Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi |
Na Emanuel Madafa, Mbeya
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Lukas Wambura (38) Mkazi wa Banana – Dar es salaam mwenye shahada ya dharura ya kusafiria
ab-10044029 akiwa na
vipande vinne vya meno yadhaniwayo kuwa ya tembo vyenye uzito wa kilo 8.4 yenye
thamani ya dola za kimarekani 30,000, sawa na tshs 64,140,000/=.
Tukio hilo limetokea Novemba 30 -2015 majira ya saa12 jioni katika eneo la custom – mpakani tunduma, ,
wilaya ya momba Mbeya ..
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya
Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa
anavuka mpaka akitokea nchi jirani ya Zambia kuingia nchini na mzigo huo
alikuwa ameuficha ndani ya begi lake la nguo.
Wakati huo jeshi hilo la polisi linawashikilia watu wanne kwa
kukutwa na silaha mbili pamoja na nyara za serikali.
Kamanda Msangi amewataja watuhumiwa
hao kuwani M ohamed Ndilava [55], Mkazi
wa Mkwajuni , Nassora Omary [65] Mkazi
wa Tabora na Mwanza Mtokambali [39] Mkazi
wa Njelenje pamoja na Frank Jonas [32], Mkazi wa Bitimanyanga.
Msangi amesema watuhumiwa hao
sita walikamatwa Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha
Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watuhumiwa walikutwa na silaha moja aina ya
riffle 416 yenye nambari c.6539833 na gobole moja lisilokuwa na namba, pia
walikutwa na nyara za serikali kichwa
kimoja cha paa, nyama ya paa na nyama ya sungura vyote vikiwa na thamani ya
tshs 1,176,000/=.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Msangi anatoa
wito kwa yeyote mwenye taarifa
juu ya wahalifu wakiwemo majangili
kuzitoa katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe mara
moja.
(JAMIIMOJABLOGMBEYA )
No comments:
Post a Comment