Kaimu Mkurugenzi jiji la Mbeya Dkt,Samuel Razalo |
Na EmanuelMadafa, Mbeya
HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya, imesema imejipanga vyema katika kuhakikisha
mradi mkubwa wa soko jipya la mwanjelwa unasimamiwa kikamilifu kwa
kufuata taratibu za serikali sanjali na
mikataba iliyoingia na benki ya
CRDB kwa kipindi cha miaka 15.
Mradi huo wa soko la kimataifa la Mwanjelwa lililopo
jijini Mbeya ujenzi wake imefikia asilimia 99 hivyo upo katika hatua za mwisho
za kukamilika kwake.
Akizungumza ofisini kwake , Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Razalo, amesema licha ya soko hilo
kukamilika lakini mchakato wake wa uendeshaji utazingatia taratibu za
halmashauri na mkataba walioingia na benki ya CRDB.
Amesema hatua hiyo,
inatokana na halmashauri ya Jiji hilo kukopa kiasi cha shilingi Bilioni 13
kutoka benki ya CRDB na kufanikisha ujenzi wa soko hilo ambao umedumu kwa
zaidi ya miaka 10 tangu lilipoteketea kwa moto.
Amesema,
benki hiyo kwa kukubaliana na halmashauri imepanga kiasi cha kodi
kitakachopaswa kulipwa na wafanyabiashara kuanzia shilingi elfu moja kwa
siku hadi shilingi 500,000 kwa mwezi.
Amesema Wafanyabiashara
ambao watatumia meza watatakiwa kulipa ushuru wa shilingi 1000 kwa siku huku
wale wa maduka watalipa kiasi cha shilingi 500,000 kwa mwezi na wauza nyama
watapaswa kulipa kiasi cha shilingi 400,000 kwa mwezi,”alisema.
Amesema ,
awali halmashauri hiyo ilipokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara ambao
walikuwa wakiomba kupunguzwa kwa gharama za tozo hizo kwani ziko juu
ukilinganisha na hali ya uhumi wa sasa.
Amesema,
halmashauri iliyachukua maombi hayo na kuyawasilisha kwenye mamlaka husika ya
benki ya CRDB hivyo wanasubili majibu na kuwataka wafanyabiasha kuwa wapole
wakati wanasubili majibu hayo kutoka kwenye uongozi wa benki hiyo.
Soko la
Mwanjelwa liliteketea kwa moto mwaka 2006 na kusababisha hasara ya mamilioni ya
fedha kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 2000 walionguliwa maduka yao na
ujenzi wake kuanza mwaka 2008..
Mwisho.
Muonekano wa Mradi wa Soko la Mwanjelwa Jijini Mbeya ambapo ujenzi wake bado unaendelea.(JAMIIMOJABLOG MBEYA) |
No comments:
Post a Comment