Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
VIONGOZI
wa madereva waendesha bodaboda mkoa wa Dar es salaam wamewaasa
wanachama wao kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo
ya nchi kwa manufaa ya Watanzania wote.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti waendesha bodaboda kutoka Manispaa ya Kinondoni
mkoani Dar es salaam Almano Mdede wakati akizungumza na waandishi wa
habari jana jijini Dar es salaam kuhusu utendaji wao wa kazi za kila siku.
Viongozi
hao wamesema kuwa wanaimani na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika
uongozi wake kwa dhamira yake ya kuwatumikia Watanzania na kuwataka
madereva bodaboda wenzao kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya
kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma ya usafiri katika maeneo yao.
“Ninawaomba
wanachama wa chama cha maererva bodaboda mkoa wa Dar es salaam tutambue
kuwa sisi ni wafanyabiashara kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, tafadhali tumpe sekunde aweze kutekeleza
aliyoahidi kwa Watanzania” alisema Mdede.
Aidha,
Mdede alisema kuwa waendesha bodaboda hao ni wafanyabiashara kwa mujibu
wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni vema wafanye
biashara kulingana na leseni zao.
Naye
Mjumbe wa madereva wa bodaboda kutoka Kinondoni Oscar Waluye alisema
kuwa waendesha bodaboda ambao ni wanachama katika umoja wao ni wale
waliosajiliwa na kufanya biashara kwa kuzingatia leseni zao ambapo
utambulisho wao unatokana na namba zao za pikipiki ambazo zimesajiliwa
kwa “plate number” nyeupe na namba za usajili zimeandikwa kwa rangi
nyeusi.
Aidha,
madereva hao wamewaomba madereva bodaboda wenzao nchi nzima kupitia
viongozi wao kuendelea kushirikiana na Serikali ili kujiletea maendeleo
yao wenyewe na familia zao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment