Highness Kiwia akionyesha moja ya karatasi yenye makosa.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua
kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa
huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.
Kiwia ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa
na Angelina Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.
Alieleza kuwa katika vituo mbalimbali jimboni
humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya
wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia
kura pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale
waliyojiandikishia.
Katika hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa
kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na
kwamba siku ya kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo
kuzilai.
Kwa upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi
wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu
linapaswa kulaaniwa kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka
taratibu mbalimbali za uchaguzi.
Katika Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni
Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura
85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679
ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa
na upinzani.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari
Kiwia akiteta jambo katika Mkutano na Wanahabari
Kutoka Kushoto ni Humphrey Mhada ambae ni Mwenyekiti Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, Highness Kiwia ambae alikuwa mgombea Jimbo la Ilemela Chadema na Hassan Haji ambae alikuwa Meneja Kampeni Jimboni Ilemela
Press Conference
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari
Wa kwanza kulia waliokaa ni Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema akiongea katika mkutano na wanahabari
Peter Kaiza ambae alikuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ibungilo Ilemela akionyesha moja ya karatasi yenye makosa
Kutoka Kushoto ni Julius Malifedha ambae ni Katibu Mwenezi Chadema Ilemela, Peter Kaiza aliekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ibungilo na Ivonne Highness ambae alikuwa Mratibu wa Kampeni za Uchaguzi
Kada wa Chama
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUJUZE JAMII
No comments:
Post a Comment