Benny
Mwaipaja, MoFP
Dar
es salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (pichani), Ikulu, Jijini
Dar es salaam, baada ya kumteua kushika wadhifa huo jana.
Baada
ya kuapishwa, Katibu Mkuu huyo amekula kiapo kingine cha maadili mbele ya
Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Salome Kaganda, ambaye amemtaka kutekeleza
majukumu yake kwa uadilifu mkubwa ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya
kuwatumia wananchi katika sekta ya fedha na uchumi
Bw.
Doto James anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Servacius
Likwelile, ambaye Mhe. Rais Dkt. Magufuli, amesema atampangia kazi nyingine.
Doto
James, ambaye kitaaluma ni mchumi, alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha
na Mipango akishughulikia sera, atawaongoza manaibu makatibu wakuu wengine
watatu walioko katika Wizara ya Fedha na mipango.
No comments:
Post a Comment