Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 17 November 2013

USIOMBE HAYA YATOKEE, MAITI 400 ZAZIKWA MITARONI


Grim spectacle: Hundreds of bodies lay rotting in a hastily-constructed trench
Karibu maiti 400 zilizoanza kuharibika nchini Ufilipino zimezikwa kwenye mtaro huku maiti 393 zikiwa hazijatambuliwa.

SEMA, ANAWEZA AU HAWEZI?

Sema mwenyewe, anaweza hawezi? Kama anaweza mfagilie, mpe uwezo, mwezeshe...

MAKABURI YA MACHIFU YANA MAMBO

Naam, kila sehemu kuna mambo yake, lakini hakuna kazi ngumu kama kuzuru makaburi ya machifu, inahitaji moyo. Hili ni kaburi la Mtwa Munyigumba Kilonge Mwamuyinga lililopo katika Kijiji cha Rungemba. 
Nilipofika hapa kwa mara ya kwanza mwili ulinisisimka mno, nikaogopa lakini nikaona fahari kubwa kwamba walau katika maisha yangu nimeweza kufika katika kaburi la Chifu Mkuu wa Wahehe, ambaye nilikuwa namsoma tu kwenye vitabu vya historia enzi hizo nikijua ni simulizi kama zilivyo nyingine. 
Kusema kwamba ipo siku ningeweza kufika hapa, au kuota kwamba kuna mahali hao mashujaa tunaweza kuona kumbukumbu zao, sikuwahi kutegemea. Hii ilikuwa miongoni mwa matukio ya kukumbukwa katika maisha yangu.
Naam, hapa pawekwe Makumbusho ya Taifa kwa sababu panaweza kusaidia kudumisha historia hii muhimu kwa vizazi vyetu. Bado naendelea na utafiti wangu.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa


Saturday, 16 November 2013

NYAYO ZA CHIFU MKWAWA (1)

Kaburi la Munyigumba lililopo Rungemba, Mufindi.
Daniel Mbega

UKITAJA mashujaa wa Afrika, lazima pia umtaje kiongozi mkuu wa Wahehe, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Kilonge Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa. Huyu ana mambo mengi aliyoyafanya, ya kujivunia, ambayo kizazi hiki hakifundishwi tena shuleni na hivyo historia yake inapotea.
Nitajaribu kueleza kwa ufupi ufupi tu kile ambacho nimekipata katika utafiti wangu wa historia mjini Iringa, lakini kwa vile bado ninaendelea na utafiti huo, nakaribisha taarifa zozote kuhusiana na kiongozi huyo shujaa.

AMCHOMA VISU MUMEWE, KISA HAKUMPIGIA SIMU!

MWANAMKE mmoja mwenye miaka 21 alimchoma visu mchumba wake kwa sababu alishindwa kumpigia simu kila baada ya saa mbili wakati alipokwenda kujirusha, akamuacha na majeraha makubwa ambayo madaktari walihisi amekufa, mahakama ya Uingereza iliambiwa wiki hii.

Friday, 15 November 2013

MUUAJI NA MBAKAJI ANYONGWA BAADA YA KULA PIZZA NA KUKU


MFUNGWA katika gereza la Florida, ambaye alihukumiwa kunyongwa kwa makosa ya ubakaji na mauaji ya msanii mwaka 1991, ameuawa Jumatatu jioni.

BIBI KIZEE ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA ROONEY AZUA MAMBO


Wayne Rooney (26)

MHUDUMU wa mapokezi katika jumba la upunaji (massage parlour) anayedaiwa kufanya mapenzi na Wayne Rooney alimwambia mwanandinga huyo aondoke mara moja 'kabla hajachafuliwa na soka yake kwisha', mahakama ya Old Bailey ilielezwa Jumatatu.

Tuesday, 12 November 2013

DK. MVUNGI AFARIKI DUNIA

Habari zilizoifikia blog hii hivi punde ni kwamba, Dk Sengondo Mvungi amefariki dunia nchini Afrika Kusini alikokwenda kutibiwa kufuatia kuvamiwa na watu wanaosadikiwa majambazi ambao walimkatakata mapanga.
Dk Mvungi, ambaye alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mkurugenzi wa Katiba wa Chama cha NCCR Mageuzi, amefariki kufuatia majeraha makubwa aliyoyapata pamoja na kuvilia damu kwenye ubongo.
Tutawaeletea taarifa baadaye.

SASA MNAOGOPA NINI SASA?

Walipewa madaraka, wakayatumia vibaya, walipewa madaraka, wakalala usingizi...Tembo wanateketea...

Eh, wabunge nao wameipiga 'STOP' Operesheni ya Kupambana na Ujangili... wanaogopa nini? au kwa vile nao wamo waliotajwa? Tuwaulize na watujibu...

Monday, 11 November 2013

CHADEMA KWANI NANI MCHAWI, NANI MWANGA?



RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE
CHADEMA
UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.
UTANGULIZI:Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.
Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe.

UJUZI HAUZEEKI BWANA!

Mama wa kijiji anatofautiana kwa mbali na wale wa mjini. Kila wakati anataka kujishughulisha, bila kujali umri. Na ususi ni sehemu ya kazi zinazofanywa wakati wa mapumziko.

TISA WAKAMATWA KUHUSIANA NA KUSHAMBULIWA DK SENGONDO MVUNGI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova.

RAIS KIKWETE, AKINA KAGAME WANAKUONEA GERE WEWE KUAMBATANA NA OBAMA

Rais Kikwete (kulia) akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana nchini Afrika Kusini.

Mheshimiwa Rais,
Nimesikiliza hotuba yako Bungeni kuhusu msimamo wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ilikuwa nzuri na uliondoa shaka iliyokuwa imetanda miongoni mwa Watanzania na hata wale waliodhani pengine utawakashfu ama kuwalalamikia marais wenzako ndani ya EAC ambao wanakutenga.

Friday, 8 November 2013

SITA MBARONI KUCHARANGWA MAPANGA DK. MVUNGI

Dk. Sengondo Mvungi akiwa taabani hospitalini

Na Waandishi Wetu
5th November 2013
Jeshi  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumvamia na kumjeruhi kwa mapanga Mjumbe wa  Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi.

BOSI WA TBS KIZIMBANI KWA UFISADI

Aliyekuwa  Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege, jana alifikishwa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la ada ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia shirika hilo hasara ya Dola 42,543 za Marekani (Sh. 68,068,800).

NI MAAFA MVOMERO


Watu  sita wameuawa, 36 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Bwagala na 30 wanashikiliwa kufuatia mapigano na mauaji baina ya wakulima na wafugaji zilizotokea katika eneo la Hembeti wilaya Mvomero mkoani hapa huku maganda ya risasi yameokotwa katika eneo la tukio.

KIBANDA AFUNGUKA KUTESWA KWAKE

Absalom Kibanda akiwa hospitalini na mkewe Angela Semaya

Na Waandishi Wetu8 Novemba 2013
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Cooperation (2006) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda amezungumzia tukio la kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa kwake lililotokea Machi mwaka huu.

KING LOWASSA: VIJANA WATATUNG'OA MADARAKANI

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

Na Muhibu Said5 Novemba 2013
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametahadharisha kuwa kama tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana halitapatiwa ufumbuzi, itakuwa chanzo cha serikali kupoteza madaraka.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014/2015, uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.

KAMA AMINA CHIFUPA VILE, ESTER BULAYA NAYE ATIKISA NCHI!

Ester Bulaya akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Na Muhibu Said5 Novemba 2013
Mbunge  wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya, amewasilisha bungeni maelezo binafsi akiitaka serikali pamoja na mambo mengine, kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za kulevya na kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia wahalifu wa dawa hizo.

JK ATEMA MOTO - HATUTOKI AFRIKA MASHARIKI

Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Irene Mark
RAIS Jakaya Kikwete amesema Tanzania haina mpango wa kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), itaendelea kuwepo licha ya kutengwa na baadhi ya nchi wanachama.