Meneja Mradi Ruvu chini Mhandisi Emmanuel Makasa akiwaonesha waandishi wa habari sehemu ya bomba la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Ruvu chini kwenda jijini Dar es salaam.
Sehemu ya bomba la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Ruvu chini kwenda jijini Dar es salaam lilivyozamishwa chini tayari kwa kusafirisha maji ambayo yatawanufaisha wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kwa matumizi mbalimbali.
Baadhi ya mitambo ya kusafisha maji ambayo yamesafishwa tayari kwa matumizi ya wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani.
Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi kutoka Wizara ya Maji wakiwa eneo la chanzo cha maji cha Ruvu Chini.
Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi kutoka Wizara ya Maji wakiwa eneo la chanzo cha maji cha Ruvu Chini wakipita juu ya eneo la kusafisha maji kabla ya kusafirishwa kwa matumizi mbalimbali.
Meneja Mradi Ruvu chini Mhandisi Emmanuel Makasa (aliyevaa tai) akiongea na waandishi wa habari walipotembelea ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam.
Fundi akiendelea na kazi ya kuunganisha na kuchomelea bomba la maji ambalo litasafirisha maji kutoka Ruvu Chini kwenda jijini Dar es salaam.
Muonekano wa maji yakiwa mtoni kabla ya kuanza kusafishwa kupitia hatua mbalimbali kwa matumizi.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Mamlaka ya Maji Safi na
Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu
ya maji ili kuwanufaisha wakazi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kupata maji
kwa mahitaji yao ya kila siku.
Mioundombinu hiyo inayoboreshwa ni pamoja na bomba la Ruvu
Chini lenye urefu wa Jumla ya km 55 ambapo hadi sasa km 52.6 zimekamilika na
zimebaki km 2.4 ili kukamilisha mradi huo
ambao utasaidia kusimamia moja ya sentensi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
ya “Kuwatua akina mama ndoo za maji kichwani”
Ili kufikia azma hiyo
ya kuwapatia maji safi na salama wakazi wa mikoa hiyo, Mkurugenzi wa Usimamizi
na Ufundi wa DAWASA, Romanus Mwang'ingo alisema kuwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu
Chini na ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo Kikuu cha
Ardhi ndiyo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika jiji la Dar es salaam na
maeneo ya mkoa wa Pwani.
Akiongea na waandishi
wa habari ofisini kwake kabla ya waandishi hao kwenda kujionea hatua
iliyofikiwa, Mwang'ingo alisema kuwa ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika
ifikapo Februari 2016 na kuondoa adha ya
maji kwa wananchi na kuwaunganishia wengine ambao hawakuwa na huduma ya maji.
“Tumelazimika kufikia
hatua ya kupanua huduma ya upatikanaji wa maji katika mikoa ya Dar es salaa na
Pwani kutokana na ongezeko la watu kulingana na sensa ya watu ya mwaka 2012,
mkoa wa Dar es salaam una jumla ya zaidi ya watu milioni 5 ambao watatumia maji
zaidi ya lita milioni 5 kwa siku”,
“Katika upanuzi huo, kumekuwa
na changamoto ya makazi ya watu kuwa ndani ya mradi ambapo kulikuwa na kesi 17 katika
mahakama mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo mahakama ya ardhi, hadi sasa
DAWASA imeshinda kesi 13 na kupewa haki ya kutumia njia hiyo kukamilisha
upanuzi wa mradi” alisema Mwang'ingo.
Kwa mujibu wa Mwang'ing'o
kesi nne bado zipo mahamani na ambazo zimefikia hatua mbalimbali kulingana na
taratibu za kimahakama.
Lengo la mradi huu ni
kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 182 hadi 270 kwa siku. Mradi
ambapo awamu itakayofuata ni lita milioni 360 kwa siku.
Chanzo cha maji cha
Ruvu Chini ndiyo chenye kiwango kikubwa ambacho kina wapatia maji wakazi wa Dar
es salaam kwa zaidi ya asilimia 75 ikilinganishwa na asilimia 25 kutoka Ruvu
Juu.
Mradi wa upanuzi wa
mtambo wa Ruvu Chini unalenga kuongeza uzalishaji maji na kuwahudumia wakazi wa
maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa
wa Pwani
Maeneo mengine
yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo,
Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani,
Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala.
No comments:
Post a Comment