Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 February 2016

BEKI WA ZAMANI TAIFA STARS APONGEZA TAMASHA LA PASAKA

Alphonce Modest (kulia) akipokea msaada wa fedha kutoka kwa Alex Msama, Mkurugenzi wa Msama Promotions.

Na Mwandishi Wetu
Akizungumza jana, Modest alisema Msama kupitia Tamasha la Pasaka anatenda kazi ya Mungu kwa sababu alikua na uwezo wa kuendelea na shughuli zake nyingine lakini anamkumbuka Mungu kwa kukusanya makundi ya waumini ambao wanamtaja Mungu kwa pamoja.
Modest alitumia fursa hiyo kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa linakofanyika Tamasha la Pasaka mwaka huu kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa pamoja."Unajua wanapokusanyika idadi kubwa ya watu, tambua na Mungu pia yupo, hivyo Msama mara nyingi anatenda kazi ya Mungu, hivyo na wengine tumuunge mkono katika hilo," alisema Modest na kuongeza.
"Nampongeza sana Msama kwa utekelezaji wake wa Tamasha la Pasaka, kwani ni wachache wenye moyo kama wake, kwani alikua na uwezo wa kuendelea kula bata kwa kidogo alichonacho, lakini muono wake ni kuwa karibu na Mungu mara kwa mara," alisema Modest.
Naye Msama alitumia fursa hiyo kueleza kwamba tamasha la mwaka huu linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita, Machi 27 jijini Mwanza na kumalizia Kahama Machi 28.
Msama alisema waimbaji mbalimbali wanatarajia kupanda jukwaani kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

No comments:

Post a Comment