Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 29 November 2015

KAMANDA MPINGA AZINDUA OPERESHENI PAZA SAUTI JIJINI DAR

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP  Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam.

Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari  zake mkoani wakati wa  kuzindua  wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona  viashiria vya uvunjifu wa sheria za  barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam.
Wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikilizaKamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua  Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa  wanapoona kuna viashiria vya  uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment