Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 21 September 2014

TAASISI ZA DINI ZATAKIWA KUCHUNGUZA MAJANGA MBALIMBALI YANAYOTOKEA DUNIANI


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha.
VIONGOZI wa dini pamoja na taasisi zao wametakiwa  kuhakikisha wanaangalia majanga mbalimbali ambayo yapo kwenye jamii na kisha kuwatahadharisha waumini wao kwani kwa kufanya hivyo kutweza kuokoa nchi na bara la Afrika dhidi ya majanga mbalimbali ambayo kwa wakati mwingine yanaweza kuepukika.
Pia wakati wanawatadharisha waumini wao pia wanatakiwa kuwa

wachunguzi wa majanga hayo ili  wanapotoa elimu hiyo iweze kufikia kwenye jamii kwa haraka sana.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa mtandao wa Leadership Empowerment Africa Region Network (LEARN) Miburo Celestin wakati akiongea kwenye kongamano ambalo liliwahusisha viongozi mbalimbali wa dini kutoka barani Afrika.
Miburo alisema,kwa sasa viongozi wengi wa dini wanajikuta wakiwa wanawahutubia waumini wao mambo ya dini pekee na kuacha majanga mbalimbali ambayo wakati mwingine yanasababisha hata vifo visivyo na hatia kwenye jamii.
Alidai umefika wakati sasa wa viongozi wa dini kuweza kuhubiri vitu ambavyo vinatokea au vitatokea kwenye jamii kama vile majanga ya magonjwa, vifo, ukame kwani kama watahubiri basi wataweza kuisaidia jamii.
“Viongozi wa dini wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwa waelimishaji hasa pale ambapo wanapokutana na waumini wao tofauti na serikali ambapo ikitaka kuwaelimisha wananchi wake ni lazima iwakutanishe kwenye semina , ni muhimu sasa tukabadilika”aliongeza Miburo
Aliendelea kwa kutolea mfano wa Gonjwa la ebola ambapo alidai kuwa kelele nyingi ambazo zinapigwa zinatokea zaidi kwa viongozi wa serikali kuliko wale wa dini kitu ambcho viongozi wa dini sasa wanatakiwa kubadilika.
Alimalizia kwa kusema kuwa umefika wakati sasa wa Viongozi wa dini kubadilika lakini pia kuwa watafiti, wachunguzi na hata wafumbuzi wa masuala ambayo yanaweza kuepukika kwenye jamii zetu.
Hataivyo Mwenyekiti wa mtandao huo hapa nchini, Philemon Mashauri alidai kuwa mtandao huo utaendelea kuwalea viongozi wa dini kwa kuwapa elimu mbalimbali ambazo ni muhimu kwao na maslahi ya taifa kwa Ujumla.

No comments:

Post a Comment