kufanya kazi kwa mazoea
kuna mambo mengi mapya anajipanga tumpe nafasi
Kwa
sasa anaangalia pale alipo kama kuna makosa anarekebisha kabla ya kuanza kazi.
nadhani tumpe nafasi anayostahili ili afanye kazi na baadhi ya mambo mengi
ameshaanza kutekeleza kwa kukusanya fedha za mlipa kodi, ambapo zamani tulikuwa
tunachangia. Mfano hapa Bukoba naona kwenye hospitali zetu angalau sasa dawa
zinapatikana, wananchi watambue utekelezaji huu utaanza kuboreka polepole sio
kwa mara moja kwa hiyo wanapopata changamoto ndani ya utekelezaji wa ahadi za
Rais waziseme kwa nguvu zote ili zitatuliwe tuweze kusonga mbele . Pole pole
utekelezaji huo utaboreka.
Reli
ya kati aliahidi kuijenga kwa viwango vya kimataifa (Standard Gauge) tunaona ameshaanza kutekeleza wanajenga kwa vipande
vipande lakini mwisho wa siku tutafika angalau sasa kila kisemwacho kinaonekana
Mheshimiwa
Rais ameahidi kununua Ndege kweli ametimiza, ameahidi, kuleta
Meli, utaratibu umeshaanza nina
hakika tutapiga hatua kubwa sana baada ya muda mfupi ujao.
SWALI: Kuna maeneo ambayo
yanawagusa moja kwa moja wananchi katika maisha yao ya kila siku na Mhe. Rais
aliahidi kuyafanyia kazi kwa nguvu zote je hili limeanza kutekelezwa? Ni upi mtazamo
wako kuhusu utekelezaji huo?
JIBU: Mheshimiwa Rais ameanza
kutekeleza, watu wanalalamika hatuna hiki hatuna hiki lakini ameanza na
anatekeleza, mfano shule za msingi na sekondari elimu bure ameanza polepole, amepeleka
fedha kila mahali penye shule ya msingi na sekondari. Kwa upande wa afya
zahanati zetu, hospitali zinaboreshwa pole pole Reli ya kati ni uti wa mgongo,
nina uhakika polepole atafanya bila ya kuanza A huwezi kufika Z,
kilichohitajika ni kukata mzizi wa kutokufanya.
Inaonekana
kama hakipo lakini kipo kinaendelea na mwisho kitaonekana. Nafurahi kwa kuwa
dhana ya kunena na kutenda ipo tutafika tunapotarajia na huu ndio mtazamo wangu
kwa serikali ya awamu ya tano.
SWALI: Ili kuijenga
Tanzania iliyo bora ni vema kukubali changamoto zote zinazojitokeza na kuzifanyia kazi. Una lipi la kusema kuhusu madai
ya Vyama vya Siasa nchini kunyimwa uhuru wa demokrasia?
JIBU: Madai ni kitu ambacho
unatakiwa kukiangalia kwa uangalifu.Serikali ina mamlaka ya kuamua, kutenda na
kutawala, haki ya vyama vya siasa kufanya kazi ya kuikosoa serikali katika hali
chanya, sio hasi ni lazima kama watanzaniia tupendane na kuwa kitu kimoja na kufanya
kazi kwa pamoja, kwa kuwa tunajemga nchi yetu sote. Tukumbuke mihimili mitatu Serikali,
Mahakama na Bunge, hivi vyote vinapashwa kushirikiana na kuwa na uhusiano
mzuri.
Uhusino
kati ya serikali na vyama vya siasa vyama vya siasa kuikosoa serikali kwa
mtazamo chanya serikali pia ijue vyama vya siasa ni lazima vipewe nafasi ya
kuongea na serikali itimize wajibu wake
Serikali,
vyama vya siasa lazima waelewe kuwa tunajenga nchi moja ya Tanzania, nchi hii
ikibomoka tutabomoka wote hakuna atakaye nufaika na ukosoaji hasi ambao hauna
manufaa kwa nchi ya yetu. Hivyo wanasiasa
waongee, kuongea, kwa maana ya vyama vya siasa kukutana na serikali na serikali
uitimizwe wajibu wake Serikali mamlaka
ya kuamua na kutawala.
Mahakama,
lazima Itoe haki bila kuingiliwa, Wabunge ni wawakilishi wa wanannchi na sehemu
mahususi ya kuongea ni Bungeni. Wanasiasa wanaotoka kwa watu wanaowakilisha
watu lazima wawasilishe matakwa wa wananchi, lakini wakumbuke umuhimu wa
kukutana na kuongea badala ya kuleta vurugu ambazo wananchi hawakuwatuma hiyo
haikubaliki.
SWALI: Watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa
wakiishi kwa kuvumiliana na kuchukuliana bila kujali imani zao itikadi za
kisiasa na makabila yao. Hivi karibuni uvumilivu huo umepungua na kukaribia
kutoweka kabisa. Wewe kama kiongozi wa kiroho unaona nini kifanyike ili kulinusuru
Taifa na migogoro ambayo imeanza kujitokeza?
JIBU: Tunu ya Tanzania ni uzalendo,
umoja na amani, tumshukuru Baba wa Taifa kutuwekea misingi hii kwa kweli alifanya
kazi kubwa katika kuimarisha umoja wa Tanzania. Misingi hii imewekwa bila
kujali dini zetu itikadi zetu na makabila yetu.
Mfano
viongozi wa dini tulijitahidi sana kupitia Baraza la Maaskofu wakati huo nikiwa
Katibu wa Baraza hilo tuliunda baraza La maridhiano katika dini zetu zote
tulizonazo, tukashirikiana kutatua matatizo madogo madogo yaliyokuwa
yanajitokeza kwa kweli tulifaniikiwa. Hata sasa lipo Baraza la maridhiano kwa
dini zote linafanya kazi nzuri sana sana, hili linatusaidia kutatua migogoo
yote inayojitokeza katika jamii, serikali na vyama vya siasa.
SWALI: Unatoa ushauri gani
juu ya changamoto unaziona kwa sasa ili Taifa liweze kusonga mbele na kutimiza
azma ya Mhe Rais ya kuwatumikia wananchi kwa kuboresha maisha yao.
JIBU: Ili tuende pamoja
tunahitaji kuwa kitu kiimoja ninaomba chama tawala, vyama vingine vya siasa na
Bunge kuwa na lengo moja.
(a)
Serikali
ifanye kazi yake ya kutawala na sisi ni lazima kutoa ushirikiano kwa watawala wetu, tusiwaache wenyewe tuwape
ushirikiano. Kila mmoja apewe nafasi
yake, tufanye kazi vyombo vya dola tuvisaidie
ili tuweze kuishi kwa usalama mfano mimi nipo hapa kwa sababu kuna vyombo vya
usalama vinavyonilinda. Ukiona vyombo vya usalama vinashambuliwa ujue tupo
katika hali mbaya sana tusiruhusu hali hii ianze kuota mizizi. Usalama ukikosekana wote tutaangamia usalama
wetu hauna mjadala.
(b)
Kwa
wale ambao sio wana siasa tusaidie kutoa maoni yetu kwa serikali ukifanya
vizuri katika nafasi yako lazima utachaguliwa tu na ukifanya vibaya watakutoa.
Nashukuru sana kwa wabunge wa upinzani kwa kukubali kurudi bungeni.
(c)
Kuhusu maaandamano, nadhani tufanye maandamano
lakini yawe maandamano chanya yanayoleta maendeleo, Mfano kupinga ukatili kwa Albino
na sio maandamano ya kupinga serikali hata kwa jambo lililo jema. Kazi ya vyama
vya siasa ni kukosoa, kuisimamia serikali itekeleze majukumu yake na kutunga
sheria sio kuhamasisha maandamano yasiyo na tija.
(d) Nashukuru sana kusikia
wapinzani wanarudi Bungeni kuendelea na shughuli zao, wananchi wanatoa maoni yao ili yaweze kufanyiwa kazi na serikali, tunapashwa
tuongee kwa uwazi na uhuru. Tuna vyombo vingi sana vya kutoa maoni yetu na
yatawafikia wahusika ambao lazima wayafanyie kazi hakuna haja ya kufanya
maandamano yasiyo na tija.
SWALI: Ushauri wako kwa
Serikali, Vyama ya siasa na watanzania kwa ujumla?
JIBU: Serikali isikilize watu,kuchukua
maoni yao na kuyafanyia kazi. Serikali ifanye kazi kwa bidii kuwaletea
maendeleo wananchi, changamoto zipo ila wazifanyie kazi na kusonga mbele.
Vyama
vya siasa vinatakiwa kushauri na kukosoa ikiwa ni pamoja na kuisimamia serikali
katika utekelezaji kwa kile walichoahidi na kupitishwa ndani ya Bunge tukufu.
Wananchi
wenzangu wa Tanzania tumuunge mkono mheshimiwa Rais tufanye
kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo nasema “Hapa kazi tu” Hapa kazi tu
No comments:
Post a Comment