Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiendelea na kazi ya
kuchambua maoni yaliyotumwa na wadau wa habari ili kuboresha Muswada wa Sheria
ya Huduma za Habari leo mjini Dodoma.
(Picha na MELEZO)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO, Dodoma
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inaendelea na kazi yao ya
kutunga Sheria ya Huduma za Habari kwa kutumia maoni yaliyowasilishwa na wadau
mbalimbali na kuwasilisha Serikalini kabla ya kupelekwa Bungeni ili muswada ukajadiliwe na Wabunge na hatimaye
kupatikana Sheria ya Habari ambayo inalenga kuleta heshima kwa Watanzania.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mhe. Peter Serukamba amebainisha hayo leo mjini Dodoma alipokuwa
akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kabla ya Kamati hiyo kuendelea na kazi
yake ya kuchambua maoni yaliyotumwa na wadau wa habari ili kuboresha Muswada huo
kabla ya kuwasilishwa Bungeni kusomwa kwa mara ya pili.
Serikali
imekuwa ikiwasikiliza wadau wa habari kwa muda mrefu licha ya kuwa na tabia ya
kutokuwasilisha maoni yao kila mara wanapoomba kupewa muda wa kutoa maoni yao juu
ya kuboresha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari nchini.
“Ni vizuri ifahamike, huu ndio umekuwa mchezo
wa Muswada huu tangu mwaka 1993, kila mara Muswada ulipokuja Bungeni, wadau
walisema hawapo tayari wanasema utoke” alisema Mhe. Serukamba.
Aidha,
Mhe. Serukamba amesisitiza kuwa huo umekuwa ni mtindo wa wadau hao kwa miaka zaidi
ya 22 sasa ambapo Serikali imekuwa imekuwa ikiwasililiza kila waliposema hawapo
tayari, muswada huo ulitolewa Bungeni.
Kufuatia
tabia ya wadau kutokuwasilisha maoni yao kwa kisingizio cha kutopewa muda Mhe.
Serukamba amesisitiza kuwa kamati itaendelea kujadilia maoni yaliyowasilishwa
kwako na kuahidi kutunga Sheria itayozingatia na kujali maslahi ya wadau wote
wa habari ili kuufanya Muswada huo kuwa wenye tija kwa wananchi na taifa kwa
kuleta mabadiliko katika tasnia ya
habari nchini.
Ili
kusimamia nia na maslahi ya wadau na taifa, Serikali imeuleta tena Muswada huo
Bungeni ambapo Kamati ya Huduma za jamii inaendelea kuujadili na kuchambua
maoni yaliyowasilishwa na wananchi pamoja na wadau wa habari kwa njia
mbalimbali ikiwemo kwa maandishi kupitia barua pepe ya Bunge cna@bunge.go.tz
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo amewataja wadau waliothibitisha kupokea barua ya mwaliko wa
kuleta maoni yao kwa Kamatikuwa ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS), MCT, LHRC, UTPC pamoja na Pili Mtambalike.
No comments:
Post a Comment