TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania kuongoza nchi za Afrika katika maboresho ya utoaji haki za watuhumiwa na mahabusu
UTEKELEZAJI
wa Miongozo ya Luanda (Luanda Guidelines) kuhusu ukamataji na
ushikiliaji wa watuhumiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka utakaoanza hivi
karibuni unatarajiwa kuimarisha haki za watuhumiwa na mahabusu nchini.
Aidha,
miongozo hiyo inatarajiwa kuipunguzia Serikali mzigo mkubwa wa gharama
za uendeshaji wa mahabusu na magereza ambayo mengi yao yana msongamano
mkubwa wa watuhumiwa na wafungwa.
Kutokana
na tafiti zilizofanyika barani Afrika ikiwemo Tanzania imebainika kuwa,
kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kwenye mchakato mzima wa mfumo
wa haki–jinai (criminal justice) ambao unaanzia pale mtu anapokamatwa
na vyombo vya dola (arrest), wakati wa mahojiano (interrogation) na hata
anapokuwa mahabusu katika vituo vya polisi na magerezani.
Kwa
mujibu wa taarifa za kiutafiti, wengi wao wanakamatwa pasipo utaratibu,
kudhalilishwa, kuteswa, kubambikiwa kesi, kuwekwa muda mrefu bila
kufikishwa mahakamani na kuwepo mazingira magumu ya dhamana jambo
linalokiuka haki za binadamu zilizoainishwa katika Ibara ya 12 mpaka 24
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sheria
nyinginezo za nchi pamoja na Mikataba ya Kimataifa ambayo nchi
imeridhia.
Miongozo
hii inatanabaisha namna binadamu walioko katika hali na mazingira tajwa
wanapaswa kuangaliwa kulingana na taratibu, kanuni na sheria zenye
vigezo na viwango vya kitaifa na kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Miongozo
hii inahimiza uzingatiaji wa haki za binadamu katika mfumo wa
haki-jinai - yaani katika hatua ya ukamataji na uhifadhi wa watuhumiwa
wa uhalifu kabla hawajafikishwa mahakamani (Arrest and Pre-Trial
detention) kama vile mahabusu za polisi na magereza.
Kwa
mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Mtandao wa
wataalamu wa masuala ya kipolisi kutoka taasisi za Serikali na zisizo za
Kiserikali Afrika (African Policing Civilian Oversight Forum – APCOF)
yenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini asilimia 50 ya watu
wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini ni mahabusu ambao, ama
wanasubiri kufikishwa mahakamani au kesi zao bado zinaendelea katika
mahakama mbalimbali (yaani hawajahukumiwa). Hali hii inaisababishia
Serikali gharama kubwa za uendeshaji wa taasisi hizo.
Kuanza
kutekelezwa kwa Miongozo hii ya Luanda kutaipunguzia Serikali gharama
za uendeshaji kutokana na kupungua kwa idadi ya watu watakaokuwa
wakishikiliwa vizuizini kwa kuwa wengi wengi wao wanashikiliwa kwa
makosa ambayo yana dhamana (bailable offences) yakiwemo makosa madogo
madogo kama vile wizi mdogo mdogo na kadhalika
Athari
za watu kushikiliwa vizuizini pasipo ulazima ni pamoja na Serikali
kuendelea kubeba mzigo mkubwa wa gharama za uendeshaji, watuhumiwa wa
uhalifu (mahabusu) kupata magonjwa ya kuambukizwa kutokana na
msongamano, kupata ulemavu na hata kufariki kutokana na mateso pale
ambapo watumishi wa vyombo vya dola wanapotumia nguvu kupita kiasi
wakati wa ukamataji na mahojiano.
Athari
za kiuchumi ni pamoja na familia nyingi huathirika kwa kukosa mahitaji
muhimu kama vile chakula, elimu kwa watoto, matibabu n.k kutokana na
watafutaji (breadwinners) kushikiliwa vizuizini kwa muda mrefu.
Matatizo yaliyopo
Ukamataji unaofanywa na vyombo vya dola hususan jeshi la polisi mara nyingi unakiuka haki za binadamu kwani tafiti zinaonyesha kwamba kumekuwepo na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya watuhumiwa, ambapo huambatana na vitendo vya utesaji wa watuhumiwa. Utesaji huo hufanywa wakati wa mahojiano (interrogation) kwa lengo la kuwashinikiza watuhumiwa kukiri makosa. Takwimu za tafiti zilizofanywa na Tume nyakati tofauti zinaonyesha pia kwamba yapo malalamiko mengi yanayopokelewa kutoka kwa watuhumiwa na wafungwa wanaolalamikia kubambikiwa kesi na polisi.
Ukamataji unaofanywa na vyombo vya dola hususan jeshi la polisi mara nyingi unakiuka haki za binadamu kwani tafiti zinaonyesha kwamba kumekuwepo na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya watuhumiwa, ambapo huambatana na vitendo vya utesaji wa watuhumiwa. Utesaji huo hufanywa wakati wa mahojiano (interrogation) kwa lengo la kuwashinikiza watuhumiwa kukiri makosa. Takwimu za tafiti zilizofanywa na Tume nyakati tofauti zinaonyesha pia kwamba yapo malalamiko mengi yanayopokelewa kutoka kwa watuhumiwa na wafungwa wanaolalamikia kubambikiwa kesi na polisi.
Aidha,
kuna mapungufu katika mfumo wa sheria za jinai nchini Tanzania.
Mathalani, ingawa Ibara ya 13(6)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya
mwaka 1977 inakataza utesaji kwa watuhumiwa na kuelekeza mamlaka za nchi
kutunga sheria kwa minajili hiyo, bado kuna upungufu katika sheria
kwani Kifungu cha 29 cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 ya Sheria za
Tanzania kinakataza ushahidi uliopatikana kwa shinikizo la aina yoyote
kutumika kama ushahidi halali mbele ya mahakama.
Hivyo,
mapungufu yanayojitokeza ni kwamba Sheria za nchi zinakataza vitendo
vya utesaji kwa watuhumiwa wa uhalifu lakini hazitamki wazi ni hatua
gani zitachukuliwa dhidi ya mtumishi wa chombo cha dola ambaye
atajihusisha na vitendo vya utesaji wa watuhumiwa. Nafuu (remedy) pekee
ya kisheria inayopatikana ni muathirika (victim) kufungua kesi ya madai
dhidi ya serikali. Kwa upande mwingine, Sheria ya Kukazia Haki na Wajibu
(Basic Rights and Duties Enforcement Act) ya mwaka 1994 nayo pia
changamoto kwani ili kesi inahyohusu ukiukwaji wa haki za binadamu
isikilizwe, linahitajika jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu. Katika
mazingira ya sasa, upatikanaji wa jopo hilo ni mgumu kutokana na
upungufu wa maji.
Tatizo
jingine kubwa katika ukamataji, ushikiliaji watuhumiwa vituo vya polisi
na kabla ya kesi kusikilizwa ni uelewa mdogo wa sheria, kanuni na
taratibu zinazohusiana na haki za binadamu katika mfumo wa haki-jinai.
Kufuatia
matatizo yaliyobainishwa hapo juu (matatizo katika ukamataji na
ushikiliaji wa watuhumiwa katika mahabusu zilizoko katika vituo vya
polisi na sehemu nyingine wanamoshikiliwa watuhumiwa kabla ya
kushtakiwa), Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (African
Commission on Human and Peoples Rights - ACHPR) ilianzisha mchakato wa
kuandaa Miongozo (Guidelines) ya namna ya kukuza na kulinda haki za
binadamu nyakati za kukamatwa kwa watuhumiwa, kuwekwa ndani ya selo za
polisi na wakiwa mahabusu za magereza.
Miongozo
hii iliridhiwa katika Mkutano Mkuu wa 55 wa Tume hiyo uliofanyika
Luanda, Angola Mei, 2014 na hivyo kujulikana kama “Luanda Guidelines.”
Luanda Guideline ziliandaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 45(1)(b) ya Mkataba
wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and
People Rights) wa mwaka 1981.
Aidha,
katika kutekeleza jukumu tajwa na mchakato uliopitishwa na ACHPR,
Miongozo imeanza kufanyiwa kazi kwa kuitambulisha kwa nchi wanachama wa
Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) ili kuijua na kisha kurekebisha
taratibu, kanuni na sheria za jinai za nchi husika ili ziendane na
miongozo tajwa.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi tano (5) za mwanzo Afrika zilizopewa kipaumbele
katika utekelezaji wa miongozo hiyo ambayo itapelekea maboresho ya mfumo
wake wa haki-jinai. Nchi nyingine zilizopewa kipaumbele sambamba na
Tanzania ni Zimbabwe, Malawi, Tunisia na Ivory Coast.
Mwelekeo
THBUB kwa kushirikiana na African Policing Civilian Oversight Forum – APCOF, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) pamoja na wadau wengine ndani ya serikali na asasi zisizo za serikali imeanza mchakato wa kuhamasisha utekelezaji wa Luanda Guideline hapa nchini. Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ofisi ya Kanda ya Afrika ndilo linalofadhili mchakato huu kwa sasa.
THBUB kwa kushirikiana na African Policing Civilian Oversight Forum – APCOF, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) pamoja na wadau wengine ndani ya serikali na asasi zisizo za serikali imeanza mchakato wa kuhamasisha utekelezaji wa Luanda Guideline hapa nchini. Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ofisi ya Kanda ya Afrika ndilo linalofadhili mchakato huu kwa sasa.
Mchakato
bado upo katika hatua za awali ikiwa ni pamoja na kuandaa Mpango-Kazi
wa Utekelezaji, kubaini taasisi zitakazo husika na utekelezaji huo na
muda wa utekelezaji wa Luanda Guidelines.
Hata
hivyo, zoezi la kutambulisha miongozo hii limekwishaanza tangu mwishoni
mwa mwezi uliopita kwa warsha iliyowashirikisha wadau mbalimbali wa
hapa nchini. Katika warsha hiyo ya siku mbili wadau walipata fursa ya
kutoa mawazo yao juu ya Mpango-Kazi wa Utekelezaji wa miongozo hii. Na
kwa kupitia kwenu tunatarajia wadau na wananchi wengi zaidi watapata
taarifa juu ya miongozo hii - tunaomba ushirikiano wenu.
Hatua
zitakazofuata hapo baadaye zitajumuisha kufanya mapitio ya sheria za
jinai zinazohusiana na ukamataji na ushikiliaji wa watuhumiwa na
kubainisha mapungufu yaliyomo na kisha kuzifanyia marekebisho sheria
hizo ili zikidhi viwango vilivyoainishwa katika Luanda Guidelines.
Pale
ambapo mapungufu yatabainika kuwepo katika utekelezaji, sheria zitungwe
au kurekebishwa ili kuwabana watendaji wa vyombo vya dola wanaokiuka
sheria na miongozo ya kazi zao.
Kwa
ujumla utekelezaji wa dhati wa sheria zilizopo au zitakazofanyiwa
marekebisho au zitakazotungwa upya utasaidia kuimarisha utawala wa
sheria, utu wa mtu, uhuru binafsi wa mtu, amani na utulivu nchini.
Tanzania
ni mwanachama wa Umoja wa Afrika na imeridhia Mkataba wa Afrika wa Haki
za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples Rights). Kwa
kuridhia mkataba huo, Tanzania inapaswa kutekeleza Haki za Binadamu kama
zilivyoainishwa katika Mkataba huo pamoja na miongozo mingine ya Haki
za Binadamu ambayo imebuniwa kwa mujibu wa Mkataba huo.
ACHPR imepewa mamlaka ya kusimamia haki za binadamu barani Afrika kama zilivyoainishwa katika Mkataba.
Ili
kufanikisha majukumu yake, ACHPR imekuwa ikishirikiana na Taasisi za
Kitaifa za Haki za Binadamu kama vile Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora kwa upande wa Tanzania. THBUB ina hadhi ya mwanachama
shirikishi (affiliate member) katika ACHPR.
THBUB inatoa wito kwa wadau kuonesha ushirikiano ili tuwe na mifumo mizuri itakayoimarisha haki za binadamu nchini Tanzania.
Pamoja tunaweza, tekeleza wajibu wako, tulete maboresho katika mfumo wa haki-jinai nchini.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tuandikie au tupigie simu:
E-mail: chragg@chragg.go.tz au nabor.assey@chraggg.go.tz au germanus.joseph@chragg.go.tz au jamila.sulu@chragg.go.tz
Simu: +255 22 2135747/8; 2135222; 784 873 761; 784 329 900;
714 775 722.
714 775 722.
No comments:
Post a Comment