Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 February 2016

GOODLUCK GOSBERT KUZINDUA ALBAMU TAMASHA LA PASAKA


Na Mwandishi Wetu
MUIMBAJI nguli wa muziki wa Injili jijini Mwanza, Goodluck Gosbert anatarajia kuzindua albamu yake ya Ip[o siku yenye nyimbo nane kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama  tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita kwenye ukumbvi wa Desire kabla ya kumalizia uwanja wa Taifa Wilayani Kahama ambalo litafanyika Machi 28.
Msama alisema albamu hiyo ni moto wa kuotea mbali, hivyo wakazi wa mikao ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo litashi8rikisha waimbajki mbalimbali wa Tanzania.
Msama alizitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Ipo siku, Acha waambiane, Haohao, Nisamehe, Pendo langu, Ndiwe Mungu, Moyo tulia na Surprise.
Aidha Msama alitumia fursa hiyo kueleza kwamba viingilio katika tamashja hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000.
"Tamasha la Pasaka ni sehemu ya kusaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na walemavu, yatima na wajane ambao wanahitaji msaada kutoka kwa wadau kama kampuni ya Msama Promotions," alisema Msama.
Msama aliwataja waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Jennifer Mgendi, Sifael Mwabuka, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Christopher Mwahangila, Anastazia Mukabwa, Kwaya ya AIC Makongoro, Kwaya ya Wakorintho wapili, Faustine Munishi, Solomon Mukubwa.

No comments:

Post a Comment