Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango Mkoani Kilimanjaro. Ibada hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya shs Milioni 100 zilipatikana. (Picha na Francis Dande)
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiijili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Cuthbert Temba akiongoza ibada.
Waumini wa Kanisa hilo wakiwa katika ibada.
Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Goodfrey Nkini na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakiwa kanisani na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Huduma Shirikishi, Esther Kitoka.
Mkurugenzi Benki ya CRDB tawi la Moshi, Francis Mollel
(kulia) akipokea mbuzi kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Siha Sango, Cuthbert Temba (wa pili
kushoto) katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika
wa Siha Sango. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi mbuzi Mchungaji Emmanuel Kileo
baada ya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa
Kanisa hilo. Kushoto ni Solomon Nkini.
Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Goodfrey Nkini akipokea mbuzi baada ya kumnunua katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha.
No comments:
Post a Comment