Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 8 November 2015

ZIARA YA KUSHTUKIZA YA RAIS MAGUFULI WIZARA YA FEDHA

Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile leo alipotembelea ofisi za Wizara ya Fedha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile wakati wa ziara hiyo leo jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na uongozi wa Wizara ya Fedha leo jijini Dar es salaam.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Inline image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2015.

Katika ziara hiyo Mhe. Rais alipatafursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo zinaikabili Wizara ya Fedha.

Wakati akimkaribisha Mhe. Rais Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.  Miongoni mwa sababu ni misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwepa kodi, makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo. Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo matumizi ya Tehama na EFDs. 

“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini na wanafanyakazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu ya kuja hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe. Rais.

Nimesikia changomoto nyingi na ninaagiza kuwa muhakikishe walipakodi wakubwa wanalipakodi na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iwezeze kukusanya kodi kikamilifu na si kuwabana wafanyabiashara wadogo wa dogo.

Mhe. Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanyakazi kwa bidii ili kuvuka lengo.
Imetolewa na;
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Ingiahedi C. Mduma
6.11.2015

No comments:

Post a Comment