Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 31 December 2015

NAIBU WAZIRI WA HABARI ATEMBELEA MAELEZO

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura katikati akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Assah Mwambene wa kwanza kulia ya jinsi ya kutunza picha za matukio mbalimbali wakati alipofanya ziara Idarani hapo leo, kushoto ni Afisa Habari Mkuu Anna Itenda.(picha na Benjamini Sawe-WHSUM).

MAWAKALA WA TIGO PESA ZENJ WAPEWA ELIMU

Mkurugenzi  wa Tigo Pesa Tito Magesho akizungumza na mawakala wa Tigo Pesa walioko Zanzibar wakati wa mkutano wa kuwakutanisha mawakala wa Zanzibar jinsi ya  kuendesha huduma hiyo kwa wateja wao mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa skuli ya sekondari ya ben bella Zanzibar

WANANCHI WA KIJIJI CHA SHENDA WILAYANI GEITA WALALAMIKIA UCHAFU ULIOTUPWA TAREHE 9 DISEMBA




Huo ndio uchafu uliotupwa katika kijiji cha shenda siku ya tarehe 9 Disemba ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima 

WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE WAPATA UJASIRI WA KUTUMBUA MAJIPU BAADA YA MAFUNZO YA URAGHABISHI




Ndugu Halidi Abdu toka kijiji cha Shenda chenye wakazi wapatao 2,800 katika kata ya Masumbwi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita;akihojiwa na mtangazaji wa redio free africa william bundala almaarufu Kijukuu cha Bibi k akielezea jinsi walivyoweza kuwaadaa viongozi wao waweze kuwasomea taarifa yao ya mapato na matumizi.
Na Krantz Mwantepele, Geita 

Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. 

MAAMUZI MABOVU NA UTENDAJI MBAYA WA KAZI WAWAPELEKEA WENYEKITI KUMCHUKULIA HATUA MWENYEKITI WAO WA KIJIJI


Wanafunzi katika shule ya msingi Shenda wakiwa wamekaa kwenye moja ya darasa lililosakafiwa

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na kilio toka kwa wananchi kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na viongozi waliowachagua pasipo kuchukua hatua zozote. Ukimya huu wa wananchi ndio unaosababisha kilio hicho kuendelea kukuwa kila siku.   Ila vilio hivi huishaga pale tu wananchi wanapoamua kwa dhati kuchukua hatua, kama walivyofanya wananchi wa kijiji cha Shenda.  Shenda ni moja kati ya vijiji zaidi ya 200 vinavyofanya kazi na programu ya Chukua Hatua mkoani Geita.

MIGOGORO 41 YATUA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MAFUNZO YA AWALI KWA WATUMISHI WA IDARA YA WAKIMBIZI, LEO JIJINI DAR ES SALAAM


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza  na washiriki  wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi(hawapo pichani),wakati alipofungua mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wapya, katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.Kulia ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo.

SALAMU ZA MWAKA ZA RAIS WA TFF KWA WADAU KWA WADAU WA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Rais wa TFF, Jamal Malinzi

Ndugu zangu, Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kupitia kwenu wanahabari ninaomba nitoe salam za mwaka za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Awali ya yote tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametulinda kwa mwaka mzima na kupitia Baraka zake tumeweza kuwa na nguvu, uwezo na hekima za kutimiza majukumu yetu mbalimbali katika kipindi hiki cha mwaka 2015. Tuzidi kumuomba atuvushe salama mwaka 2015.

UTAJIRI WA RIDHIWANI, HATA BILL GATES HAFUI DAFU!

           Ridhiwani Kikwete

NA LUQMAN MALOTO

UKIPANDA daladala huwa hakuna mfumo unaoeleweka, siku nyingine utakutana na kelele kama sokoni, wale wanaongea yao, hawa wanabishana hivi, hapa napo kuna ubishi wa soka.

TAARIFA YA KUFUKUZWA KWA OFISA BIASHARA DODOMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA
Simu Na: (026) 2322848, 2321607, 
                            2322853, 2322420,
Nukushi: (026) 2322116,  2322146.
                             2321013,      
Barua pepe:ps@poralg.go.tz


Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa,
S. L. P. 1923,                          DODOMA.
  
TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na  Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

WATAKAOFANYA FUJO MKESHA WA MWAKA MPYA KUKIONA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova

Na Jacquiline Mrisho, MAELEZO

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi kutokufanya fujo wakati wa  mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati mikali kwa watakaokaidi amri hiyo.

WAZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA MKOANI KIGOMA, ATEMBELEA KAMBI ZA WAKIMBIZI, AWAONYA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimzungumza na watumishi wa Serikali na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika Ukumbi wa NSSF mjini humo. Majaliwa aliwataka watumishi wa mkoa huo wafanye kazi kwa juhudi ili kuuletea maendeleo zaidi mkoa huo. Waziri Mkuu Majaliwa,  pia aliwaonya wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu na Nduta kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika kambi hizo . Kulia meza kuu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI WA AFYA, MHE. UMMY MWALIMU ATEMBELEA MSD, AAHIDI KUWA BALOZI WAO NA KUWATATULIA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI IKIWEPO DENI WANALOIDAI SERIKALI

ummy-msd 175
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia.

JK, WAZIRI LWENGE WAKAGUA MITAMBO YA MAJI WAMI, CHALINZE



Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA KAZI, VIJANA NA AJIRA, MHE. ANTHONY MAVUNDE AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA TIGO

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijtonyama  jijini Dar es Salaam.

LIGI KUU YA ZANZIBAR KVZ NA JKU MCHEZO ULIOFANYIKA UWANJA WA AMAAN TIMU YA JKU IMESHINDA 2--0

Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya KVZ kabla ya kuaza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda 2--0.

WANAWAKE NDIYO NGUZO MUHIMU YA UCHUMI TANZANIA

Anna Alphonce (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busolo akifafanua jambo wakati akielezea uraghbishi anaofanya.


Na Krantz Mwantepele, Kahama

Wanawake ni nguzo muhimu sana katika uchumi wa watanzania wengi. Mwanamke ana ushawishi mkubwa na hasa pale anapoamua kuwa chachu ya maendeleo. Na hasa anapowezeshwa kufanya hivyo.

MSANII TEKNO MILES KUNOGESHA TAMASHA LA JOHNNIE WALKER “GROWN & SEXY THE GOLD FINALE”

Mkurugenzi wa Straight up Vibes Omary Abood (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya.

MWALIMU GODFREY GODWIN KIHENGU NA MISS MARIAM BARAKA BINAGI WAUAGA RASMI UKAPERA

Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akiwafungisha ndoa Bi.Mariam Baraka Binagi (wa pili kulia) wa Rebu Tarime, Mara pamoja na Mwalimu Godfrey Godwin Kihengu (wa pili kushoto) wa Nyansurura Tarime, Mara ikiwa ni katika ibada iliyofanyika jana Desemba 30,2015 katika Kanisa Anglikana Buhemba Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Picha na BMG (Binagi Media Group)

Tuesday, 29 December 2015

SERIKALI HAIJUI AU INAZUGA UFISADI NGUZO ZA UMEME?


Na Daniel Mbega
HATUA ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Uledi Mussa, kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuacha kasumba ya kutumia mabilioni ya fedha kununua nguzo za umeme nje ya nchi ni sawa na serikali kujipiga kofi na kulia yenyewe.

HAWAMTAKI MUHONGO, WALITAKA WATEULE WAO?

Profesa Sospeter Muhongo siku alipojiuzulu Januari 24, 2015

Na Daniel Mbega
UTEUZI wa Baraza la Mwaziri umepokelewa kwa hisia tofauti ambapo wapo wanaosema Rais Dk. John Magufuli amekosea kuwateua Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harrison Mwakyembe.
Wanaokosoa uteuzi wa mawaziri hao wawili kuwemo kwenye baraza wanawahusisha na ufisadi, hali wanayosema inaweza isilete mabadiliko ambayo yalianza kuonekana katika serikali ya awamu ya tano.

ZAMU YA KURUDISHA MABILIONI YA VIGOGO YALIYOFICHWA USWISI

Zitto Kabwe, ambaye aliibua kashfa ya vigogo walioficha mabilioni nchini Uswisi.


Na Daniel Mbega
IJUMAA Mei 16, 1997 mara tu baada ya Laurent Kabila kuipindua serikali ya mwanahabari Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga nchini Zaire, alitangaza kutaifisha mali zote za dikteta huyo aliyeitawala kwa mkono wa chuma nchi hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa miaka 32.
Siku moja baadaye, yaani Jumamosi Mei 17, 1997 serikali ya Uswisi nayo ikatangaza kuzuia mali za Mobutu kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa utawala mpya wa Kabila. Hadi kufikia mwaka 2009 mali hizo, karibu Dola 6.7 milioni, zilikuwa hazijarudishwa.

KWA HERI IPTL, VIPI WALE WALIOTUINGIZA MKENGE?

 Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi (Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL. Wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya IPTL.

Na Daniel Mbega
ACHANA na Shs. 240 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow, tunazungumzia mabilioni ambayo Serikali imeilipa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwa miaka 20.
Mkataba wake umekwisha mwaka huu 2015 kwa staili ya aina yake, ukitanguliwa na wakubwa kugawana mabilioni yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow, huku wengine wakiziita fedha hizo kwamba ni ‘za mboga’.

TANZANIA YAPOTEZA, BOTSWANA NA NAMIBIA ZAVUNA MADAKTARI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka akiuliza swali wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012. (Picha na Maktaba
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka baada ya kuzungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012. (Picha na Maktaba) 

Na Daniel Mbega
SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imewaahidi Watanzania kuboresha sekta ya afya. Hili ni jambo jema.
Imeahidi kujenga hospitali za wilaya, mikoa na hospitali za rufaa pamoja na kutekeleza Sera ya Afya inayosisitiza kwamba kila kijiji kiwe na zahanati na kkila kata iwe na kituo cha afya ili kusogeza karibu huduma za afya kwa jamii.
Licha ya kuahidi pia upatikanaji wa dawa, lakini bado haijazungumzia mikakati yake ya kuhakikisha wanakuwepo watumishi wa kutosha wa afya, hususan madaktari.

SERIKALI MAKINI HUKUSANYA KODI!

Bandari ya Dar es Salaam ambayo kutokana na ufisadi na rushwa, watendaji wa serikali wanaikosesha mabilioni ya fedha za kodi na ushuru mbalimbali. (Picha ya mtandao).

Na Daniel Mbega
NAKUMBUKA hotuba ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa Mei Mosi 1995 pale kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Alisema mambo mengi sana, yote yenye maana, lakini kubwa ninalolikumbuka leo, alisisitiza umuhimu wa kukusanya kodi.

RAIA WAAMILIFU WALILIA HUDUMA BORA KWA WAKULIMA

Mraghibishi Alex John maarufu kwa jina Mafuriko akiongea na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Herieth Makwetta alipotembelea kijijini hapo 

Na Krantz Mwantepele, Geita

“Huku tupo tu tunahangaika na kilimo, tunalima kila mwaka, lakini ukweli ni kwamba kilimo chetu wala hakina faida basi tu bora siku ziende”.

WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA ENGUSEROSAMBU WAFURAHIA MSITU KUREJESHWA MIKONONI MWAO



Mraghbishi Noorkiyengop Mbaima toka kijiji cha Enguserosambu akisimama mbele ya mifugo iliyokutwa msituni  katika eneo lililoruhusiwa la msitu wa  jamii wa Enguserosambu

Ilikuwa ni siku ya shangwe na furaha kwa wananchi wa kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro. Hii ni baada ya serikali kukubali ombi lao la kusimamia rasilimali  ya msitu wa Loliondo namba 2 unaopakana na vijiji vinne vinavyokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi wapatao 20,000 wanaotegemea mahitaji yao toka katika huo msitu.

WARAGHABISHI WAKOLEZA KASI YA MABADILIKO WILAYANI KISHAPU

Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wilayani Kishapu  wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi. 
Na Krantz Mwantepele ,Kishapu 

Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko, kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka.

WAANDISHI WA HABARI WASAIDIA WANAVIJIJI NCHINI KUSIKIKA KUPITIA SAUTI ZAO


Mraghabishi mwalimu Revocatus Renatus ( kulia )  wa kijiji cha Unyanyembe mkoani  Shinyanga akihojiwa na mtangazaji wa Redio Free Africa Felista Kujirilwa wakati wa  kuandaa  moja ya vipindi vya redio vya Chukua Hatua. 

“Haijatokea hata siku moja mwandishi wa habari akaja huku kwa kweli. Hii ni mara yangu ya

kwanza kuona wanahabari katika kijiji chetu. Toka nimezaliwa sijawahi kumuona mwandishi wa habari kuja hapa na mimi nina miaka 70.”  Hayo ni maneno ya Mzee Titus Ndugulile mraghabishi wa kijiji cha Mwamala-B kilichopo kata ya Mwamala wilaya ya Shinyanga vijijini.

GO FOR ZANZIBAR (GOZA) A GERMAN NGO SUPPORTS THE WELEZO OLD AGE HOME

Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleischer na Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha , wakimkabidhi  msaada Mwakilishi wa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar  Mzee Kombo Shein, vyakula kwa ajili ya wazee hao ili kuweza kujimuika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismax  na mwaka mpya  kulia Msimamizi wa Kijiji hicho Sister Mary Gemma na Hassan Khamis hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya wazee hao Welezo.

DKT. MPANGO AMEWAASA WATUMISHI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (wa pili kulia) mara baada ya kuwasili Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

KIDOA AIBUKA KIDEDEA IJUMAA SEXIEST GIRL 2015

IMG_1255 
Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

UBADHIRIFU WA FEDHA NA RASILIMALI WAPUNGUA VIJIJINI KWA VIONGOZI KUHOFIA KUCHUKULIWA HATUA NA WAKAZI WA MAENEO HAYO

 Waraghbishi toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.

Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. 

TIGO YAGAWA SIMU 200 KWENYE “MRADI WA KUWAUNGANISHA WANAWAKE” RUFIJI

Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine kulia kwake ni John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na kushoto kwake ni  Dkt. Flora Myamba Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA.

WATOTO WA WAHADHIRI WA UDSM WAJUMUIKA PAMOJA KWENYE 'GET TOGETHER' YA NGUVU

Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu. Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo.

WAWEKEZAJI KATIKA MIGODI TANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAKAZI WAISHIO MAENEO HAYO ILI KUPUNGUZA MIGOGORO



Baadhi ya Washiriki wa Mdahalao huo wakifuatilia mada iliyokuwa ikijadiliwa wakati wa mdahalo.

Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji, uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania.  

VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI WAFURAHIA MAFUNZO YA URAGHABISHI





Baadhi ya wenyeviti toka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya uraghabishi  yaliyofanyika wilayani hapo

Na Krantz Mwantepele


“Unakuja kwenye ofisi yangu na kutoa taarifa za ubadhirifu wa mtendaji wa kijiji. Nakuuliza, je umechukua hatua zipi kama kiongozi wa kijiji kabla kuja kwenye ofisi yangu? Unanijibu hapana, hii si sahihi,” 

BELLA KUFUNGA MWAKA NA KOFFI, DAR LIVE

BELAKING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.
Na Mwandishi Wetu 
 KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufunga mwaka (Desemba 31) na wimbo alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide uitwao Acha Kabisa, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

RIDHIWANI KIKWETE ATETA NA KATIBU MKUU KIONGOZI,OMBENI SEFUE IKULU


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya Rais Dk John Magufuli kuwaapisha mawaziri waliokuwa wamesalia Ikulu, Dar es Salaam jana.

TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK



Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa Facebook, www.facebook.com/TigoTanzania  kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa Tanzania.

Wednesday, 23 December 2015

JAMII YETU IKO MIKONONI MWETU


Mratibu wa Vijana, Bahati Juma (wa kwanza kulia) akiwa na wanafunzi wa darasa la saba, shule ya Msingi Uchunga, kupitia pamoja somo la kiswahili kituoni hapo.

WASHINDI KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI PANGANI WAPATA ZAWADI

ø;
Meza kuu,wa kwanza kulia ni Meneja wa redio PANGANI FM Maimuna Msangi, wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA ambalo limeratibu tamasha hilo VERA PIEROTH,wa tatu ni Kaimu mgeni Rasmi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya PANGANI Bi Patricia, na wanne ni Mratibu wa masuala ya UKIMWI wilaya ya PANGANI.

WAZIRI APIGA MARUFUKU WAHANDISI 'UCHWARA' KUPEWA TENDA ZA UJENZI WA BARABARA

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto), akitoa maagizo mbalimbali kwa uongozi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini, alipotembelea bodi hiyo, Dar es Salaam juzi, kujua utendaji wake. Kulia ni Meneja wa bodi hiyo, Joseph Haule. (HABARI,PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

KIWANDA CHA TBL ARUSHA CHATOA ZAWADI KWA WALIOFANYAKAZI KWA MIAKA 10 HADI 30

Wafanyakazi wa kiwanda cha Tanzania Breweries Limited(TBL)mkoa wa Arusha waliofanyakazi wa miaka 10 katika kampuni hiyo wakiwa wameshika vyeti vya kutambua mchango wao na hundi.Waliosimama nyuma ni maafisa waandamizi wa TBL

HOSPITALI ZAAGIZWA KUTENGENEZA MFUMO WA MALIPO WA KIELEKTRONIKI

IMG_9410
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahi jambo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mwishoni mwa juma mkoa wa Lindi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

WAZIRI UMMY MWALIMU AVAMIA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO MKOANI TANGA, KUKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA LEO

IMG-20151220-WA0011
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya (jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi) wa dirisha la dawa katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 20, 2015.

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO


Samaki na Mafuta ya samaki ambayo ni muhimu katika mwili

Pilipili kali 

Brokali

Nyanya 

#‎AfyaYako‬ Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
1.MAFUTA YA SAMAKI