Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 31 January 2014

TP MAZEMBE YAMTAKA MESSI

Kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’.
MAMBO yamekucha kwa kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya klabu tajiri ya TP Mazembe ya Lubumbashi, DR Congo kuonyesha wazi kuwa inamtaka.
TP Mazembe tayari imetuma mtu ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kumshuhudia Messi akiichezea Simba na ameeleza nia ya klabu hiyo.
Shushu huyo wa usajili wa TP Mazembe alikuwa uwanjani wakati Simba ikicheza na Rhino ya Tabora kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili na kushinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Messi.
Habari za uhakika zimeeleza mara baada ya mtu huyo kumshuhudia Messi akifunga bao na pia kukosa penalti amewaeleza viongozi wa Simba kutokana na nia ya klabu hiyo maarufu barani Afrika.

“Jambo hili bado ni siri kubwa, lakini TP Mazembe walimtuma mtu wao, huyo ndiye alitumwa mara ya kwanza kuifanyia umafia Simba kabla ya TP Mazembe kuja hapa kucheza.
“Alipokuja akamuona (Mbwana) Samatta na kuwaambia kuna mchezaji hatari, ndiyo maana uongozi wote wa juu wa TP Mazembe ukaja kuja kushuhudia mechi hiyo na kweli Samatta akafanya vizuri.
“Kutokana na hali hiyo huyo jamaa anaaminiwa sana, akirudi na kusema Messi yuko safi, basi jamaa watakuja kufanya rasmi mazungumzo na Simba,” kilieleza chanzo cha uhakika.

TP Mazembe sasa inamlipa Samatta kitita cha dola 10,000 (Sh milioni 16.5), kwa mwezi. Kama itafanikiwa kumpata Messi, basi huenda akachota kuanzia dola 3,000 hadi 5,000, kwa mwezi.
Messi amekuwa gumzo kuanzia mwanzo wa msimu huu kutokana na kiwango chake kupanda kwa kasi kubwa.

<GPL>

ARSENAL WAINGIA MKATABA MPYA MNONO NA PUMA

Hii ni jezi mpya ya Arsenal? Thierry Henry akiwa na Bacary Sagna, Linford Christie na Olivier Giroud

KLABU ya Arsenal imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu wa udhamini wa vifaa vya michezo na kampuni ya Puma kuanzia Julai mwaka 2014.

Pamoja na hayo hakuna kiwango cha fedha cha udhamini huo kilichothibitishwa Jumatatu, ingawa dili hilo linatajwa kama kubwa zaidi katika historia ya uhusiani wa Puma na Arsenal.
Inafahima Washika Bunduki hao wanapokea kiasi cha Pauni Milioni 30 kwa mwaka kutoka kwa wadhamini wakuu, shirika la ndege la Emirates, na imeripotiwa dili hilo jipya litakuwa sawa na lile ambalo Puma walitoa wakati wanaiponya timu hiyo Nike, waliokuwa wadhamini wa Arsenal tangu 1994.

This Is It! A picture of a potential new kit, the same one as Henry was wearing, was leaked on Twitter
Hii iko hivi! Picha ya jezi mpya ya Arsenal, ambayo ni sawa na ile aliyokuwa anavaa Henry, imevuja kwenye Twitter
Sorted: Chief executive Ivan Gazidis (right) shakes on the deal with Puma's CEO Bjoern Gulden
Mtendaji Mkuu, Ivan Gazidis (kulia) akipeana mikono na Mtendaji Mkuu wa Puma, Bjoern Gulden
Done deal: The Gunners announced the long-term contract with Puma at a press conference on Monday
Dili imetiki: The Gunners imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu na Puma katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jumatatu.

<BIN ZUBEIRY>

A-Z MSANII BONGO MOVIES ALIVYOJINYONGA

Mwili wa marehemu Victor Peter ukipelekwa mochwari.
SAKATA la kujinyonga kwa msanii wa filamu Bongo, Victor Peter limegubikwa na matukio tofauti ya kustaajabisha ambayo marehemu aliyafanya siku kadhaa kabla hajapatwa na umauti, Ijumaa limefukunyua kila kitu.
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, Hamisi Koba, msanii huyo alijinyonga usiku wa Februari 27, mwaka huu mkoani Tanga ambapo marehemu alifika jijini humo kuigiza filamu yake iitwayo Our Family.
Hamisi alisema Victor aliwasili jijini humo akiwa na timu ya wasanii sita na kufikia kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Safari Junior iliyopo maeneo ya Kisosora ambapo punde walianza kushuti filamu hiyo ambayo yeye na Mzee Jengua ndiyo walikuwa wahusika wakuu.
Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.
“Mimi ndiye nilikuwa kama mwenyeji wake mkubwa hapa Tanga, alikuwa ni mpole na siku zote tulipokuwa kazini kwa ajili ya kushuti filamu hiyo aliniambia mambo mengi kuonesha amejipanga kuhakikisha anaifikisha mbali.
“Victor alitokea Mwanza, akaenda Dar ambapo alifika na kuandaa filamu yake ya kwanza aliyoiita Chozi ambayo tayari ilikuwa imekamilika na kuiuza kwenye Kampuni ya Kapiko ya jijini humo,” alisema Koba na kuongeza:
“Filamu hiyo ilikuwa bado haijatoka, akaamua kuja Tanga kuandaa filamu hiyo ya pili ambayo nayo ilikamilika juzi. Naumia sana ninapokumbuka mipango yake maana alikuwa ana ndoto za kufanya makubwa.
Wasanii wenzake na marehemu wakilia kwa simanzi.
“Siku ya Januari 27 tulipokuwa tunakamilisha filamu, kuna muda alikuwa anaonekana kama ana wenge hivi... alipomaliza kushuti sehemu yake tulienda benki, akachukua fedha na kuwalipa wasanii wote.”
Akiendelea kutiririka juu ya tukio hilo, Koba alisema marehemu alionesha kama alikiona kifo chake kabla kwani aliuliza mara mbilimbili kama kuna mtu anamdai ili amlipe.
“Wakati anatupatia fedha kila mara alikuwa anauliza kama kuna mtu anamdai hadi tuliingiwa wasiwasi na ingawa wengine walisema atakuwa amefurahia labda kumaliza muvi yake,” alisema.
Koba alizidi kueleza kuwa, marehemu akiwa na furaha ya kumaliza muvi hiyo, alikwenda chumbani kwake na kujifungia lakini alfajiri (Januari 28) walipomgongea mlango waligundua amejinyonga.
Baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
“Tulichungulia kupitia tundu la funguo tukaona kama ananing’inia ndipo tukaenda kwenye kituo cha Polisi cha Chumbageni na kuchukua askari ambao walishirikiana na mwenye gesti hiyo kuvunja
mlango na kumkuta kajinyonga, tukachukua mwili na kuupeleka kwenye Hospitali ya Bombo, mipango ya kuusafi risha mwili kwenda Kahama nyumbani kwao imeanza,” alisema Koba na kuongeza:

“Kwenye hiyo filamu yake, stori ilikuwa mzee Jengua kama baba wa Victor ambapo Mzee Jengua alikufa na baadaye Victor anakufa kiajabu, kifo kimempata kweli.”
Kuhusiana na kifo hicho, Koba alisema kilimuuma kwani alikilinganisha na kile kilichomtokea marehemu Steven Kanumba ambaye pia aliigiza filamu ya Power of Love ikionesha anakufa, akafa kikwelikweli.
Mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Bombo ulitarajiwa kusafi rishwa juzi kwenda nyumbani kwao Kahama kuzikwa.

<GPL>

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA WAKANUSHA UZUSHI WA NEWS OF RWANDA

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz 
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120, 
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ubalozi wa Tanzania katika Rwanda usiku wa jana, Jumatano, Januari 29, 2014 ulitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikikanusha habari za uongo na uzushi ambazo ziliandikwa mwishoni mwa wiki na gazeti la Serikali ya Rwanda la News of Rwanda.

Ifuatayo ni taarifa kamili iliyotolewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mheshimiwa Francis Mwaipaja:

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

30 Januari, 2014


STATEMENT ON CLAIMS BY THE NEWS OF RWANDA

The Embassy of Tanzania in Rwanda is deeply saddened by malicious and untrue reports, published over the weekend by the Rwanda Government Owned Newspaper, The News of Rwanda, in which it accuses the President of the United Republic of Tanzania, HE Jakaya Mrisho Kikwete, of supporting and holding meetings with members of rebel groups opposed to the Government in Kigali.

Indeed, these reports are nothing but a bunch of dangerous lies fabricated by editors of this publication with obvious malicious intent to attack the person of the President of a friendly neighbouring country and create an impression that Tanzania is working with enemies and groups opposed to the Government of Rwanda.

The News of Rwanda, which has gained uneviable notoriety of reporting and publishing malicious, dangerous and perpetual propaganda, quoting unnamed sources claims, among other things, that two founding members of the Rwanda National Congress (RNC) including Dr. Theogene Rudasingwa met secretly in Dar es Salaam with top commanders of the Democratic Forces for Liberation of Rwanda (FDLR).

Given the enormity and dangerous nature of these reports, the Embassy of Tanzania in Rwanda would like to make the following clarification:

1. That the so called founding members of Rwanda National Congress, Dr. Rudasingwa and adviser Condo Gervais together with top commanders of FDLR, namely Lt. Col Wilson Irategeka and Col Hamadi were not in Tanzania last week. Indeed, our records do not show that they have visited Tanzania in the recent years.


2. That, there was no meeting of any kind at any official residences of President Kikwete, either in Dar es Salaam or in Dodoma or anywhere. Indeed, President Kikwete has never met any of those people mentioned anywhere – in Tanzania or outside. Moreover, on the day that News of Rwanda claims that the meeting took place, Thursday 23rd, this month, the President was not even in the country – he was in Davos attending the meeting of the World Economic Forum (WEF).


3. That, the former Prime Minister of Rwanda Faustin Twagiramungu was also not in Tanzania on any or the same mission and did not attend the meeting with representatives of RNC and FDLR as no meeting of such nature took place in Dar es Salaam or anywhere in Tanzania as alleged by this paper. The Immigration Department in Tanzania does not have a record of such people entering or exiting the country.


4. That, The Tanzania Immigration Department has never issued any travel document to any Rwandan citizen including those claimed in the News of Rwanda that they travelled to Mozambique using Tanzanian passports on or around December 20th 2013. It is not the business of Tanzania to issue travel documents to citizens of other countries.


5. That it is also untrue that the so-called, “insider establishment” in Tanzania is providing the base for organization and facilitation for travel for FDLR fighters. It is open secret that there is no presence of even a single FDLR fighter in Tanzania. The News of Rwanda should know better where these fighters are based and operate from.
As mentioned earlier, this report and other similar reports published in recent weeks by the News of Rwanda are not only untrue, baseless and mere fabrication but also dangerous and threatening to the excellent and sound diplomatic and social relations between our two neighbouring countries, both of which are members of the East African Community (EAC).

President Kikwete is deeply hurt by these lies and his humble advice to the editors of this publication is to stop fabricating untrue claims which potentially could create and fuel animosity and confusion among the people of our two neighbouring and friendly countries. At a time when President Kikwete and President Paul Kagame of Rwanda had agreed in Kampala to foster friendly relations, such newspaper claims can only sour the atmosphere and President Kikwete would like to know what the editors of the publication are up to?

The Embassy of Tanzania in Rwanda does not take lightly these allegations by the News of Rwanda given the position that this publication occupies in Rwanda.

WASTARA: NIKIKUMBATIWA NAKUWA HOI

Wastara Juma.
MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia yoyote huwa hoi.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.
“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda kukumbatiwa.”
<GPL>

TAMKO LA JUMUIYA YA VIJANA KUUNGA MKONO KAZI YA SEKRETARIETI YA CCM


“..Chama Cha Siasa chochote duniani hubomoka kutokana na migongano iliyokithiri ya muda mrefu. Uzoefu wa vyama vikubwa vilivyoporomoka umeonyesha hivyo! Chama lazima kidhibiti uchu wa madaraka wa baadhi ya viongozi wake na ndani ya serikali yake...” – Dr Eginald P. Mihanjo

“..Chama cha siasa ni itikadi. Chama cha siasa ni siasa kwa maana halisi ya neno lenyewe siasa –“siasa”. Ni mahali ambapo watu wenye madhumuni mamoja yaliyoainishwa waziwazi hukutana na kuwa kitu kimoja. Chama cha siasa sio mkusanyiko wa “majini dume yenye tamaa”, - majini ambayo yametanguliza mbele tamaa kufa na kupona-tamaa ya kutengeneza pesa au kupata vyeo kwa gharama yoyote! – Dr Bashir Ally

UTANGULIZI:
Hili ni tamko la vijana makini wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono juhudi na utendaji wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Katibu Mkuu Komredi Abdulrahaman Kinana.
Maneno ya utangulizi yamebeba dhima ya tamko hili, kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vikiwanukuu baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, wakiwatuhumu Viongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.
Sisi Vijana tunatambua kuwa tuhuma hizo na maneno hayo ya hovyo yametolewa kwa nia ovu yenye kulenga kuwakatisha tamaa Viongozi hao wa Chama. Tunafahamu kuwa upo mkakati wa kiuhaini ulioandaliwa na kuratibiwa na “mtandao” ndani ya Chama ambao umejipanga kuendesha uhaini huo.
Sisi vijana wa UVCCM tunatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga na kukiimarisha Chama kwa kuisimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake, katika umri wetu hatukuwahi kuona Chama kikiwa karibu na wananchi kwa kufuatilia, kusikiliza na kushiriki katika utatuzi wa kero, shida na changamoto zao kama ilivyo katika kipindi hiki chini ya Comrade Kinana na timu yake. Juhudi hizi ni za kuungwa mkono na kamwe si za kubezwa na mwanaCCM muadilifu, muaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Chama.
Juhudi za kukiimarisha Chama kutoka ngazi za chini, kwa mabalozi ni mkakati bora kuwahi kutekelezwa na Chama, kukirudisha Chama kwa wanachama ni kutimiza lengo la kuundwa kwa Chama hiki, Chama hiki ni cha wanyonge, masikini wa Taifa hili, HAIWEZEKANI matajiri watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema tutakilinda Chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu.
Ni hawa ambao wanabezwa leo ndio wameweza kurudisha Imani ya wananchi kwa Chama, Imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na Chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wan chi hii.
Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliozunguka kwenda kukutana na wakulima wa Pamba kule mikoa ya Kanda ya ziwa na kumpeleka balozi wa China na kumshawishi kujenga viwanda ili kuboresha manufaa kwa wakulima.
Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliokwenda Kusini kukutana na wakulima wa Korosho na kushirikiana nao pamoja na bodi kutatua tatizo la Korosho.
Ni Comrade Kinana na timu yake ndio walioibua hoja na kero za wafugaji, walimu na wananchi kwa ujumla, na kuwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi walipa kodi wa Taifa hili.
Kupinga mafanikio ya Ziara hizo ni kupinga utetezi wa wanyonge.
Mtu anayebeza ziara hizo na kuwaita Viongozi waliozifanya waropokaji na wahuni wahuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo,hana maadili, asiyekipenda Chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.
TAMKO hili limezingatia wosia wa Baba wa Taifa, muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika kitabu Chake TUJISAHIHISHE.
“Inapofikia wasimamizi wa Kanuni za Chama wanapigwa vita ya wazi kwa uamuzi wao wa kukisimamia Chama, tafsir yake ni moja tu watu wanaowapiga vita hawakitakii mema chama chetu.”

Imetolewa na Paul Christian Makonda.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi.

SHILOLE ANASA KWA MZUNGU


KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyokwenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni atakwenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.
“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole.

<GPL>

MALECELA AUNGA MKONO KAULI YA PAUL MAKONDA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI --30/01/2014


Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.

Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?

Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.

Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.


JOHN SAMWELI MALECELA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS SASA!

Kuwa wa kwanza kupata Breaking News za wasanii, watu maarufu na zingine kutoka Magazeti Pendwa ya IJUMAA WIKIENDA, UWAZI, RISASI, AMANI, IJUMAA na CHAMPIONI moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa shilingi 100 tu kwa SIKU!
Kujiunga tuma GLOBAL kwenda 15778
Huduma hii ni kwa watumiaji wa Vodacom pekee. Kwa maelezo zaidi LIKE Ukurasa wetu wa Facebook hapa: http://on.fb.me/L0OSPD

VIJANA WATAKAOIGA TAMADUNI ZA NJE KUCHAPWA VIBOKO 60 HADHARANI


Na Mwandishi Wetu, Meru

UONGOZI wa Kimila ujulikanao kama 'Rika la Kilovio' kutoka katika kabila la Wameru umepitisha sheria kali ya kudhibiti maadili kwa vijana wa kike na wa kiume, hasa wale wanaoiga tamaduni za mataifa ya nje, ambapo watakaokiuka watachapwa viboko 60 hadharani.
Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya vijana katika eneo hilo la Meru kuanza tabia ya kuiga tamaduni na madili ya mataifa ya nje hali inayochangia kwa kiwango kikubwa kuporomoka kwa maadili.
Hayo yameelezwa na Akundaely Mbisse ambaye ni kiongozi wa marika ya vijana katika kabila hilo wajulikao kama "Kilovio" wakati wakimsimika na kumuingiza rasmi kiongozi wa vijana katika eneo hilo la Mareu, Herieli Mafie, mapema jana.
Mbisse alisema utaratibu huo wa adhabu ya viboko 60 utaweza kurudisha maana halisi ya kijana wa kabila hilo ambapo kwa sasa jamii ya Mkoa wa Arusha bado inaonekana kuendelea kuelemewa na tatizo la vijana wengi kuiga tamaduni za nje ya nchi huku hali hiyo nayo ikichangia hata ubaribifu wa amani ya kaya, hadi mkoa.
Alifafanua kuwa adhabu hiyo ya viboko 60 hadharani itaenda sanjari na vijana wote wenye tabia mbalimbali ambazo hazina tija kwenye jamii hiyo ya Meru kama vile uzinzi, ulevi wa kupindukia saa za kazi, wizi, mavazi yanaonesha maumbile, ukosefu wa adabu pamoja na makosa mengine ambayo chanzo chake ni kuiga maadili yasiyokuwa na tija kwennye jamii.
"Tumejipanga kuhakikisha wilaya ya Meru inakuwa na tofauti katika suala la mila kwani tunao uwezo wa kuwaweka vijana wetu wawe katika maadili mazuri, masuala kama ya uvaaji wa nguo za ajabu utakwisha na kwa hali hiyo jamii itaweza kupungza hata ujinga unaofanywa na baadhi ya vijana wachache huku wakisingizia umaskini," aliongeza Mbisse.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, John Palangyo, alisema kuna umuhimu mkubwa wa maadili ya kila kabila kurudiwa ili kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao ya kila siku.
Palangyo alisema suala la kulinda maadili lina manufaa siyo kwa vijana bali hata kwa taifa kwani kwa sasa wapo baadhi ya vijana ambao wanaharibu na kuvunja amani ya nchi kwa kuwa hawana maadili ambayo yanaanzia ngazi za marika hadi taifa.
"Hili jambo la kuwaweka vijana katika mazingira mazuri ya kimaadili linawezekana kabisa na sisi Watanzania tunatakiwa kuondokana na dhana potofu kuwa eti vijana wa sasa hawana maadili.
"Wa kuwafundisha maadili ni sisi wazee wa ukoo, rika, na hata wanasiasa, hivyo basi kila mtu anatakiwa kuzingatia hili lakini pia kuona kuwa kijana wa mwenzake ni wa kwake na kama ataharibikiwa basi atachangia uharibifu bila kujali anaharibu kwa nani," aliongeza Palangyo.

Thursday, 30 January 2014

SIRI YA USALITI CHADEMA

JUMAPILI, JANUARI 26, 2014

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amefichua siri ya madai ya usaliti ndani ya chama hicho.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Profesa Baregu alisema kiini cha tuhuma na madai ya usaliti ndani ya Chadema ni kutoaminiana na kukosekana kwa uvumilivu.
Alisema kitendo cha wanachama na viongozi kunyoosheana vidole vya usaliti kinakiangusha chama na kwamba Chadema kimefeli katika mambo matatu, ambayo ndiyo yanapaswa kuwa msingi wa chama na kama yangezingatiwa mapema, hoja ya usaliti isingezungumzwa leo.
Aliyataja mambo hayo yanayozalisha hoja nzito ya usaliti iliyosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho kuvuliwa uanachama kuwa ni kusikilizana, kuvumiliana na kuaminiana.
“Kukosekana kwa mambo hayo ndio kiini cha kuibuka kwa hoja ya usaliti, hatua hii ni mbaya katika maendeleo ya chama kinachojijengea uaminifu kwa wananchi,” alisema.
Alisema kuendelea kwa hali ya kushutumiana ndani ya chama kunasaidia kukitafuna na ipo siku Chadema haitakuwa na mtu msafi, kwani wote wataitana wasaliti.
“Chadema ni chama kizuri cha siasa, lakini kimefeli kabisa katika kuyadhibiti mambo hayo matatu muhimu, nadhani hili ni tatizo kubwa linalokiandama chama hiki.
“Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati chama hakitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti,” alisema Profesa Baregu.
Akizungumzia mgogoro wa hivi karibuni ndani ya chama hicho uliosababisha Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo kuvuliwa uanachama, huku Zitto Kabwe akikimbilia mahakamani, Profesa Baregu alisema hayo ni madhara ya kutotumia hekima na kukosekana kwa busara ya kumaliza tofauti kwa mazungumzo.
“Kama hamsikilizani wala kuaminiana, lazima athari ziwepo, tena kubwa tu, kwa sababu matukio ya namna hiyo yanakuwa endelevu, leo kashutumiwa huyu ni msaliti, huwezi kujua mwingine atashutumiwa lini …na mvurugano uliotokea hivi karibuni ndio uhalisia wa kile nilichokisema hapo awali, kwamba ndani ya Chadema kumekosekana utamaduni wa kumaliza tofauti kwa mazungumzo, kwa ujumla watu hawavumiliani wala kusikilizana,” alisema Profesa Baregu.
Aidha alitahadharisha kwa kusema, usaliti utakidhoofisha chama kwa kiasi kikubwa, ambapo alikitolea mfano Chama cha NCCR-Mageuzi, ambacho kilikumbwa na mazingira kama hayo na mwisho wake kikaparaganyika ovyo kwa sababu kila mtu alijikuta anatazamwa kuwa msaliti.
Wakati huo huo, imebainika kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini haijatoa mwongozo wowote juu ya barua iliyoandikiwa na Mwigamba, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha. Mwigamba aliitaka ofisi hiyo iingilie kati suala la kunyofolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama hicho.
Inaelezwa kuwa Mwigamba alifikia hatua ya kuandika barua hiyo kabla hajavuliwa uanachama, ambapo alifanya hivyo baada ya kutokea sintofahamu baina ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto, Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na wafuasi wanaomuunga mkono Mbowe.
Akithibitisha madai hayo, Mwigamba alisema ni kweli kuwa alimwandikia barua Msajili, ambayo ilikuwa ikihoji ukiukwaji wa katiba ya chama pamoja na kuondolewa kwa kipingele cha ukomo wa muda wa uongozi, hata hivyo mpaka sasa hajapatiwa majibu.
Alisema mara baada ya kuandika barua hiyo, Msajili aliwaandikia Chadema ili kupata ufafanuzi wa madai hayo, ambapo walijibu kuwa walisambaza waraka kwa makatibu wa chama hicho wa mikoa ili kupata uungwaji mkono kabla ya kukiondoa.
Hata hivyo, Mwigamba alilalamikia hatua hiyo kwa madai kuwa inakiuka katiba na utaratibu wa chama hicho na kwamba barua iliyosainiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Shaibu Akwilombe, Julai 13, 2006, kwenda kwa makatibu hao ilikuwa ikiwaarifu kuwa yanapelekwa mapendekezo ya ziada.
Kwamba waunge mkono pendekezo kuwa Katibu Mkuu na manaibu wawili wateuliwe na Mwenyekiti, wasipigiwe kura na majina yao yapelekwe Baraza Kuu kwa ajili ya kupiga kura kuchagua mmoja.
“Katiba ya mwaka 2006 isomeke pia kiongozi anaweza kuchaguliwa tena na ndiyo walileta mapendekezo na mwanzo mpaka mwisho wa barua ilikuwa inaongelea mapendekezo tu. Msajili alinitumia nakala ya majibu yao ili nitoe maelezo ya ziada, ambayo pia nilishafanya hivyo tangu Desemba 30 mwaka jana,” alisema Mwigamba.
Alisema kuwa katika majibu ya Chadema ya Desemba mwaka jana kwa Msajili, yalionesha wazi kwamba Mwigamba alishavuliwa uanachama wa chama hicho, wakati alikuwa bado hajafukuzwa, ambapo walidai kwamba kipengele hicho kilifanyiwa marekebisho.
“Nilimweleza Msajili kuwa katiba ya Chadema, inataka mapendekezo ya katiba yapelekwe kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, siku 30 kabla ya mkutano huo, ukizingatia kikao cha Mkutano Mkuu kilifanyika Agosti 13, 2006 na kufanya mabadiliko ya Katiba Julai 13, mwaka huo huo ndiyo iliandikwa barua, sasa hata kama barua ingesafirishwa kwa ndege ama kwa usafiri wowote lazima zingeanza kupokelewa kuanzia Julai 14 mpaka 16, hapo tayari siku zimepungua, si 30 tena,” alisema Mwigamba.
Alisema kuwa waraka huo uliosambazwa kwa wajumbe ulitakiwa kuwafikia siku 30 kabla na kwamba haukueleza iwapo mapendekezo hayo yaliandaliwa na Baraza Kuu ambalo linatoa mapendekezo kwa Mkutano Mkuu au la!
Alisema waraka huo, ambao alibahatika kuuona, ulikuwa hauna uzito unaostaili, kwani ulikuwa sawa na barua ya uchumba ambayo ni tofauti na cheti cha ndoa unachoweza kupeleka ushahidi Mahakamani.
Anasema wakati barua ya Akwilombe ikisambazwa ilikuwa pamoja na rasimu, ambapo yeye (Mwigamba) akiwa mmoja wa Makatibu wa Wilaya hakuona nakala yake.
Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ili kupata ufafanuzi, hata hivyo hakuweza kupatikana, kutokana na kuwa katika vikao, huku simu yake ya kiganjani ikiwa haipatikani.
Alipotafutwa Msemaji wa Chadema, Tumaini Mkene, alishindwa kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa, ambapo alisema suala hilo lilishazungumzwa katika mkutano wa waandishi wa habari na majibu yake yanajitosheleza.

JF chanzo.

MRITHI WA RAIS KIKWETE HUYU HAPA

TUSIUMIZE VICHWA BURE
MRITHI WA RAIS KIKWETE HUYU HAPA
 
Na Mwandishi Maalum
Mwenendo wa upepo wa kisiasa ni vigumu kuwa na utabiri wa kuaminika kutokana na ukweli kuwa wakati wowote hubadilika na kugeuza mwelekeo. Hali hii inatokana na ukweli ambao hauzuiliki unaotokana na hali ya kimaumbile ya binadamu ya kuwa daima ya hamu ya kutaka mabadiliko hata bila ya kujua atafaidikaje na mabadiliko hayo.
Ni kwa silika hii baadhi ya watanzania hasa vijana wasiojua nchi ilikotoka, imefikia wapi na inataraji nini sasa na kwa mustakbali, waliweka matumaini yao kwenye vyama vya upinzani kama njia ya kufikia mapinduzi ya hali zao hasa za kiuchumi kwa dhana kuwa hali ngumu ya uchumi waliyonayo inasababishwa na chama tawala CCM.
Matumaini ya wenye nadharia ya kuhitaji mabadiliko kwa mujibu kisilika ya kibinadamu tu,  na ambao  wengi wao ni vijana wadogo, wameweka tumaini lao kwenye vyama vya upinzani hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho katika chaguzi zilizopita kilifanya vizuri ukilinganisha na vyama vingine vya upinzani.
Hata hivyo matumaini hayo yamefifia katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja uliopita, baada ya kuzuka malumbano makubwa na kutoaminiana baina ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.
Katika kipindi cha mwaka mzima wa 2013 viongozi wa Chadema wamejishughulisha zaidi na mapambano ya ndani badala ya kuimarisha chama, kitendo ambacho kimekidhoofisha na kukirejesha nyuma lakini pia kuwakatisha tamaa watanzaniajuu ya uwezekano wa chama hicho kukiangusha Chama tawala katika uchaguzi wa mwaka 2015.
 Hali ya mapambano ndani ya chama hiki kikuu cha upinzani kumekinufaisha chama cha Mapinduzi ambacho watendaji wake wakuu walitumia mwanya huo kukiimarisha chama chao na kuwajengea wananchi dhana ya kupuuza upinzani huku serikali ikishadidisha kusimamia miradi ya maendeleo ambayo ni mtaji wenye nguvu kisiasa mbele ya jamii.
Kitendo cha kutuhumiwa Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe na wenzake kuwa wasaliti wa chama hicho kwa kutumiwa na CCM, kitaendeleza dhana mbili endelevu zilizo muhimu na zinazohitaji tafakuri.
Kwanza ni kuwa, kuna udhaifu mkubwa ndani ya uongozi wa Chadema ngazi ya Taifa kwa kiasi kwamba CCM imeweza kupenya na kuingia ndani na kufaulu kujenga dhana ya kutoaminiana na kuusambaratisha uongozi.
Pili, Chadema watapaswa kufahamu kuwa ikiwa vyanzo vyao vya uchunguzi vimebaini kuwa CCM ilijipenyeza ndani yao kwa kiasi kinachoelezwa, ni wazi pia bado ndani ya Chadema kuna CCM wengine ambao wana jukumu la kuendeleza wimbi la kutoaminiana na hivyo hali ya mambo bado si shwari.
Kwa ujumla katika uwanja wa siasa za vyama vingi bado CCM inatawala kwa kigezo cha ukweli kuwa inamiliki serikali na vyombo vyake na hakuna shaka kuwa vyombo hivyo kwa pamoja vitaendelea kuhakikisha vinailinda Ikulu kuangukia mikononi mwa wapinzani na njia mojawapo ni kuwasambaratisha wapinzani kama walivyofanya kwa NCCR-Mageuzi.
NCCR-MAGEUZI ni chama kilichokuwa na nguvu kubwa lakini kama ambavyo kila mmoja wetu anafahamu hadi leo chama hicho  kinachechemea baada ya kutokea machafuko ya ndani kama haya tunayoyaona sasa ya Chadema ambayo kuna kila dalili inayoonyesha virusi vya ugonjwa huu kiasili vinategenezwa na CCM.
Chama cha Wananchi (CUF) kama vyama vingine vya upinzani kinaendelea kushuka chati baada ya kuwa na magomvi ya ndani ambayo tunaweza kuyaita ni maradhi ya wapinzani. Chama hiki katika sura yake halisi kinaonyesha uhai wake uko mikononi mwa mtu binafsi.
Ukiondoa visiwani Zanzibar ambako Maalim Seif Shariff Hamad ni mwanasiasa nyota anayeng'ara kwa siasa za upinzani visiwani humo, CUF hakina mvuto wa kisiasa popote Tanzania Bara na kila uchaguzi mkuu wa Rais unapofanyika Chama hicho huzidi kupoteza umaarufu wake na kudidimia.
Kwa upande wa demokrasia ndani ya vyama vyote viwili vikuu vya upinzani CUF na Chadema havina demokrasia ya kweli ndani yake ukilinganisha na CCM. Mfano mdogo ni huu kwamba haihitajiki mkutano mkuu ndani ya Chadema wala CUF kumtambua nani atakuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa Bara au Visiwani na anayejaribu kuhoji jambo hilo hapana shaka atafukuzwa si tu uongozi bali hata uanachama wa chama chenyewe.
Sasa kama nilivyotanguliza kusema awali upepo wa kisiasa hubadilika, lakini hadi sasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais wa mwaka 2015 hakuna matumaini yanayoonyesha kuwa mrithi wa Dk Jakaya Kiwete atatokea chama cha upinzani, bali bado upepo unaashiria kuendelea utawala wa CCM.
Kuwapo kwa wanasiasa wengi wenye kujikweza kwenye dhana ya sifa za kugombea nafasi hiyo, kunakiweka chama cha Mapinduzi katika wakati mgumu kutokana na makundi yaliyomo ndani kugombea nafasi hiyo muhimu katika taifa.
Ukweli wenyewe ni kuwa Rais JK ana wakati mgumu sana katika shughuli ya kuutua mzigo wa uongozi wa Chama chake kwa sababu huenda chama hicho kikasambaratika kabisa au kikapata ushindi kiduchu utakaokipa serikali dhaifu yenye kutegemea maridhiano na upinzani endapo vita ya kugombea urithi wa kiti cha rais ndani ya CCM haitodhibitiwa.
Ndani ya CCM kuna hazina kubwa ya viongozi wenye maadili na uwezo mkubwa kiuongozi lakini wamekuwa kimya na hawaoni busara ya kujitokeza na kujitangaza kufaa kwao kwa sababu maadili mema hayamfundishi mtu mwadilifu kujitukuza na kujinaki kwa kujipa sifa mwenyewe.
Pengine wapenzi wa wanasiasa wa kambi mbali mbali hawawezi kufurahia uchambuzi huu, lakini ni ukweli usioepukika kuwa Edward Lowassa kwa sasa anatambulika kuwa ndiye mwana-CCM aliyejipanga na kufanikiwa kuwarubuni wana-CCM wengi kuamini kuwa yeye ndiye rais ajaye.
Lowassa anafahamika kama mwanasiasa hodari, mwenye haiba na shakhsiya, hutambulika pia kama mtu mwenye maamuzi na uwezo mkubwa wa kusimamia maamuzi yake. Mwandishi wa uchambuzi huu ni mmoja wa watu ambao wasingependa Lowassa ashike nafasi ya Urais, lakini chuki na utashi wake binafsi hauna nguvu ya kuzuia ukweli kusimama mahala pake.
Lowassa ameshikilia turufu kutokana na uwezo wake mkubwa kifedha ambao ameutumia bila ajizi kuugawa kwa mahitaji ya kijamii hususan kupitia taasisi za kidini na kumfanya Lowassa kukubalika zaidi Makanisani.
Lakini hata hivyo Lowassa bado hajamaliza tofauti zake na Waislamu wanaomtazama kama mdini kutokana na kusaini mkataba  (Memorandum of understanding) baina ya Serikali na Wakristo unaoipa jamii hiyo fursa ya kufaidika na fedha kutoka serikalini.
Lowassa ambaye alijiuzulu nafasi ya waziri mkuu kutokana na kashfa ya kampuni iliyodaiwa kuwa hewa ya kufua umeme ya Richmond, licha ya kugawa mamilioni ya fedha kila anapoalikwa bila ukomo, amekuwa akikanusha kuwa yeye si tajiri na kwamba nyuma yake wako watu ambao anawaita marafiki wanaochangia mamilioni hayo.
Jambo ambalo wengi wanajiuliza bila kupata jibu kuhusu suala la fedha  anazogawa Lowassa ni je, hawa marafiki zake wanaojitolea mamilioni haya wana nia gani katika utoaji wao? Marafiki hawa wema kiasi hicho ni watanzania au ni raia wa kigeni? Nini madhumuni yao katika kumjenga Lowassa kupitia njia ya kumwaga mapesa?
Wanategemea kupata nini kwa Lowassa akishaingia Ikulu? Akiwa Ikulu Lowassa anategemea kuwa na hiyari juu ya wafadhili wake hao? Wafadhali hao hawawezi kuwa na kauli yoyote juu ya mfadhiliwa? Je haiwezi kuwa watu hawa wana nia ya kumfanya Lowassa akubalike ili baadae ajikute kuwa rais wakala wa wawezeshaji wake?
Uchunguzi wa uhakika wa mwandishi wa dodoso hili unaonyesha kuwa uongozi wa CCM katika mikoa mingi unamuunga mkono Lowassa kwa kiwango kwamba kuna tetesi kuwa kuna baadhi ya viongozi kimkoa wanapata posho zao ama kwa Lowassa mwenyewe au kwa watu wanaodhaniwa kuwa wapenzi wake.
Kwa kuzingatia udhaifu wa vyama vya upinzani, na dhana kuwa mgombea wa CCM ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuwa rais, na kwa namna Lowassa alivyojipanga ndani ya chama, na ukweli kuwa endapo jina la Lowassa litaingizwa katika mkutano mkuu hakuna wa kumshinda, basi hapana shaka Lowassa ana nafasi ya kuwa mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.
Hii si maana yake kuwa Edward Lowassa ndiye pekee mwana-CCM anayefaa kwa nafasi hiyo. Wapo wengine wanaotajwa tajwa na ambao wana sifa bila dosari za wazi japo hawana mamilioni ya kumwaga akiwemo Benard Membe,  Dk Hussein Mwinyi, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Asha Rose Migiro.
Wengine ambao wanatajwa kuwa wanafaa ni pamoja na Dk Harison Mwakyembe, Anne Makinda, Dk John Magufuli, na pia kuna wengine kama Samuel Sitta na waziri mkuu mstaafu Fredirick Sumaye.
Kwa kadiri ya mjadala huu utakavyoendelea jambo kubwa la msingi linaloweza kutokea ni CCM kusambaratika baada ya jina la Lowassa kuondolewa katika kinyang'anyiro cha urais na Lowassa naye akajibu kwa kuamua kujiondoa ndani ya chama hicho.
 Endapo jambo hilo litatokea CCM itagawanyika vipande ambavyo ama vitawapa nguvu wapinzani kuchukua nchi au CCM kupata ushindi kiduchu utakaokifanya kuwa na rais atakayekuwa na wabunge wachache na hivyo kuongoza serikali dhaifu.
Naomba nihitimishe makala hii kwa kuwakumbusha wanaogombea nafasi ya urais na wapambe wao kuwa mbali na kampeni zao wenyewe wasije wakasahau kuzihusisha jitihada zao na matakwa ya Rais Kikwete kama kiongozi wa nchi, lakini pia Kikwete kama mtu mwenye shakhsiya na mvuto maalum wenye nguvu na ushawishi wake binafsi.
Lakini kubwa kuliko yote msilolijua wagombea masikini na matajiri, ni hilo la kuwa Rais wa Tanzania atakayemrithi Jakaya Kikwete ni huyo hapa, "Mgombea ambaye ataungwa mkono na Jakaya mwenyewe iwe wakati huo kikatiba anaruhusiwa kumfanyia kampeni au haruhusiwi.

Nafahamu kuwa wako watakaosema ya kuwa hata viongozi waliomtangulia JK walishindwa kuwaweka warithi waliowataka wao kwa kuwa walikinzana na upepo wa kisiasa. Lakini upepo wa kisiasa unaotoa ishara ya kubadilishana uongozi baina ya Rais Kikwete na mrithi wake uko wazi kuwa miongoni mwa watu anaowafikiria yeye basi mmoja wao ndiye atakayemrithi.  Kama wengine walishindwa kuna kila uwezekano JK hatoshindwa. Kwa hiyo usisumbuke na kuumiza kichwa chako bure atakayeungwa mkono na Kikwete mwenyewe ndiye rais ajaye.
<WANABIDII>

KIFO CHA MCD, SIMULIZI INAUMA


KIFO cha aliyekuwa mpiga ngoma (tumba) maarufu wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Soud Mohamed ‘MCD’ kimeacha simulizi inayouma, Amani linalia sanjari na ndugu.
MCD ambaye Agosti 4, 2013 alimpoteza baba yake mzazi, alifariki dunia usiku wa kuamkia Januari 28, mwaka huu katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Simulizi inayouma ya mwanamuziki huyo ilianzia mwishoni mwa mwaka jana ambapo akiwa na bendi yake katika ziara ya kikazi mikoa ya Kanda ya Ziwa, wakati wa kurejea Dar, MCD aliuomba uongozi umruhusu aende nyumbani kwao Majengo Moshi, Kilimanjaro kupatiwa matibabu na kuwa karibu ya uangalizi wa ndugu zake.
Luiza Mbutu akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mpiga tumba wao MCD.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani alisema uongozi ulimruhusu MCD kwenda kwao na kumuahidi kuwa naye karibu kwa kila hatua.
“Tulimkubalia kwenda kwao, lakini tulikuwa tukifuatilia hali yake kila siku,” alisema Rehani.

Rehani alisema: “MCD tulikuwa tukiwasiliana naye kujua hali yake, kabla ya usiku huu kupata taarifa za kifo chake watu wa hapa ofisini walizungumza naye vizuri tu mchana wake.”
Chanzo kingine kimeweka bayana simulizi hiyo inayouma kwamba, Jumatatu iliyopita, marehemu MCD alituma ujumbe kwa uongozi akisema hali yake  haiendi vizuri, hivyo viongozi wake waliamua kumtumia nauli siku ya Jumatatu ili arudi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
“Maskini, pesa ya nauli aliipata ili arudi Dar Jumanne (iliyopita) lakini akiwa anajipanga kusafiri hali ikazidi kuwa mbaya, akakimbizwa hospitalini ambako alifariki dunia. Kwa hiyo nauli yake ikanunulia sanda,” kimesema chanzo hicho.
Kikaendelea: “Si ajabu angewahi kusema hali yake si nzuri akatumiwa nauli mapema, akaja Dar leo hii tusingekuwa tunalia.
Juzi Jumatatu baada ya kupokea habari za kifo cha mwanamuziki huyo, baadhi ya viongozi wa Twanga waliwapigia simu wanamuziki wa bendi hiyo na kukutana kwa ajili ya kupanga taratibu za safari ya kwenda Moshi.
Aprili 27, mwaka jana, MCD aliondoka Twanga Pepeta na kwenda kujiunga na Mashujaa Music Band kabla ya kurejea tena.
Marehemu MCD amezikwa jana kwenye Makaburi ya Njoro, Moshi. Ameacha mke na watoto wawili. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.
Wakati huohuo, taarifa za kifo cha msanii wa Kundi la Futuhi, Omary Majuto maarufu kama Mzee Dude zimelishtua Jiji la Mwanza na kuwafanya baadhi ya watu kukaa kwa mafungu kumzungumzia marehemu.
Mzee Dude enzi za uhai wake.
Kifo cha Mzee Dude, kilimtikisa pia msanii maarufu nchini, Kulwa Kikumba ‘Dude’  baada ya  baadhi ya watu kudhani kwamba yeye ndiye aliyefariki dunia.
Dude alilazimika kuwapigia simu baadhi ya ndugu na  marafiki na kuandika katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Facebook kuwafahamisha kwamba yeye ni mzima wa afya njema.
<GPL>

BARUA KUTOKA CHINA: VIGOGO WA DAWA ZA KULEVYA (10)


v2catholic.china8.org

TUMETOKA MBALI... TOKA MBALI... TOKA MBALI!

Unatuona lakini?

MATUKIO YA UJANGILI WA CHUI NA TEMBO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

MATUKIO YA UJANGILI WA CHUI NA TEMBO 

Jumamosi, tarehe 19 Januari 2014, majira ya saa 12:45 jioni katika eneo la Yombo Vituka, Jijini Dar Es Salaam, askari wa wanyamapori wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Mashariki walifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa ujangili kwa jina Mwajuma Hamis. Mwajuma alikutwa akiwa na nyara za Serikali ambazo ni ngozi mbili za chui ndani ya nyumba anamoishi kinyume cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009. Mtuhumiwa huyo amekabidhiwa kwa Polisi kwa hatua zaidi za kisheria na amefunguliwa jalada na. CHA/RB/564/2014. 

Pia, siku ya Ijumaa, tarehe 17 Januari 2014, jioni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, askari wa KDU kanda ya Mashariki walimkamata raia wa China aliyefahamika kwa jina la LING TIAN mwenye hati ya Kusafiria na. G28214172. Bwana Tian alikutwa akiwa na bangili 2 na mkufu 1 wenye golori 11 zilizotengenezwa kutoka meno ya tembo. Mtuhumiwa amefikishwa Polisi na kufunguliwa jalada na. JNIA/IR/16/2013 kwa hatua zaidi za kisheria. Mtuhumiwa huyo, ambaye kwa sasa yuko rumande, alikuwa anatokea Msumbiji kwenda China.

Serikali haitalala hadi majangili wote wanapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Ilani inatolewa kuwa Tanzania si kichaka cha kupitishia meno ya tembo au magendo ya aina yoyote. Wizara inawahakikishia wananchi kuwa imejizatiti vilivyo kupambana na vitendo vya ujangili katika mapori yote, maeneo yote ya mipaka ya nchi yetu na kwenye viwanja vyote vya ndege pamoja na bandari zote. 

Wizara inatoa pongezi kwa raia wote ambao wanaisaidia kuwabaini waalifu. Tunatambua kuwa wengi wa wahalifu ni raia walio miongoni mwetu. Tunawaomba wananchi waendelee kutoa kwa Wizara habari zinazohusu ujangili ili tuendelee kuwabana na hatimaye kuusambaratisha mtandao wa ujangili ili tusalimishe maliasili zetu na kuokoa uchumi wa nchi. 

Imetolewa na:
Chikambi K. Rumisha
Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii

MIRATHI YA KULOLA, FAMILIA YAMEGUKA

Marehemu Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake

SHETANI ana majaribu yake! Anaendelea kuifuatilia familia ya mtumishi wa Mungu aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Dkt. Moses Kulola.

Habari za karibuni, mpasuko mkubwa umeibuka baada ya kuwepo kwa sintofahamu dhidi ya mirathi ya marehemu huyo aliyefariki dunia Agosti 29, mwaka jana huku makundi mawili yakiibuka.
Awali, Mchungaji Katunzi aliibuka na kudai kuwa yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya ambapo tamko hilo lilipingwa na baadhi ya wanafamilia.

Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni Katunzi alitimuliwa nyumbani kwa marehemu Kulola akiwa amepeleka mchele na pesa taslimu shilingi laki tatu (300,000) alizodai ni sadaka kwa mjane wa marehemu.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT City Center, Florian Katunzi.
“Hivi karibuni Mchungaji Katunzi alikwenda kwa mjane wa marehemu akatimuliwa, walidai ni msaliti mkubwa wa familia.
“Wakati akitimuliwa nyumbani hapo maeneo ya Capripoint, Abel (mtoto wa marehemu) naye alimshambulia mchungaji huyo na kumwambia asirudi tena nyumbani kwa marehemu kwani amekiuka miiko ya uchungaji ya kiapo cha uaminifu,” kilisema chanzo chetu na kuomba hifadhi ya jina.
Pia kiliongeza: “Familia kwa sasa ina mpasuko mkubwa, kuna makundi mawili, wapo wanaomuunga mkono Mchungaji Katunzi na wasiomuunga.
“Kundi linalomuunga mkono linaongozwa na watoto wawili wa marehemu (majina tunayo).
Kundi jingine ni la mjane wa Kulola, Elizabeth Kulola linaundwa na watoto wa marehemu wakiongozwa na Abel aliyekuwa dereva wa marehemu, Mchungaji Dany, Goodluck, Mary, Anna, Janga Faith na Susan.

Mke wa marehemu Moses Kulola.
Mchungaji Dany Kulola kwa sasa yuko Marekani na inasemekana kuwa amechukizwa sana na kitendo cha ndugu wanaomuunga mkono Katunzi.
Marehemu Kulola alikuwa na watoto 13, waliofariki dunia ni Flora, Benjamin na Rachel.
Wosia wa marehemu uliopatikana hivi karibuni unaonesha kuwa, mjane wa marehemu ndiye mrithi halali wa mali zote.

Habari zaidi zinasema Katunzi ameshaitwa na wachungaji wa Kanisa la EAGT ngazi za juu na kumtaka ajitoe katika sakata hilo la mirathi lakini anaendelea kufuatilia.
Habari nyingine kuhusu sakata hilo zinasema kuwa, Jumapili iliyopita akina mama 150 wa Kanisa la EAGT Jimbo la Mwanza walikwenda nyumbani kwa marehemu baada ya kusoma habari kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi Toleo Namba 1074 la Januari 25-28, 2014 likiwa na kichwa cha habari; Mgogoro Mzito Mirathi ya Kulola.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, akina mama hao walimuombea mjane wa marehemu huku wakimshutumu vikali Katunzi kwa kufanya jaribio la kumpeleka mahakamani mama Kulola kabla ya kufanyika kwa kikao cha ukoo na kuona nani anaweza kuwa msimamizi wa mirathi hiyo.
Mjane wa marehemu alipozungumza na gazeti hili alikuwa na haya ya kusema:
“Familia yangu ina mpasuko mkubwa, watoto wangu hawaelewani na Katunzi, nimepata mfadhaiko kuhusu mambo ya familia kuanza kuhusishwa na mahakama, watoto wangu siku hiyo walipomfukuza Katunzi nyumbani niliwagombeza sana kwani halikuwa jambo la kawaida.

“Kwa sasa mambo yote namwachia Mwenyezi Mungu, wote ni watoto wangu siwezi kuwabagua hata siku moja. Kinachosumbua hapa ni kila mmoja kuwa na tamaa ya mali za kidunia. Haya yote ni majaribu ya mwovu shetani.”
Jumatatu iliyopita, saa 2:56- 58 asubuhi, Mchungaji Katunzi hakupokea simu ya mwandishiili kujibu madai ya kuwa aliwahi kutimuliwa na baadhi ya watoto wa mzee Kulola kama chanzo chetu cha habari kilivyodadavua.

<GPL>