Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 30 September 2016

SERENGETI WAJIFUA ILI ‘KUIZIKA’ CONGO JUMAPILI

CONGO TUTAWAZIKA HAPA...
Ndivyo anavyoonekana kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.

BRITISH COUNCIL WAZINDUA UTAFITI WA SAUTI ZA VIJANA JIJINI ARUSHA


Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza  la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini,kulia ni Meneja Mradi wa British Council Tanzania,Elizabeth Nkanda.

TAASISI YA ADLG YABAINISHA SABABU ZA KUWEPO MAENDELEO DUNI KWENYE BAADHI YA VIJIJI VYENYE WAWEKEZAJI WA MADINI NCHINI.

Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, imebainisha kwamba kukosekana kwa uwajibikaji miongoni mwa baadhi ya viongozi, kunasababisha maendeleo duni kwenye baadhi ya maeneo/vijiji yenye wawekezaji ikiwemo migodi.

WAREMBO 30 MISS TANZANIA WATINGA KAMBINI LEO, WAPEWA SOMO LA AWALI NA MISS TANZANIA WA SASA

Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKABIDHIWA RIPOTI YA UKAGUZI WA MANUNUZI YA UMMA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akikabidhiwa Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga. Makabidhiano yaliyofanyika Wizarani jijini Dar es Salaam, Septemba 30, 2016.

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo Septemba 30, 2016 kwa mchezo mmoja tu, unaozikutanisha timu za Toto Africans na Ndanda ya Mtwara katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA BARABARA YA JUU KUKAMILIKA KWA WAKATI


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale(Wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya ramani ya Ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover) kwa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa( Wa kwanza kushoto) wakati alipokagua ujenzi  huo Jijini Dar es salaam.

BASATA YAMPONGEZA MUSTAFA HASANNALI KWA KUSHINDA TUZO YA UBUNIFU WA MAVAZI

                                                           National Arts Council BASATA
 Tarehe: 30/09/2016
  
BASATA Arts Centre                                                             
Tel. 2863748/2860485
 Fax: 0255- (022) – 286 0486                                                                                                                         
Ilala Sharif Shamba                                                                                                                                                                       
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail:basata06@yahoo.com

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa nchini linapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza msanii na mbunifu wa Mavazi Mustafa Hassanali kwa kushiriki kinyanga’anyiro cha Tuzo ya Mavazi ya Afrika Mashariki Kenya 2016 (Kenya Fashion Awards 2016) yaliyofanyika tarehe 03/09/2016 na kupata tuzo ya Mbunifu Bora wa Mwaka wa Afrika Mashariki.

MASHINDANO YA TIGO IGOMBE MARATHON KUFANYIKA JUMAPILI HII

Meneja  Mauzo wa Tigo mkoani Tabora, Bright Kisanga(kushoto) akiongea na wanahabari jana wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Igombe marathon yatayofanyika jumapili mkoani Tabora. Wengine ni Amon Mkoga Mratibu wa mashindano na katibu wa chama cha riadhaa mkoani Tabora, SalumTaradadi. Kampuni ya Tigo ndio mdhamini mkuu wa mashindano hayo.

SERENGETI YAJIFUA KINOMANOMA KUIABILI CONGO KESHO



Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakijifua kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).

DC MWILAPWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MAJI KUHUSU MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA


Mkuu wa wilaya ya Tangaa,Thobias Mwilapwa akifungua mkutano wa akifungua mkutano wa wadau kuhusu mkataba wa huduma kwa mteja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) uliofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na kulia ni Afisa Tarafa ,Suleiman Zumo anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji, Haika Ndalama.

Thursday, 29 September 2016

ZIMWI LA TEGETA ESCROW LAMTISHA PROFESA TIBAIJUKA, AKATAA KUPOKEA DOLA 300,000 BAADA YA KUPEWA TUZO YA KIMATAIFA

 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.

MRADI WA URASIMISHAJI ARDHI UBUNGO WAINGIA MIZENGWE, WATENDAJI WATISHIA KUGOMA KWA KUKOSA POSHO

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi



Na Dotto Mwaibale
WATENDAJI na vibarua wanaofanya kazi ya kupima ardhi katika mradi wa urasimishaji wa ardhi katika maeneo yaliyojengwa kiholela katika Kata ya Kimara wilayani Ubungo umeingia mdudu baada ya kutishia kugoma kutokana na kutolipwa fedha za posho ya kazi hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu.

KAULI NZITO YA MAKOCHA SERENGETI BOYS

Makocha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania ‘Serengeti Boys’, Bakari Nyundo Shime na Muharami Mohammed anayewanoa makipa watatu wa timu hii, wamesema kwa pamoja: “Tuko tayari kwa vita.”

TAIFA STARS WATAKAOIVAA ETHIOPIA HAWA HAPA

Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa (pichani) ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.

MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA KURINDIMA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI MWANZA


Kanisa la EAGT Posta “B” Mabatini Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Lameck Nkumba, linawakaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika katika viwanja vya kanisa hilo vinavyotizamana na geti la polisi Mabatini nyuma ya iliyokuwa Orange Tree Hotel.

TIGO YAWAKUMBUKA WAHANGA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA KWA KUTOA SARUJI MIFUKO 2424



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu (kushoto) akipokea sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya, kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

SERIKALI YATOA RAMBIRAMBI KWA WAFIWA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiongea na wawakilishi wa familia waliopoteza ndugu zao (hawapo pichani) kwa tetemeko la ardhi lililotokea mapema Septemba 10 mwaka huu Bukoba mjini wakati wa kukabidhiwa rambirambi iliyotolewa na Serikali milioni 17 pamoja na kampuni ya simu ya Halotel ambayo imetoa shilingi milioni 15. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa.

VIJANA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUONDOKANA NA UMASKINI



Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa kupata maendeleo.

Wednesday, 28 September 2016

MAFAHARI WAWILI KWELI HAWAKAI ZIZI MOJA! WASHIRIKI KUTOKA RWANDA NA BURUNDI WATWANGANA NDANI YA KIJIJI CHA MAISHA PLUS






Katika hali isiyotarajiwa katika kijiji cha Maisha Plus, jana washiriki wawili, KAREKEZI Jean kutoka Rwanda na BASWARI Nibigira kutoka Burundi walipigana hadharani huku wakirekodiwa na camera zilizofungwa kijijini hapo. 

SERENGETI BOYS WATUA CONGO LEO

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville.  Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini hapa. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI NDEGE MBILI MPYA ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KWA AJILI YA ATCL JIJINI DAR LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya utakaofanyika kuanzia Septemba 30 hadi   Octoba 2 mwaka huu.

SSRA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.

TAARIFA YA KATIBU MKUU JUU YA UPATIKANAJI WA DAWA


SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LINALOENDESHWA NA OXFAM LAZINDULIWA RASMI MONDULI MKOANI ARUSHA MSHINDI KUONDOKA NA TSH 25,000,000

Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania limezinduliwa Rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan Kamanta aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo na kuoneshwa  na ITV kila siku (kuanzia 27/09/2016 - 17/10/2016) saa 12.30 jioni, Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Enguiki, wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mwakilishi wa DED, DAS, wazee wa kimila, wenyeji wa kijiji cha Enguiki, wafanyakazi wa shirika la Oxfam.

MKURUGENZI WA IDARA YA USALAMA NA MAZINGIRA, WIZARA YA UCHUKUZI AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA BAHARI DUNIANI


 Kulia ni Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani  ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande kushoto ambaye alimuwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Makame Mbawara katika maashimidho hayo akiingia kwenye viwanja vya Tangamano kunakofanyika maadhimisho hayo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra,Gilliard Ngewe  kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras)Mhandisi Zena Saidi.

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUJIAJIRI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo akifungua warsha ya kutengeneza mkakati mmoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa NACTE jijini Dar es Saalam. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za serikali.

Tuesday, 27 September 2016

MASAUNI AWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA VITUO VYA WATOTO YATIMA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi fedha taslimu Shilingi 1,119,000, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya kusaidia majukumu mbalimbali ya ulezi wa watoto hao. Fedha hizo zilitolewa na Masauni pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo kwa lengo la kusaidia kituo hicho. Pia Baraza hilo lilitoa mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BURUNDI YAWAFUTA MACHOZI WANAKAGERA KWA TANI 183 ZA VYAKULA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, MJINI GEITA LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika leo katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

UWT WATOA MIFUKO 200 YA SARUJI KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea moja ya mfuko wa saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT-CCM) Sophia Simba ukiwa ni miongoni mwa mifuko 200 sa saruji iliyotolewa na UWT kusaidia maafa Kagera.

NHC YAKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA TOFALI KWA VIJANA BUKOBA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kushoto) akimkabidhi tofali Afisa Miradi wa Kikundi cha vijana cha Tuinuane cha Bukoba Mjini Christopher Vincent wakati wa makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali iliyotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yenye ubora unaofaa kujengea katika mazingira ya Bukoba kulingana na asili ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera.

DC KONGWA AMTUMBUA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa kikao cha Kumng'oa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na salama wilayani humo.

MAONYESHO YA FILAMU ZA BEIJING 2016 CHACHU KWA UKUAJI WA SANAA NCHINI

 Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.

LHRC WASHEREHEKEA MIAKA 21 NA WATOTO WANAOISHI MAKAO YA TAIFA YA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu kuanzishwa kwake.

TAMWA YATAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUTOA FURSA YA WANAWAKE KUSIKIKA

Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu, wakiwa kwenye semina iliyofanyika Jumamosi wiki iliyopita Septemba 23, 2016 Jijini Dar es salaam. 

MKURUGENZI WA ILEJE HAJI MNASI ATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO



 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotembele hivi karibu na kujifunza mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya hayati baba wa taifa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi nzima.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari

SUMATRA KUPAMBANA NA WACHAFUZI WA MAZINGIRA YA BAHARI


 Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini  (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo  kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud.

'PANYA ROAD' WAIBUKA UPYA NA KUTESA WANANCHI MOSHI BAA JIJINI DAR ES SALAAM

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar. Simon Sirro


Na Dotto Mwaibale

KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.

WANANCHI WAILALAMIKIA TAZARA KWA KUFUNGA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.

TIGO FIESTA YAITIKISA MKOA WA KILIMANJARO

Wasanii Barnaba na Nandy wakitoa burudani pamoja kwenye tamasha la Tigo Fiesta kwenye uwanja wa Majengo,Moshi mkoani Kilimanjaro usiku wa kuamkia jana.

WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.

WAFANYABIASHARA KARIAKOO WACHANGA SH. MILIONI 60.7 KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA


 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, akizungumza jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea michango ya fedha na vifaa kutoka kwa wanachama wa jumuia hiyo kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.  Jumla walichanga fedha na vifaa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 60.7. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

ERICK MASHAURI AELEZEA JINSI VAT INAVYOATHIRI BIASHARA UTALII, AIOMBA SERIKALI KUPITIA TENA ONGEZEKO HILO


Kufuatia serikali kupitisha muswada wa ongezeko la VAT kwa watalii ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali, MO Blog imepata nafasi ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri ili kujua ni kwa kiasi gani ongezeko hilo limeathiri biashara kwa makampuni yanayopeleka watalii mbugani na kwa sekta ya utalii kwa ujumla.

Sunday, 25 September 2016

TASWIRA; KISHINDO CHA TIGO FIESTA KILIVYOFIKIA JIJI LA TANGA IJUMAA HI

Roma Mkatolili akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta katika Tamasha hilo liliofanyika katika viwanja vya  Mkwakwani Jijini Tanga usiku wa Ijumaa .