Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 21 September 2014

TANESCO YAWATIA MBARONI WEZI 30 WANAOHUJUMU UMEME


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog


Arusha.
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha limewakamata zaidi  ya wezi 30 wanaohujumu shirika hilo kwa kujiunganishia umeme kwa wizi bila ya kufuata kanuni na sheria za shirika.
Aidha kukamatwa kwa wezi hao kunatokana na

operesheni endelevu ambayo tayari imeshaanza katika wilaya za Meru, Mererani pamoja na Arusha mjini ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakijiunganishia umeme wa wizi na hivyo kusababisha madhara mbali mbali kwa jamii wanazoishi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana  mara baada ya kukamata baadhi ya wezi hao katika operesheni iliyofanyika ngaramtoni katika kijiji cha Emaoi, ofisa usalama wa Tanesco mkoa  Kembe Sabini alisema kuwa tayari watu  hao wameshakamatwa kutokana n shirika kuamua kufanya zoezi la wanaoiba umeme.
Alisema kuwa kati ya watu hao waliokamtawa baadhi yao watafikishwa
mahakamani huku wengine wakilipa fidia kutokana na makosa waliyokutwa nayo ambayo hayakuzingatia kanuni na sheria za kujiunganishia umeme.
Alifafanua kuwa ni vema jamii ikatambua madhara ya kujiunganishia umeme wa wizi kwa kuwa mara nyingi wamekuwa wakijiunganishia bila utaalam wa aina yeyote na hivyo kuleta madahara kama vile ya nyumba kuungua.
“Naishauri jamii ichane na wizi wa kujiunganishia umeme kwani ni hatari sana nah ii imekuwa pia hata ikiletea shirika hasara huku hata na jamii nayo ikipata hasara kwani wezi wote tunaowakamata lazima tuwachukulie hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa faini ambazo zingeweza hata kuwasaidia wao na familia zao”aliongeza Sabini.
Hata hivyo aliitaka jamii kutambua kuwa kwa sasa shirika hilo lipo kwenye zoezi hilo ambalo ni endelevu na wajue kuwa ni hatari hasa pale wanapotumia miti kwa kujipitishia nyaya za umeme.
Mmoja wa watu hao wanaohujumu umeme  ambaye ni Ismaely Gideon mara bada ya kukamatwa alishikwa na kigugumzi cha kujieleza huku akidai kuwa yeye hana matumizi makubwa ya umeme bali ni watoto wake ndio waliohusika kujiunganishia umeme huo.

No comments:

Post a Comment