Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Sunday, 28 February 2016
KAPOMBE MCHEZAJO BORA MWEZI JANUARI 2016
Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016.
Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016.
RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.
WALIMU DAR KUPANDA DALADALA BURE!!
Paul Makonda
Walimu wa shule za msingi na sekondari za serikali mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.
Hayo yamesemwa leo hii na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, alipozungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam kueleza jitihada alizozifanya katika kutafuta namna ya kuwasaidia walimu kuondokana na adha ya usafiri ambayo husababisha wengi wao ama kuchelewa vipindi au kukosa kabisa kufika katika maeneo yao ya kazi.
Saturday, 27 February 2016
MCHAPALO WA UZINDUZI WA INTANETI YA KASI ZAIDI YA TIGO 4G MKOANI KILIMANJARO WAFANA
NAPE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA MWANZA
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza Machi 27.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.
YANGA YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAITUNGUA CERCLE DE JOACHIM 2-0
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, leo wamefanikiwa kusonga mbele kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitandika klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga imefuzu raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 ugenini wiki mbili zilizopita.
Mshambuliaji hatari Mrundi Amisi Tambwe ndiye aliyeanza kuiandikia Yanga bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya tatu ya mchezo akiunganisha krosi ya Simon Msuva.
BEKI WA ZAMANI TAIFA STARS APONGEZA TAMASHA LA PASAKA
Alphonce Modest (kulia) akipokea msaada wa fedha kutoka kwa Alex Msama, Mkurugenzi wa Msama Promotions.
Na Mwandishi Wetu
VIJANA KUTOKA JKT KUPATA AJIRA DAR
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imejipanga kuajiri vijana waliopita Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kama mgambo ikiwa ni jitihada za Halmashauri hiyo kupambana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya kazi hiyo kwa baadhi ya mgambo kujihusisha na vitendo vya rushwa.
BASATA YAONYA WASANII DHIDI YA MATAPELI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawataka
wasanii wote kuwa makini na wakuzaji Sanaa (Mapromota) au baadhi ya wanaojiita
wadau wa Sanaa ambao wamekuwa wakitumia njia za kiulaghai na utapeli katika
kujipatia faida na manufaa kupitia mgongo wa Wasanii.
Baraza linatoa angalizo hili kufuatia kuwepo kwa
ongezeko la matukio ya baadhi ya watu wanaojiita wadau wa Sanaa ambao wamekuwa
wakiwadanganya wasanii na kuwalaghai kwa kuwaahidi fursa mbalimbali kama za
maonesho ya ndani na nje ya nchi ambazo hata hivyo zimekuwa zikiishia katika
kuwaletea wasanii matatizo kiuchumi na kijamii.
MAFANIKIO YA KIPINDI CHA RADIO CHA WALINDE WATOTO
TIGO YAFIKISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA 4G LITE MOSHI
CHAMA CHA BODABODA WILAYA YA NACHINGWEA CHATOA MIKOPO YA PIKIPIKI 62 KWA WANACHAMA WAKE
Mgeni rasmi bwana Wilson Nyamanga aliyekuja kumwakilisha mkuu wa wilaya ya Liwale mh,Ephraim Mmbaga.
STATEMENT BY HEAD OF UN MISSION IN TANZANIA ON THE OCCASION OF THE 50TH ANNIVERSARY OF UNDP
UN Resident Coordinator in Tanzania and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez.
Today marks the 50th Anniversary of the United Nations Development Programme (UNDP). Founded in 1966, UNDP now works in some 170 countries and territories to help eradicate poverty and reduce inequalities and exclusion.
MKALI WA NDONDI THOMAS MASHALI KUTAFUTIWA MBABE PASAKA
Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.
50 CENT REACHES OUT TO SON MARQUISE BUT IT DOESN’T GO WELL
Marquise is now 20 and the two have been estranged for quite some time. The personal issues between 50 and his ex-Shaniqua Tompkins have publically exacerbated that separation between father and son.
WAS DONALD TRUMP AUDITED 12 YEARS IN A ROW?
Republican presidential candidate, businessman Donald Trump
There's new heat on Donald Trump over a rather dry topic: his tax returns. Mitt Romney, who has been making the TV news rounds, claimed this week that he expects a "bombshell" in Trump's tax returns, if only the candidate would release them.
SDL KUMALIZIKA WIKIENDI HII
Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika makundi ya A, B, C & D katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila kundi likitoa timu moja ya juu itakayocheza fainali za kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Kesho Ijumaa, michezo mitatu ya kundi C itachezwa katika raundi hiyo ya mwisho, Villa Squad watacheza dhidi ya Mshikamano (Mabatini, Mlandizi), Abajalo Dar v Karikaoo FC (Karume) na Changanyikeni watakuwa wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA NIDA, AWATAKA KUONGEZA KASI UANDAAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji
Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi
ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza upande wa kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
MASHINDANO YA SHINDA NYUMBA, MSHINDI AKABIDHIWA PIKIPIKI
Afisa Masoko Msaidizi wa Global Publishers, David Mwaipaja (kushoto) akimkabidhi Lucy Swai ufunguo wa pikipiki aliyoshinda kwenye droo ya pili ya Shinda Nyumba, hafla imefanyika leo kwenye Ofisi za Kampuni ya Global Publishers, Bamaga Mwenge - Dar.
KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO YATOA MSAADA WA FEDHA ,KIASI CHA SHILINGI MIL TANO NA VIFAA VYA MICHEZO KWA WATOTO WA KITUO CHA AMANI CENTER CHA MJINI MOSHI
Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 afisa uhusiano wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Amani Center ,Kampuni ya Tigo imetoa kiasi hicho cha fedha pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya mbio za Kilimanjaro Marathoni.
BURIANI SAJINI KASSIM SAID MAPILI
Mzee Kassim Mapili wakati akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo November.
Kassim Mapili akipiga gitaa la solo kwenye jukwaa la bendi ya Mjomba Mrisho Mpoto.
Na Daniel Mbega
“KIFO oooh kifoo, kifooo kifoooo, kifo
hakina huruma!” Naam. Ndivyo alivyoimba marehemu Ramazan Mtoro Ongalla ‘Dk.
Remmy’ wakati akiwa na bendi yake ya Super Matimila ‘Wana Bongo Beats’
akiomboleza kuhusu ‘kifo’, Fikra Pevu
inaripoti.
Kweli
kifo hakina huruma, kwa sababu kinaweza kumchukua yule umpendaye katika wakati
ambao bado unamhitaji.
Katika
albamu yao ya Nippon Banzai ya mwaka 1994, Zaiko Langa Langa ‘Nkolo Mboka’
wanasema ‘Liwa yo Moyibi’, yaani ‘Wewe kifo ni mwizi’! Hakika kifo ni
mwizi kwa sababu kinatokea bila taarifa, hakipigi hodi, kinashambulia na
kuwaacha watu wakiwa na majonzi na mpendwa wao.
WAZIRI NAPE AAHIDI UPATIKANAJI WA SERA YA FILAMU NCHINI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwasili eneo la tukio kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo.
SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAPATA VIONGOZI WAPYA
Simon Mwakifwamba
Na Shamimu Nyaki-Maelezo.
Kufuatia uchaguzi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam wa kutafuta viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) viongozi wapya wamepatikana ambao ni Rais, Makamu wa Rais, pamoja na Wajumbe kumi wa Bodi watakaongoza Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne.
BASATA YAMLILIA KASSIM MAPILI
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha
Msanii Mkongwe wa muziki wa dansi Kassim Mapili kilichotokea katikati ya wiki
hii nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.
Kassim
Mapili ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa
na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga
angavu kwenye sekta ya Sanaa.
DAWASCO YANASA NYUMBA TANO KWA WIZI WA MAJI TABATA
Na Mwandishi Wetu
Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es
Salaam (Dawasco), imenasa wizi mkubwa wa Maji katika nyumba tano ambazo
zimeunganishiwa huduma ya majisafi kinyume cha utaratibu maeneo ya Tabata
Magengeni, nyumba hizo zinamilikiwa na mfanyabiashara mmoja ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja, nyumba hizo zimepangishwa kwa familia tano tofauti
(Apartments).
MWANAHABARI SULEIMAN MSUYA WA GAZETI LA JAMBO LEO AACHANA NA UKAPERA
Mwanahabari Suleiman Msuya wa Gazeti la Jambo Leo akitafakari jinsi atakavyoyaanza maisha ya ndoa baada ya kufunga ndoa na Shamim Rabim nyumbani kwa bibi harusi Jet Lumo jijini Dar es Salaam jana mchana.
YANGA KATIKA MTIHANI WA AFRIKA, APR, GOR MAHIA NA MAFUNZO KAZI NGUMU
Na Daniel Mbega
WAKATI
ambapo Yanga ya Tanzania na Vital’O ya Burundi zinacheza nyumbani Jumamosi hii
Februari 27, 2016 zikihitaji sare tu kutokana na ushindi katika mechi zao za
kwanza za Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu za APR ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya
na Mafunzo ya Zanzibar ziko katika wakati mgumu.
Gor Mahia
ilikubali kipigo cha nyumbani Nairobi cha mabao 2-1 kutoka kwa CNaPS Sports ya
Madagascar katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali, na sasa inahitaji miujiza
ili isonge mbele wakati zitakaporudiana mjini Antananarivo.
Mafunzo
yenyewe ina wakati mgumu Zaidi wa kuvuka mbele ya AS Vita Club baada ya kipigo
cha mabao 3-0 mjini Unguja na kuwang’oa wakongwe hao wa soka Afrika ni sawa na
kupanda mlima Kilimanjaro wakikimbia.
Tuesday, 23 February 2016
KITWANGA AAGIZA MABADILIKO MAKUBWA IDARA YA UHAMIAJI
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji
Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini (kushoto) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa
kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa
kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KINDONDONI YAPANGA KUNUNUA MAGARI 40 YA KUKUSANYA TAKA NGUMU.
Na
Nyakongo Manyama
MAELEZO
Dar
es Salaam
23.02.2016
HALMASHAURI Wilaya ya Kinondoni
Jijini Dar es Salaam katika mwaka kipindi cha 2016/17 imepanga kununua magari
40 yatakayotumika kwa ajili ya zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu katika Kata na
Mitaa ya Halmashauri hiyo.
TFF, KTA ZAZINDUA PROGRAMU YA MAENDELEO YA SOKA KWA WANAWAKE
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine (katikati), na mratibu wa KTA, Mia Mjengwa (kulia)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Taasisi binafasi ya Karibu Tanzania Association (KTA) kwa pamoja wamezindua programu ya maendeleo ya soka kwa wanawake vijana ili kuhamasisha usawa wa kijinsia, uwezeshaji kijamii na kiuchumi kwa wanawake nchini itakayofadhiliwa na Shirika la Forum Syd kutoka nchini Sweden.
HUDUMA YA MAJISAFI YAREJEA JIJINI DAR
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Dar es salaam
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imerejesha huduma ya upatikanaji wa Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 36 kuanzia siku ya Alhamisi 18/02/201.
HAFLA YA PSPF YAFANA
Afisa Mauzo na Masoko kutoka PSPF Bw. Ismail Omary kulia akimpa maelekezo ya
juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo mgeni rasmi Yeremia Mbaghi
kutoka TRA ikiwa ni pamoja na huduma ya uchangiaji wa hiari kwa
wajasiriamali.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Benjamin Sawe-WHUSM).
WAKULIMA WILAYANI RORYA MKOANI MARA WAPATIWA MAFUNZO YA KUPATA HUDUMA ZA UGANI KWA NJIA YA SIMU
Mtafiti Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk. Emmarold Mneney.
MFANYABIASHARA WA MCHELE ASHINDA SAFARI YA STARTIMES KWENDA UJERUMANI
Mshindi wa droo ya pili wa promosheni ya Pasua Anga na StarTimes, Bw. Johannes Maluli (kulia), akibonyeza kitufe cha kuchezesha droo ya kumpata mshindi wa tatu wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga. Wakishuhudia katikati ni Balozi wa kampuni hiyo kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda na Meneja Uhusiano wa Umma, Bw. Muddy Kimwery (kushoto).
WANAHABARI, WATAFITI KUTOKA COSTECH WAZURU KABURI LA BABA WA TAIFA BUTIAMA MKOANI MARA
Wanahabari na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliokuwa katika ziara ya kuzungumza na wakulima wa mkoa wa Mwanza kuhusu changamoto za kulimo zinazo wakabili pamoja na matumizi ya bioteknolojia katika kilimo wakiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walipozuru kaburi hilo hivi karibuni Kijiji cha Mwitongo Butiama mkoani Mara.
Monday, 22 February 2016
CCM YAIPONGEZA NRA KUSHINDA UGANDA
PRESS
RELEASE
CONGRATULATORY
MESSAGE OF CHAMA CHA MAPINDUZI TO THE NATIONAL RESISTANCE MOVEMENT OF UGANDA
Chama cha Mapinduzi has received with great joy results of the
just-concluded general elections in Uganda. As a sister country we have been
following the entire process with keen interest and were confident that the
National Resistance Movement, under the leadership of Chairman Yoweri Kaguta
Museveni, would emerge triumphant. It therefore gives us great pleasure to
congratulate President-elect Museveni and our brothers and sisters of the NRM
on this resounding victory.
HILI NALO NI JIPU LASUBIRIWA KUTUMBULIWA: TANESCO YAPUUZIA WITO WA WANANCHI KUHUSU NGUZO HATARISHI
Wananchi wa Eneo la Tegeta Nyuki Jijini Dar es Salaam wamelilalamikia Shirika la TANESCO kushindwa kutatua Kero ya Nguzo ambayo inahatarisha Maisha ya wakazi Hao katika eneo hilo kwa zaidi ya Miaka 8 hivi sasa, nguzo hiyo imesogelea Kibanda cha Biashara na kusababisha hali ya Sinto fahamu kufuatia usalama wao.
WAZIRI KITWANGA AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WAKUU WA JESHI LA POLISI NA WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji
Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi
hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na wakwanza upande wa kushoto
ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Subscribe to:
Posts (Atom)