Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 28 November 2013

SIYO MZEE MTEI, HATA MWALIMU NYERERE ‘ALIICHAGULIA’ CCM VIONGOZI



Na Daniel Mbega

NIMEKUWA nikifuatilia mijadala inayoendelea ya siasa ndani ya Chadema, lakini kubwa zaidi lililonifanya niandike waraka huu mfupi ni madai kwamba muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, anawachagulia viongozi.

ZITTO KABWE 'AMEFUNANIWA' KWEUPE

 Dk. Kitila Mkumbo na Zitto Kabwe


Na Daniel Mbega

NI kweli, ‘amefumaniwa’ kweupe safari hii. Ndiyo lugha pekee ambayo tunaweza kuitumia tunapolizungumzia suala la Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zuberi Zitto Kabwe, ambaye kwa sasa amevuliwa nyadhifa zote ndani ya Chama na hata Bungeni.
Uamuzi uliochukuliwa na Kamati Kuu ya Chadema dhidi ya Zitto Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo (schoolmate wangu pale Pugu sekondari mwanzoni mwa miaka ile ya 1990) unaonekana kuwashangaza wengi, lakini kimsingi, pamoja na utetezi alioutoa yeye mwenyewe binafsi, au ule uliotolewa na Dk. Kitila, bado hawezi kukwepa lawama za ‘uhaini’ kama zilivyoitwa na viongozi wa Chadema.

DK NCHIMBI ATOA ZAWADI KWA WAHITIMU WALIOFANYA VIZURI CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti mwanafunzi Nuru Ally aliyefanya vizuri kuliko wanafunzi wote katika somo la Development Studies katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilichopo mjini Morogoro. Mwanafunzi huyo pia alikabidhiwa zawadi ya Shilingi 50,000. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma SUA, Profesa Peter Gillah. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WASHINDI WA DROO NDOGO YA CHAMPIONI 'SHINDA MAHELA' WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO


Clement Michael (kulia) ambaye ni mkazi wa Mbagala-Zakhem, Dar, akikabidhiwa Sofa Set yake na Mr Championi.

NYAYO ZA CHIFU MKWAWA (6)

Na Daniel Mbega

Ndugu zangu,
Kwanza kabisa niwieni radhi kwa kushindwa kuendelea na simulizi yetu ya kufutilia Nyayo za Chifu Mkwawa kwa siku kadhaa. Hii imetokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu.
Hata hivyo, karibuni tuendelee na simulizi yetu.

Wednesday, 20 November 2013

HIKI KINAKUJA, KAENI MKAO WA KULA

Jiandae kukisoma...

NYAYO ZA CHIFU MKWAWA (5)

Askari wa Kijerumani

Na Daniel Mbega

Ndugu zangu,
Tunaendelea na simulizi ya historia ya kufuatilia ‘Nyayo za Chifu Mkwawa’. Baada ya kufanikiwa kuurejesha utawala kwenye himaya yake mwaka 1890 kufuatia kumtwanga Mwambambe Mwalunyungu aliyekuwa na walugaluga kutoka Tabora, Chifu Mkwawa aliendelea kuuimarisha utawala huo kwa ujasiri mkubwa akiwazuia Wamasai wasiende kusini pamoja na kupambana pia na biashara ya utumwa iliyokuwa ikiendeshwa na Waarabu.

DK. NCHIMBI AKUTANA NA VIONGOZI WA SHIRIKA LA MISAADA LA HANNS SEIDEL FOUNDATION


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada la Hanns Seidel Foundation masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na shirika hilo. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Dk. Peter Witterauf, anayefuata ni Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert, na Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo nchini Tanzania, Konrad Teichert. Viongozi wa Shirika hilo lenye Makao Makuu yake jijini Munich nchini Ujerumani walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Tuesday, 19 November 2013

NYAYO ZA CHIFU MKWAWA (4)

Mti wenye miaka zaidi ya 100 katika eneo la Lundamatwe ambapo mganga wa jadi Ngondo Kimamula aliwatengenezea dawa wapiganaji wa Mkwawa kabla ya kumpiga Mwamubambe Mwalunyungu.
Eneo ambalo inaelezwa kwamba ndiko vichwa vta wapiganaji wa Mwambambe vililundikwa baada ya kuuawa na wapiganaji wa Chifu Mkwawa.
Makaburi ya ukoo wa Ngondo Kimamula Mbugi katika eneo la Lundamatwe.

Na Daniel Mbega

Ndugu zangu,
Tunaendelea na simulizi ya historia ya kufuatilia ‘Nyayo za Chifu Mkwawa’. Tumeona jinsi ambavyo baada ya kifo cha Chifu Munyigumba mkwewe Mwambambe Mwalunyungu alivyomuua baba yake mdogo Chifu Mkwawa, Mtwa Mhalwike na yeye akajitangazia mtawala wa himaya ya Wahehe, ingawa wakati huo walikuwa bado hawajaanza kuitwa ‘Wahehe’.

Monday, 18 November 2013

SIRI 100 USIZOZIJUA KATIKA MAPENZI

Ndugu zangu,
Wasomaji wangu wengi hawakukipata kitabu changu hiki kilipotoka kwa mara ya kwanza mwaka 2005. Kwa hiyo, wengi wao wamekuwa wakiniomba nikichape tena. Hata wale waliobahatika kukipata wamepoteza nakala zao kwa sababu kila waliyemwazima asome, alitoweka nacho.
Sasa basi, naomba mnisaidie jambo moja, yeyote anayekihitaji, au kama kuna rafiki yake, ndugu yake, jamaa yake anakihitaji, basi naomba anijulishe kupitia barua-pepe brotherdanny5@gmail.com.
Lengo ni kutaka kujua mahitaji ni makubwa kiasi gani ili nikakichape tena.
Nitashukuru kwa ushirikiano wenu.

Ndugu yenu,
Brother Danny

UNATAKA KWENDA MBINGUNI?

Mchungaji Chavalla alikwenda kwenye baa moja mjini Iringa na kumwendea jamaa wa kwanza aliyemuona akigida pombe. "Unataka kwenda mbinguni?" akamuuliza jamaa huyo, ambaye naye alijibu, "Ndiyo, Baba Mchungaji, nataka kwenda."

NYAYO ZA CHIFU MKWAWA (3)

Eneo la makaburi alimozikwa Chifu Munyigumba na baadhi ya wanafamilia ambalo limezungushiwa uzio. Hapa panahitajika kuwa sehemu ya Makumbusho ya Taifa, ni urithi wetu - Mali Kale.

Na Daniel Mbega

Utawala wa Munyigumba Kilonge Mwamuyinga ulidumu kwa muda wa miaka 19 tangu alipomuua kaka yake Ngawonalupembe mwaka 1860.

NCHIMBI ATEUA BODI YA SHIRIKA LA UZALISHAJI POLISI

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Simu:  +255-22-2112035/40
          S.L.P.  9223
Nukushi:  +255-2122617/2120486
Barua Pepe:  ps@moha.go.tz
       Dar es Salaam


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana na Maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi kumekuwepo na mikakati mbalimbali  inayolenga uboreshaji wa miundombinu yake, ikiwa ni pamoja na kupata ofisi, vituo vya polisi, makazi ya kuishi askari makambini, vifaa na vitendea kazi ili kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

SHETANI AINGIA KANISANI

Jumapili moja asubuhi, shetani aliingia kwenye kanisa moja katika mji fulani. Kila muumini aliyekuwepo ibadani, pamoja na mchungaji na wainjilisti, wakaanza kugombea mlango wa kutokea, wakipigana vikumbo kunusuru maisha yao.

Sunday, 17 November 2013

GOGO LA SAMORA MACHEL NA MONDLANE


Ndugu zangu,
Kimsingi napenda sana historia, niliipenda tangu nikiwa mtoto, tangu wakati nilipokuwa nasimuliwa hadithi. Tabia ya kupenda kujikumbusha mambo ya zamani ninayo na nitaendelea nayo, ndiyo maana nafanya utafiti wa historia, japokuwa sijasomea historia.

VIPAJI HIVI, NANI WA KUVIENDELEZA?

Watoto wanaweza kufikia malengo na ndoto zao ikiwa wazazi wataamua kutambua vipaji vyao. Tabiri, hawa watakuwa akina nani?

RESOURCES TO CHANGE LIVES RADICALLY

Coal mining is a capital and labour intensive undertaking, but it is considered a cheap source of energy for many developed economies around the world. PHOTO | FILE 

By Daniel Mbega, The Citizen Songea. For Emmanuel Kipande, 82, a resident of Liuli village, Nyasa district in Ruvuma region, who has never travelled by a train in his entire life, the construction of a railway line in Southern Tanzania was a big surprise.

KWANI PROFESA KAPUYA NI MNYAMWEZI AU NI WALE WALIOTOKEA BURUNDI, CONGO NA RWANDA? NAITAFAKARI MAKALA HII HAPA...

Usanii wa Profesa Kapuya ni matusi kwa Wanyanyembe

Toleo la 316
18 Sep 2013

MANAMBA ni binadamu, nguvu kazi ya vijana waliokuwa wakitumikishwa kwenye kilimo cha mashamba makubwa ya mkonge na hasa katika mikoa ya Morogoro na Tanga, enzi za wakoloni wa Kijerumani na Mwingereza.

UTETEZI WA JUMA KAPUYA HUU HAPA...

Profesa Juma Kapuya


TAMKO LANGU KWA UMMA JUU YA UZUSHI UNAOENEZWA DHIDI YANGU.

Ndugu wanahabari,

Baada ya kumshukuru na kumtukuza mwenyezi Mungu mwingi wa rehema. Natanguliza salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu mwanazuoni na mwanaharakati mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya Haki siku chache zilizopita huko Afrika ya kusini.

NYAYO ZA CHIFU MKWAWA (2)

Malugala Mwamuyinga, kitukuu wa Musengele Kilekamagana Munyigumba Mwamuyinga, akimsimulia mwandishi wa blog hii Bw. Daniel Mbega.
Kaburi la Musengele Kilekamagana Munyigumba Mwamuyinga 'Msigawabena' ambalo liko pembeni mwa kaburi la baba yake, Munyigumba.

Na Daniel Mbega

Ndugu zangu,
Tunaendelea na simulizi ya ‘Nyayo za Chifu Mkwawa’. Tumeona jinsi Mufwimi alivyotoka Ethiopia (kwa mujibu wa simulizi za ukoo wa Mwamuyinga) na hata alipoingia katika himaya ya Chifu Mwamduda na kujenga naye urafiki kwa sababu ya mawindo yake.