Badhi ya watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.
KATIKA kutekeleza kauli mbiu ya Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli ya “Hapa Kazi tu” serikali mkoani Kilimanjaro imetangaza kusitisha likizo na ruhusa zote kwa watumishi wake katika kipindi cha siku kuu za Krismasi na mwaka mpya.
Agizo hilo linakuja wakati tayari baadhi ya watumishi wa serikali kuanza taratibu za kuomba likizo na ruhusa kwa ajili ya kwenda kushiriki siku kuu za mwisho wa mwaka za Krismasi na mwaka mpya.
.Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala alitangaza uamuzi huo jana wakati wa kikao cha kazi alichoitisha na wakuu wa wilaya zote za mkoa, wakurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na watendaji wengine wa serikali.
“Mh Rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika,Makamau wa rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika ,Waziri mkuu pia vivyo hivyo sasa sisi ni nani twende kwenye mapumziko ya siku kuu ya Krismasi.”alihoji Makala.
“Kwa maana hiyo ili haya tunayotaka ya elimu bure ,kukabiliana na Kipindupindu ,kwa madaraka niliyopewa kama mkuu wa mkoa nasitisha likizo zote,kwa Wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi na wakuu wote wa idara ili mambo haya yaweze kutekelezwa,tumesema Hapa ni kazi tu”aliongeza Makala.
Alisema utekelezaji wa agizo la rais la kufanya usafi siku ya sikuu ya Uhuru inayofanyika Desemba 9 kila mwaka ,mapambano ya ugonjwa hatari wa Kipindupindu ambao umeendelea kusambaa sehemu kubwa ya nchi hayawezi kusubiri hadi watusmishi wa serikali watoke likizo.
|
No comments:
Post a Comment