Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa
kikao cha kubadilishana uzoefu wa
kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya
kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano
wa wizara, Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto),
akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa
kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati
ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka
Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hicho
kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu
wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa
mitandao wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati
ya Tanzania na Urusi.Kushoto ni Kamishna
Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika
ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu
wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya
kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa
kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika
ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.
Kamishna
Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na
Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa
kikao cha kubadilishana uzoefu wa
kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment