Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 3 August 2015

RAIS NKURUNZIZA AOMBA UTULIVU BURUNDI

Nshimirimana
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameomba utulivu baada ya wapiganaji waliovalia magwanda ya kijeshi kumuua mmoja ya majenerali walio na ushawishi mkubwa serikalini.

JARIDA LA EUROMONEY LA UINGEREZA LATOA TUZO YA UFANISI KWA BENKI YA NMB TANZANIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Tuzo ya Ufanisi wa kibenki nchini Tanzania iliyotolewa na Shirika la Euromoney la Uingereza  kwa benki hiyo ijulikanayo Euromoney 2015 Award for Excellence. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda.

RAIS MSTAAFU WA GHANA AKUTANA NA WAFANYAKAZI WA ECOBANK TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akisikiliza kwa makini taarifa fupi iliyosomwa mbele yake na Afisa mkuu wa ubalozi wa Ghana hapa Tanzania Dr. Ken Kwaku kuhusiana na utendaji kazi wa Ecobank nchini Ghana na bara la Afrika kwa ujumla na kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa kibiashara kati ya Ghana na Tanzania. (Katikati) ni Balozi wa Ghana nchini Kenya Mhe. Karim. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE

IMG_0282
Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.

Na Mwandishi wetu, Kibaha
MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.

FILAMU YA AISHA YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYANI PANGANI

1- moja
Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.

Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.

MMLIKI WA ST. MATHEW AIHAMISHA MAHAKAMA KWA GHARAMA ZAKE

court_gavel
Na Mwandishi Wetu, Singida
MDAI katika Kesi ya madai ya talaka Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya St. Mathew, Thadei Mtembei amehoji uhalali wa mahakama kufikia kukagua mali zake siku ya Jumamosi bila kupitia mahakama yoyote hapa Singida.

MTOTO WA MAMA NTILIE JUMAA AWESO ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NDANI CCM PANGANI

aweso
Jumaa Aweso.

Na Mohammed Hammie, Pangani, Tanga
Mtoto wa mama ntilie mwenye uzao halisi kutoka wilayani Pangani mkoani Tanga, Ndugu Jumaa Aweso (pichani) ameibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi CCM.

U-15 YAREJEA NA USHINDI KUTOKA ZANZIBAR


Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15), kimerejea leo asubuhi kutokea kisiwani Zanzibar kilipokwenda kucheza michezo ya kujipima nguvu na kombani ya U-15 ya kisiwani humo.

MALINZI AMSHUKURU TENGA

Rais wa Cecafa Leodgar Tenga (kushoto) akiwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amemshukuru Rais wa CECAFA, Leodgar Tenga kwa kuipa Tanzania uenyeji wa mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) iliyomalizika jana kwa klabu ya Azam FC kutawazwa Mabingwa wapya wa michuano hiyo.

RAIS KIKWETE AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA JIJINI TANGA LEO

Mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IRENE UWOYA KIDEDEA TABORA, AMBWAGA ZAHARA MUHIDINI MICHUZI


Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.

Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na Rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi, Bi Zahara Michuzi, alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM Mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

Sunday, 2 August 2015

LOWASSA VS CHADEMA, NANI ATAMBADILI MWENZAKE?

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiteta jambo la Edward Lowassa

Na Daniel Mbega
KIMBUNGA cha kisiasa kinatarajiwa kuanza kuonekana wiki hii Ukawa watakaporihia kwamba Edward Lowassa ndiye awe mgombea pekee wa urais kutoka umoja huo, akipitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

UZINDUZI WA ALBAMU TATU ZA MWAITEGE WAFANYIKA DIAMOND JUBILEE

 Boniface Mwaitege, amezindua albamu zake tatu leo.

MUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE WAKILI ELIAS NAWERA KUMPA USHIRIKIANO ATAKAYEPITISHWA NA CCM, AELEZEA KUHUSISHWA NA RUSHWA

  Mgombea nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.

KUNRADHI KWA PICHA HIZI: HUU NI UNYAMA, MWANAFUNZI AMUUA MWENZAKE, AMCHARANGA VIPANDE NA KUMWEKA KWENYE BEGI

Mabaki ya mwili wa mwanafunzi yakiwa yamewekwa kwenye begi.
Kichwa cha marehemu.
 Huyu ndiye mwanafunzi aliyemchinja mwenzake na kuweka viungo vyake kwenye begi na kukitelekeza kiwiliwili cha marehemu.

Achana na mauaji ya albino nchini Tanzania, wala mauaji ya vikongwe yanayochangiwa na imani za kishirikina au hata yale matukio ya uchunaji wa ngozi na hata mauaji ya kunyofoa makoromeo.

DAVID RUDISHA ASHINDWA NYUMBANI

David Rudisha
Bingwa wa mbio za Olimpiki anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 David Rudisha alishindwa kwa mara ya kwanza nyumbani Kenya.

SUDAN KUSINI YATAMBULIWA NA KAMATI YA KIMATAIFA YA OLIMPIKI


Sudan Kusini imetambuliwa rasmi na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, na hivyo kuruhusu kushiriki katika Olimpiki mwakani, huko Rio de Janeiro.

WANAJESHI WAWILI WA UTURUKI WAUAWA KATIKA SHAMBULIO

Shambulizi Uturuki
Wanajeshi wawili wa Uturuki wameuawa kwenye shambulizi la bomu katika kituo kimoja cha kijeshi mashariki mwa nchi.

WAYAHUDI WAANDAMANA DHIDI YA WANAMGAMBO

Picha ya mtoto wa Kipalestina aliyechomwa moto hadi kufa
Maelfu ya watu nchini Israeli wameshiriki kwenye maandamano wakiitaka serikali kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya wayahudi wanaotajwa kuwa wanamgambo.

SWAHIBA WA RAIS NKURUNZIZA AUAWA KWA RISASI BURUNDI

Rais Pierre Nkurunziza
Mamlaka nchini Burundi inasema kuwa Jenerali Adolphe Nshimirimana ameuawa.

ARSENE WENGER AMFUNGA MOURINHO, ARSENAL YABEBA NGAO YA JAMII

Chamberlain
Mabingwa wa kombe la FA Arsenal wameshinda kombe la Charity Shield kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuwashinda mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea 1-0 katika Uwanja wa Wembley.

'MZEE WA BASTOLA' ISMAIL RAGE AANGUKIA PUA KURA ZA MAONI CCM TABORA MJINI

Mbunge wa Tabora Mjini aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage, akionyesha bastola kiunoni huko Igunga mwaka 2011. 
Ismail Aden Rage akiongoza mapambano na wanaCCM wenzake dhidi ya wafuasi wa Chadema mjini Dodoma wakigombea kusimika bendera ya tawi.

Na Hastin Liumba, Tabora
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya Tabora mjini kimetoa matokeo ya awali ya wagombea ubunge ambapo hadi sasa mbunge Ismail Aden Rage ameanguka vibaya.

NHIF YATOA SEMINA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA YA ZAWAIYATUL QADRIYA

Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Zawiyatul Qadiria (kushoto) akipongezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF), Eugine Ngoti (wa kwanza kulia) kabla ya kukabidhiwa kadi ya matibabu ya NHIF mara baada ya kumaliza taratibu husika, kiongozi huyo alionesha mfano kwa viongozi wenzake. Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Zawiyatul Qadiria (kushoto) akipongezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF), Eugine Ngoti (wa kwanza kulia) kabla ya kukabidhiwa kadi ya matibabu ya NHIF mara baada ya kumaliza taratibu husika, kiongozi huyo alionesha mfano kwa viongozi wenzake.

NI CHELSEA NA ARSENAL LEO KATIKA NGAO YA JAMII

Ligi Kuu ya Uingereza inaanza tena leo Jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa Kombe la FA Arsenal katika mechiya Ngao ya Jamii itakayogaragazwa katika uwanja wa Wembley.

KAMPUNI YA MAFUTA SOMALIA YACHUNGUZWA


Idara ya Uingereza inayopeleleza udanganyifu mkubwa, inachunguza tuhuma za rushwa, kuhusu kampuni ya mafuta ya Uingereza inayofanya kazi Somalia.

WAPIGANAJI 260 WA KIKURDI WAUWA


Shirika la habari la taifa la Uturuki, linasema kuwa wapiganaji wa Kikurd 260 wameuawa katika mashambulio ya ndege ya juma moja, dhidi ya kundi la PKK, lilopigwa marufuku.

MAELFU WAFURIKA KUTAZAMA UKUTA WA MIUJIZA


Maelfu ya raia katika mji mkuu wa Mali, Bamako, wanaendelea kufurika ili kujionea kile kilichotajwa kuwa muujiza wa kidini katika ukuta mmoja ambao ulionekana wikiendi iliopita.

MGOGORO WA UONGOZI WALIKUMBA KUNDI LA TALEBAN

Wapiganaji wa Taleban

Msemaji wa baraza kuu la kundi la Taliban nchini Afghanistan ameimbia BBC kuwa hawakuombwa ushauri wakati wa uteuzi wa hivi majuzi wa kiongozi mpya kufuatia kifo cha mwanzilishi wake Mullar Omar.

Saturday, 1 August 2015

POLICE KILL FOUR AT FOMER MINISTER'S HOUSE

A pistol recovered from a suspected gangster in a past shootout. Police in Nairobi shot dead four men allegedly found stealing froma house in Loresho. FILE PHOTO | NATION MEDIA GROUP 
By STELLA CHERONO
Police on Saturday morning gunned down four suspected robbers in former Cabinet Minister Musikari Kombo’s Loresho home and recovered two pistol and ten rounds of ammunition. 

KATIBU WA CCM WILAYA AKUTWA NA KURA ZA MAONI OFISINI KWA MGOMBEA

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe

NA JUMA MOHAMMED
Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani hapa kimetengua uteuzi wa aliyekuwa katibu wa chama hicho wilaya ya Newala, Juma Namkoveka, baada ya kukutwa akichapisha kura za maoni kwenye ofisi ya mmoja wa watia nia ya ubunge.

KADA WA VIJANA CHADEMA AUAWA KWA RISASI

By Joseph Kapinga na Bakari Kiango, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Vijana Chadema Tawi la Luis, Mbezi Luis, Dar es Salaam, Dennis Kasanga ameuawa kwa kupigwa risasi shingoni usiku wa kuamkia jana, huku taarifa zilizotolewa na polisi zikitofautiana na mashuhuda wa tukio hilo.

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA AGOSTI 6


Dirisha la Usajili kwa Vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (RCL) linatarajiwa kufungwa tarehe 06 Agosti, 2015.

KIINGILIO CHA FAINALI KAGAME KESHO NI ELFU TATU


Michuano ya Vilabu Bingwa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kufika tamati kesho jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa mchezo wa Fainali utakaozikutanisha timu ya Azam FC dhidi ya Gor Mahia.

KAMATI YA UTENDAJI TFF YATOA MAAMUZI MAZITO


Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichokutana leo kimepitia na kutoa maamuzi yafuatayo:

TAKUKURU YAKANUSHA TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA NAPE

SUSPEND FUNDRAISINGS IN CHURCHES, SAY CLERGY

Joshua Kitakule

By JOHN OKOT
Gulu.
The secretary general of the Inter-Religious Council of Uganda (IRCU) has asked all religious leaders in the country to suspend fundraising activities in the places of worship as 2016 elections draw closer.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAFANYIWA SHEREHE YA KUKARIBISHWA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO DAR

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa jana katika Kijiji cha Makumbusho.

ASKARI WA TANAPA ASHINDA TUZO YA ULINZI WA FARU AFRIKA


NA JOHN NGUNGE
Ushindi wa tuzo ya askari bora katika ulinzi wa faru barani Afrika, “2015 Rhino Conservation Awards” aliyoipata askari wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Malale Patrick Mwita, umeipaisha Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kimataifa katika uhifadhi na ulinzi wa mnyama huyo adimu.

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA IPTL DHIDI YA KAFULILA

Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, David Kafulila

NA BEATRICE SHAYO
Kesi  ya kashfa iliyokuwa imefunguliwa na IPTL dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, David Kafulila, imetupiliwa mbali na Mahakama Kuu. 

WANACCM ZANZIBAR WAKATAA KUMUUNGA MKONO LOWASSA

Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini, Muhammed Nyawenga

NA RAHMA SULEIMAN
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, wamesema hawapo tayari kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kwa kitendo cha kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema.
Wametoa tamko hilo jana mbele ya waandishi wa habari katika ofisi kuu za CCM Kisiwandui. 

WANACHAMA 60 WA CCM BABATI WATUA CHADEMA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimevuna  wanachama 60 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kitongoji cha Wangbay, kijiji cha Logia, Kata ya Sigino Wilaya ya Babati.

GOR MAHIA YATINGA FAINALI BAADA YA MIAKA 30


Timu ya Gor Mahia kutoka Kenya imeilaza AL Khartoum ya Sudan 3-1 na kufuzu kwa fainali ya mchuano wa Kagame kwa vilabu vya soka kanda ya Afrika Mashariki na kati CECAFA inayoendelea mjini Dar es Salaam Tanzania.

POLICE TRAIN 180 SPECIAL OFFICERS FOR ELECTIONS

Assistant Commissioner of Police (ACP) Mary Nzuki

The police has trained 180 officers in Public Order Command to strengthen security for the general election in October.

PCCB ARRESTS NAPE FOR ATTEMPTED BRIBERY

Nape Nnauye
The Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) has arrested Chama Cha Mapinduzi Secretary for Ideology and Publicity Nape Nnauye accusing him of attempting to bribe some of party members.

USAID HELPS 940 IRINGA VILLAGERS TO OWN LAND

United States Agency for International Development (USAID)

BY FRIDAY SIMBAYA
United States Agency for International Development (USAID) has mapped and registered land for more than 940 Ilalasimba villagers in Iringa Rural District to help rural people own land.

VIKWAZO VINNE VYA URAIS WA LOWASSA HIVI HAPA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (wa pili kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa fomu za kugombea urais kupitia chama hicho jana kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Regina ambaye ni mke wa Lowassa, na kulia ni Naibu Katibu MKuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu. Picha na Edwin Mjwahuzi 

By Nuzulack Dausen, Mwananchi
Dar es Salaam. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alichukua fomu za kuomba ridhaa ya Chadema kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano, lakini anakabiliana na vikwazo vinne kabla hajafanikiwa kuongoza upinzani kutwaa madaraka kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi.

WAHAMIAJI 2,000 WANASWA WAKIJIANDIKISHA KUPIGA KURA


Idara ya uhamiaji nchini imesema inawashikilia wahamiaji haramu 2,048 kutoka nchi mbalimbali kwa tuhuma za kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.