Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka
na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod, wakati wa
zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44
ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo
zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili eneo la Kituo cha
Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi wa eneo hilo
kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya Uhuru
wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi
hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia kukagua eneo la
kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, wakati
alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi kufanya usafi
wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya Uhuru wa Tanzania
kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na
baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa
mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya Uhuru wa Tanzania kama
alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika
nchini kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali waliojitokeza
kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha zoezi la usafi eneo la
Morocco, jijini Dar es Salaam, leo Dec 9, 2015. Picha na OMR.
14 n15:- Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka eneo la Morocco,
baada ya kushiriki zoezi hilo na wananchi wa eneo hilo la kufanya usafi wa
mazingira leo Dec 9, 2015. Picha na OMR
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo
ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na
Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 za uhuru wa
Tanzania Bara.
Akizungumza
na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais
amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni
wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.
“Haya
makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha
hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema MHe. Samia.
Alielezea
kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo
alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za
mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.
Makamu
wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni
michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na
kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa
na elimu bora.
Pamoja
na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa
Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya
DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar
es salaam
No comments:
Post a Comment