Baada ya Watu wengi kujiuliza maswali mengi juu ya alipo Sandu George, maarufu kwa jina la Kid Bway (Pichani), ambae kwa muda mrefu amejizolea sifa kubwa katika tasnia ya utangazaji na uandaaji wa muziki, ukweli ni kwamba amejiunga na kituo kipya cha redio Jijini Mwanza kiitwacho Lake Fm, Raha Ya Rock City.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday, 6 April 2016
STARTIMES YAPELEKA VIZIMBUZI BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANANCHI WAFURAHIA
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, Salimu Juma Mavaga (kushoto), akizungumza wakati wa kupokea vizimbuzi 'ving'amuzi' vya Kampuni ya StarTimes vilivyo tolewa kwa gharama ya shs. 50,000 kwa wananchi wa vijiji vitatu vya Yombo, Chasimba na Maimbwa wilayani humo jana.
NAIBU WAZIRI WA HABARI ALIPOTEMBELEA CHUO CHA TASUBA BAGAMOYO
Kaimu Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba)
Bw. Michael Kadinde wa kwanza kushoto akimfafanulia jambo Naibu Waziri
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura kulia
wakati wa ziara ya Mh. ya Mheshimiwa Waziri aliyoifanya katika Taasisi hiyo
iliyopo Bagamoyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili. (Picha na
Benjamin Sawe- WHUSM).
TAARIFA KWA UMMA: KUFUTWA KWA SAFARI ZA NDEGE APRILI 2, 2016
Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa
kufika kwenye maeneo waliyokusudia jioni ya Aprili 2, 2016.
Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa
mfumo wa taa kwenye njia ya kurukia kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na
hivyo kukosekana kwa usalama ambao
ungewawezesha marubani wetu kutua.
TAASISI YA GRACA MACHEL YAZINDUA MRADI WA KUWASAIDA WATOTO WALIO NJE YA SHULE
Na Rabi Hume, Modewjiblog, Mara
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto, Taasisi ya Graca Machel kwa kushirikiana na serikali imefanya uzinduzi wa mradi ulio na malengo ya kuwarudisha shule watoto 20,000 waishio mkoa wa Mara ambao hawakupata nafasi ya kuwa shuleni.
Akizungumzia mradi huo, Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel alisema taasisi yake imeanzisha mradi huo kwa kutambua kuwa kuna idadi kubwa ya watoto walio nje ya shule kwa sababu mbalimbali hivyo kupitia mradi huo ni matarajio yao kuona watoto wakirudi shule ili kupata elimu ambayo itawasaidia kwa maisha yao ya baadae.
TIGO YAWAPA WATEJA WAKE OFA ZAIDI KWENYE WHATSAPP YA BURE
Mkuu wa Kitengo Kitengo cha Vifaa vya Intaneti wa Tigo , David Zakaria akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha (Picha na Maktaba) |
- Wateja watafurahia ofa hizo wakinunua kifurushi cha shilling 1,000
Dar es Salaam, Aprili 5, 2016 -Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa maisha ya kidijitali imeboresha ofa yake ya WhatsApp ya bure kwa kutangaza kuwanufaisha zaidi wateja wake pindi wanaponunua kifurushi cha kila siku cha extreme kwa shilingi 1,000.
MAMBO 9 MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU UKATILI KWA WATOTO
RAIS WA RT, ANTHONY MTAKA AULA SHIRIKISHO LA RIADHA LA DUNIA (IAAF)
Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO la
mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha nchini
(RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri wa
mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.
FASTJET YASITISHA SAFARI ZA KILIMANJARO-NAIROBI
Dar es Salaam, Aprili 4, 2016 -Fastjet
Tanzania imesitisha safari zake kati ya Kilimanjaro na Nairobi.
Fastjet
ilikuwa ikifanya safari kutoka Uwanja wa
Kimataifa wa Kilimanjaro kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi
mara mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapaili.
Kusitishwa kwa
safari kwenye njia hiyo kunatokana na kuwepo mahitaji haba ya abiria kwenye
masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi hali iliyosababisha kutokuwa na
manufaa kibiashara.
Tuesday, 5 April 2016
CHACHA AJIUZULU TFF
Martin Chacha (kushoto) wakati alipokuwa mwanasheria wa klabu ya Yanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF kuanzia leo tarehe 5 Aprili 2016.
KAIRUKI ATOA WIKI MOJA KWA WAAJIRI KUWASILISHA WATUMISHI HEWA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato unaoendelea wa kubaini
watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
WIZARA YA ARDHI YAHUDUMIA WANANCHI 41.932 KWA MIEZI MITANO
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Nathaniel Methew akiwaeleza
waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kuboreshwa kwa mifumo ya
utoaji huduma kwa wananchi kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA hali iliyochangia kuongeza tija
kupitia kituo cha huduma kwa mteja kilichopo Makao Makuu ya Wizara hiyo na Katika
Ofisi zote za Kanda. Kushoto ni Msajili
wa Hati Msaidizi.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Bw. Ibrahim Mussa (kulia)
akiongea na Kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha Bi. Maria
Kirombo (kati) na Mhifadhi wa Idara ya Ulinzi Bw. Haima Hera muda mfupi
kabla ya kuwasili kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii kwa ziara fupi hifadhini hapo.
KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA VUNJO,MREMA AKUBALI YAISHE ,AMTAMBUA MBATIA KAMA MBUNGE HALALI WA JIMBO LA VUNJO
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia (TLP) ameshinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Lyatonga Mrema .
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Kangi Lugola, wakati Kamati
hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni
mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Juliana Shonza.
TANZIA: TANGAZO LA MSIBA WA BARAKA KOMBE TANZANIA NA LONDON
TUNASIKITIKA MNO KUTANGAZA KIFO CHA BARAKA KOMBE (MTANZANIA MWENZETU PICHA YAKE HAPO JUU) KILICHOTOKEA JANA JUMAPILI 03/04/16. MSIBA UKO 88 B TEMPLETON AVENUE, CHINGFORD, LONDON, E4 6SP. MIPANGO YA MAZISHI INAFANYWA NA NDUGU ZAKE MAREHEMU NA TUTAWAARIFU BAADAYE KIDOGO.
SHIRIKA LA EfG LAFANYA TAMASHA LA KUPINGA UKATILI WA JINSIA AWAMU YA PILI KATIKA SOKO LA MCHIKICHINI ILALA JIJINI DAR
Ofisa Ufutiliaji na Tathmini wa Shirika la Eguality for Growth (EfG), Shabani Lulimbeye, akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu vitendendo vya ukatili wa kijinsia katika Tamasha lililofanyika jana katika viwanja vya Soko la Mchikichini Ilala jijini Dar es Salaam.
WAJASIRIAMALI DAR WANUFAIKA NA MAFUNZO KUHUSU FURSA MPYA KATIKA KILIMO BIASHARA
Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akiwasilisha malengo ya warsha kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida kufungua warsha hiyo.
Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kupata nafasi ya mafunzo yanayohusu fursa mpya zinazopatikana katika kilimo cha biashara katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).
MDUARA UNAPOCHANGANYWA NA RAGGA JIBU NI "KITIMTIM" (VIDEO)
Muziki unakua sana na hivi karibuni wasanii wengi wa hapa nchini wamekuwa wakibuni mitindo ya aina mbalimbali ili kuzifanya kazi zao ziende mbali na kuvuta mashabiki wa muziki nchini na duniani kwa ujumla. Bayo the Great ni msanii wa kizazi kipya aliyewahi kuvuma na wimbo wa hiphop uitwao Jina Kapuni: https://www.youtube. com/watch?v=qncTaBUAL7E Baada ya ngoma hii Bayo alikaa kimya akifanya shule na baadae kuajiriwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kazi za kijamii kama Solar Aid, The Nature Conservancy, International Citizen Service na Voluntary Service Overseas (VSO) ambako Bayo ameajiriwa mpaka sasa kama Meneja mradi huko Zanzibar.
SERIKALI YASEMA WAHISANI WATAENDELEA KUISADIA TANZANIA KATIKA BAJETI KUU YA 2016/2017
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Tamko hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Washirika wa Maendeleo bado wanaendelea kuisadia Serikali katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa makundi 14 ya kuisaidia bajeti ya Tanzania sio za kweli.
KAMATI YA MISS TANZANIA YAZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI ARUSHA
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.
Baada ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika uzinduzi huo.
Sunday, 3 April 2016
WAZIRI KITWANGA ATOA MSAADA WA BAISKELI 120 KWA MAKATIBU WA MATAWI CCM JIMBONI KWAKE MISUNGWI LEO
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani
Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza,
Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa CCM Jimbo la
Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya shughuli za chama jimboni humo. Makabidhiano
hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya Chama hicho, mjini Misungwi.
LIGI KUU VODACOM KUENDELA JUMATANO
Mchezo kati ya Young African dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Jumatano ya April 6, 2016 umesogezwa mbele na sasa utachezwa tarehe 16 Aprili 2016 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Jumatano ya Aprili 6, ligi kuu itaendelea kwa michezo miwili tu, Azam FC watakua wenyeji wa Ndanda FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, huku Majimaji FC wakiwakaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Majimaji Songea.
MAAMUZI YA TFF: KIAMA CHA JKT OLJORO, GEITA GOLD HUKU WENGINE WAKIFUNGIWA MAISHA
Wakili Msemwa
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League).
TIGO YAFUNGUA DUKA JIPYA WILAYANI HANDENI
RAILA ODINGA AMTEMBELEA RAIS DKT. MAGUFULI NYUMBANI KWAKE CHATO MKOANI GEITA
Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasili kwenye viwanja
vya Shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kwenda kumsalimia Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha
Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake Chato mkoani Geita
mara baada ya Kuwasili.
LA KWETU CONCERT, TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI 2016 KUFANYIKA NCHINI TANZANIA
Linatarajiwa Kufanyika Tamasha Kubwa la Muziki wa Injili hapa nchini. Tamasha hilo limepewa jina la "LA KWETU CONCERT" na litafanyika katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga, Mbeya, Arusha, Dar es salaam na mingineyo.
Saturday, 2 April 2016
WAZIRI KITWANGA ATIKISA JIMBONI KWAKE MISUNGWI, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani
Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akishangiliwa na mamia ya wananchi wa
Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa
ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao. Waziri
Kitwanga ameanza ziara jimboni humo leo. Picha zote na Felix Mwagara.
NOAH YAACHA NJIA BANDARINI JIJINI DAR ES SALAAM NA KUTUMBUKIA KWENYE MTARO
Mwananchi wakiangalia ajali ya Noah yenye namba za usajili T 367 DAK iliyoacha njia na kutumbukia kwenye mtaro jirani na Kanisa la Mtakatifu Joseph, Bandarini Dar es Salaam jana asubuhi.
WAZIRI NAPE ALIPOKUTANA NA WASAMBAZAJI WA FILAMU NA MUZIKI NCHINI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiongea na
wasambazaji wa filamu na muziki nchini wakati wa mkutano kati yake na
wasambazaji hao uliojadili namna gani ya kuboresha tasnia hiyo kwa manufaa ya
wasanii, wasambazaji na uchumi wa Taifa.(Picha Na Benjamin Sawe- WHUSM).
KATIBU MKUU UVCCM TAIFA KUUNGURUMA KATIKA MKUTANO WA HADHARA JIJINI MWANZA.
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Katibu Mkuu Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM Taifa), Shaka Hamdu Shaka, hii leo anatarajiwa kuunguruma Jijini Mwanza, katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kirumba, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Zidi Bonyeza HAPA
Friday, 1 April 2016
KAMATI YA NIDHAMU YA TFF KUKUTANA KESHO
Eliud Mvella
Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitaendelea kesho Jumamosi saa 3 asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo Karume, na maamuzi yake yatatangazwa saa 7 mchana.
KUZIONA SERENGETI BOYS V THE PHARAOHS BUKU MBILI TU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (2,000) ndio kitakachotumika katika mchezo wa kesho Jumamosi kati ya Serengeti Boys (Tanzania) v The Pharaohs (Misri) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
TFF imeweka kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (2000) uwanja mzima, kutoa nafasi kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuja kushuhudia mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za vijana za Tanzania v Misri.
LULU DIVA: VIDEO ZA BONGO USIPOANGALIA IMEKULA KWAKO

Video Queen na msanii wa filamu Bongo, Lulu Abbasi 'Lulu Diva' akiwa katika pozi wakati wa mahojiano na Global Tv Online.
JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA ITAKUWA NI MIEZI MITATU KWA NCHI NZIMA
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo.
JOKATE NA MO DEWJI FOUNDATION KUJENGA KIWANJA CHA MICHEZO SEKONDARI YA JANGWANI
Mwanzilishi wa ujenzi huo, Jokate Mwegelo akiandika jambo wakati ujenzi wa kiwanja ukiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Taasisi ya Mo Dewji.
WATUMISHI HEWA 2,204 WALAMBA ZAIDI YA SHS. 5 BILIONI KWA MWAKA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Felix Ntibenda (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
TAKRIBAN
watumishi 2,204 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara wamekuwa wakiitia hasara serikali
ya Shs. 5.5 bilioni kila mwaka, brotherdanny.com inaripoti.
WAKUU WA MIKOA WAAGIZWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI KUKUSANYA MAPATO
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene
(kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Mhe. Aggrey Mwanri (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjeejijini
Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri
Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA WADAU WA MRADI WA MABASI YA DART
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene akiongea na wadau wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi
wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale.
AZIRI KITWANGA, VIONGOZI WAKUU UHAMIAJI NA JESHI LA ZIMAMOTO WAFANYA KIKAO CHA MAPITIO YA RASIMU YA BAJETI KWA MWAKA 2016/17
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti
ya Wizara yake ya Mwaka 2016/17 kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
pamoja na Idara ya Uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, kilijumuisha Viongozi Wakuu wa
Taasisi hizo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Katibu
Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EVENT YA "BMG MEET AND GREET LIVE" KUFANYIKA JIJINI MWANZA WIKI IJAYO.
KUTANA NA MARAFIKI ZAKO WA MTANDAONI LIVE BILA CHENGA. NI KATIKA "BMG MEET AND GREET LIVE" ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI IJAYO APRIL 09, 2016 RIVER SIDE HOTEL KILOLELI JIJINI MWANZA KUANZIA SAA NANE MCHANA NA KUENDELEA!
Wapendwa Wasomaji wa Binagi Blog-BMG, imeandaliwa event ya kuwakutanisha wadau wote ili kufahamiana kwa wasiofahamiana na kusalimiana live kwa wanaofahamiana.
Mchango kwa kila mshiriki ni shilingi 10,000 tu na utakunywa, kula na kucheza pamoja na Marafiki zako wa mitandaoni kama vile whatsupp, Instagram, facebook pamoja na Binagi Blog-BMG.
NI WAKATI WAKO SASA KUKUTANA NA KUSALIMIANA NA MARAFIKI ZAKO LIVE.
Zaidi piga simu nambari +255 (0) 757432694 au binagimediagroup@gmail.com
WASHIRIKI ISHIRINI BORA WA SHINDANO LA ‘MO ENTREPRENEURS’ WATANGAZWA
Taasisi ya Mo Dewji Foundation wakishirikiana na kampuni ya Darecha Limited wametangaza majina ya washiriki 20 bora wa shindano la Mo Mjasiriamali (Mo Entrepreneurs Competition). Shindano la Mo Mjasiriamali lilizinduliwa mwezi wa Januari, 2016 na mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya MeTL na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Bilionea Mohammed Dewji. Akizindua shindano hilo mweneyekiti huyo alisema,
"Tatizo la ukosefu wa mitaji ni kikwazo kikubwa kwenye ukuaji wa biashara za vijana wengi hapa nchini.Hivyo ni muhimu kuwaongezea vijana fursa za upatikanaji wa mitaji"
Shindano la Mo Mjasiriamali linalenga kuwainua vijana wenye shauku, ari na nia ya dhati ya kukuza biashara zao ili kujiongezea kipato na mchango wao katika ujenzi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
WAZIRI WA AFYA AKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MAJIMBO YA MTWARA VIJIJINI, MASASI NA NDANDA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akiwasili katika hospitali ya Rufaa Ndanda Mission.
Katika ziara hiyo ya siku 2 Mh. Ummy alipata fursa ya kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kukagua wodi za wagonjwa, maabara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa idara ya afya na wananchi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo hayo.
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma hiyo. (Picha na Modewjiblog)
Mwaka 2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)


















