Polisi mkoa wa Dodoma nchini Tanzania wanawashikilia wahamiaji haram 64 raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akipatikana akiwa amekufa.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Monday, 16 March 2015
MAMILIONI WAANDAMANA KUTAKA RAIS WA BRAZIL ASHTAKIWE KWA UFISADI MKUBWA
Rais Dilma Roussef wa Brazil
Zaidi ya watu milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe mashtaka ya ufisadi mkubwa uliofanyika katika shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
WAANDISHI, WANAHARAKATI MBARONI DR CONGO
Lambert Mende waziri wa habari na msemaji wa serikali ya DR Congo.
Waandishi wa habari wa kigeni, wanadiplomasia, wanaharakati na wasanii mbalimbali wametiwa mbaroni na polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wakiwemo waandishi wa habari wa BBC.
Sunday, 15 March 2015
WANAWAKE MSIWE NA WIVU, HAMTABARIKIWA
Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
ARUSHA: IMEELEZWA kuwa pamoja na kuwa baadhi ya wanawake wanadai kuwa wameokoka na wanampenda Mungu lakini bado hawatekelezei sheria na tabia ya Mungu ambayo ni upendo badala yake wengi wao wanasumbuliwa na tabia ya wivu.
ASASI ARUSHA YAPINGA MATUMIZI YA WATU WAZIMA KUOGA MITONI
Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
ARUSHA: ASASI ya Initiative for Youth (INFOY) ya jijini Arusha imeomba Serikali kushirikiana nayo kupiga vita tabia ya baadhi ya watu wazima kuoga katika mito kwani wanaoga katika mito wanaaaribu watoto wadogo ambao nao bado wanakuwa.
ARUSHA: ASASI ya Initiative for Youth (INFOY) ya jijini Arusha imeomba Serikali kushirikiana nayo kupiga vita tabia ya baadhi ya watu wazima kuoga katika mito kwani wanaoga katika mito wanaaaribu watoto wadogo ambao nao bado wanakuwa.
Saturday, 14 March 2015
KAULI ZA VIONGOZI ZATIKISA NA KUWAKERA WANANCHI
- Juma Nkamia: Mwaka 2013: “Sugu naomba ukae kimya, halafu uelewe mimi siongei na mbwa, naongea na mwenye mbwa.”
- John Magufuli: Mwaka 2012: “Asiyetaka kulipa nauli hiyo, apige mbizi baharini na kama hawezi azunguke Kongowe kuingia katikati ya jiji au arudi kijijini akalime”.
MABOMU YARINDIMA JIJINI MWANZA
Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), wakilinda Mtaa wa Makoroboi, jijini Mwanza jana, baada ya kudhibiti vurugu. Picha na Ngollo John
Na Ngollo John, Mwananchi
Mwanza. Hali ya amani katikati ya Jiji la Mwanza jana ilichafuka kwa takriban saa mbili kutokana polisi kupambana na wananchi, waliokuwa wakipinga hatua ya madhehebu ya Kihindi ya Swaminarayan kufunga Mtaa wa Makoroboi.
KINANA AMFAGILIA LOWASSA, ASEMA NYALANDU ANAZURURA
Na Habel Chidawali, Mwananchi
Kondoa/Monduli. Jana ilikuwa siku ya hisia tofauti kwa watu wawili wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro cha urais, Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kumsifu mmojawao na kumponda mwingine.
POLISI YAVAMIA OFISI ZA CUF, YAKAMATA VIONGOZI TISA
Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamCHAMA cha Wananchi (CUF) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mtwara kuvamia ofisi za chama hicho na kuwakamata wanachama tisa.
ZITTO: NITACHUKUA UAMUZI MGUMU
Na Freddy Azzah, Kigoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ametua jimboni kwake na kuomba kuungwa mkono kwa hatua yoyote atakayochukua kuanzia sasa.
SAKATA LA KUUAWA DK. SLAA LAGEUKA
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeanza kumchunguza Josephine Mushumbusi, ambaye ni mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, anayetuhumiwa kula njama za kumuangamiza.
MUME ACHOMWA KWA KUMKUMBUKA MAREHEMU MKEWE
Mwanaume aliyechomwa na maji moto kwa kumkumbuka marehemu mke wake wake amesema kuwa haoni haya kamwe kwa kitendo alichofanyiwa na mpenzi wake.
MAJANGA ARSENAL, CHAMBERLAIN KUKAA NJE MWEZI MMOJA
Alex Oxlade-Chamberlain hatokuwepo kwa mwezi mmoja
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-Chamberlain hatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
MVUA YALETA MAAFA ANGOLA, 60 WAFA MAJI
Watu 60 wakiwemo watoto 35 wamefariki dunia kufuatia mvua nyingi iliyonyesha nchini Angola.
FIFA: ALGERIA NDIYO TIMU BORA AFRIKA
Algeria imesalia timu bora barani Afrika katika orodha ya FIFA ya mwezi March licha ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa bingwa ya Afrika na Ivory Coast.
UPANDIKIZAJI WA UUME WAFAULU AFRIKA KUSINI
Kundi la madaktari wa upasuaji kutoka Afrika kusini limefanikiwa upandikizaji wa uume wa mwanadamu.
AL SHABAAB WACHUKUA MWILI WA KIONGOZI WAO
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabaab
Taarifa kutoka Somalia zinasema kundi la kigaidi la Al Shabaab limeuchukua mwili wa kiongozi wao anayedaiwa kuuwawa na kombora la Marekani.
UNENE WAMFANYA KUKOSA BURUDANI UINGEREZA
Klabu ya burudani nchini Uingereza
Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili walizuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya.
KESI YA RAIS WA KENYA YAFUNGWA RASMI
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya (kulia) akisikiliza kesi yake
Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu wa Kivita (ICC) imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
SAKAYA AISIHI SERIKALI KUNYONGA WAUAJI ALBINO
Magdalena Sakaya
Na Hastin Liumba, KaliuaMBUNGE wa viti maalumu kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Magdalena Sakaya amemwomba Rais Dk Jakaya Kikwete kutia saini ili wauaji wanne wa watu wenye walemavu wa ngozi (Albino) waliohukumiwa kunyongwa adhabu hiyo inatekelezwa.
Friday, 13 March 2015
WAZIRI CHIKAWE AKABIDHI PIKIPIKI 35 KWA MAKATIBU KATA WA CCM WILAYA YA NACHINGWEA LEO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki Mwenyekiti wa Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Ally Napepa. Waziri Chikawe alikabidhi pikipiki 35 kwa makatibu kata wilayani humo kwa ajili kazi ya uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya hiyo, Mussa Liliyo. Picha na Felix Mwagara.
HII NAYO KALI: BWANA HARUSI AACHWA KWA KUFELI HISABATI
Harusi moja ilitibuka nchini India baada ya bwana harusi kufeli swali rahisi sana la hisibati aliloulizwa na bi harusi.
Harusi moja ilitibuka nchini India baada ya bwana harusi kufeli swali rahisi sana la hisibati aliloulizwa na bi harusi.
Kulingana na ripoti za walioshuhudia kihoja hicho cha aibu bi harusi anasemekana alimuuliza bwana harusi
''15 ukiongeza 6 utapata nini ''?
Polisi katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India wanasema kuwa sherehe za harusi hiyo zilitibuka baada ya bi harusi kufoka mumewe mtarajiwa alipotoa jibu lake . ''17 ''.
Mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za harusi yao.
Alikurupuka na kuondoka jukwaani akiwa amenuna akisema hawezi kuoa mtu ambaye hakwenda shuleni.
Juhudi zote za jamaa na marafiki waliofika kushuhudia nikaa hiyo ziliambulia patupu.
Polisi katika jimbo hilo la Uttar Pradesh wanasema kuwa jamaa wa bwana na bi harusi wote walikubaliana kurejesheana zawadi zote walizokuwa wametoa kwaajili ya wapendwa hao.
Asilimia kubwa ya ndoa zote nchini India hupangwa na wazazi na mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za harusi yao.
Bwana harusi alifeli swali la hisibati
Babake bi harusi Mohar Singh aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika kijiji cha Rasoolabad aliiambia idhaa ya kihindi ya BBC kuwa mwanawe alishangaa kuwa mumewe mtarajiwa Ram Baran hakuwa msomi.
Mwezi uliopita bi harusi mwengine aliolewa na mgeni katika harusi yake baada ya Mumewe aliyekuwa amepanga kumuoa kuanguka kifaa dakika chache tu kabla ya wawili hao kuunganishwa kuwa mume na mke .
CREDIT: BBC
HATARI KUBWA: WATUMIA PLASTIKI BADALA YA KONDOMU UGANDA
Waganda wanatumia kondomu bandia “buveera- kutokana na mifuko ya plastiki kutokana na uhaba wa Kondomu
Mahitaji yanafanya waganda kuwa wabunifu hata katika masuala ya kondomu.
Katika eneo la Kiyindi, wilaya ya Buikwe-mashariki ya Kampala, watu wanatumia kondomu bandia –wao huita “buveera- kutokana na mifuko ya plastiki.
BENKI YA CHINA YATIA HOFU MAREKANI
Fedha za China
Marekani imeelezea wasiwasi wake
kufuatia uamuzi wa Uingereza kuwa nchi ya kwanza kuu ya magharibi
kujiunga na benki ya uwekezaji ya China.
RUFAA YA OSCAR PISTORIOUS YATUPWA
Mwanariadha Oscar Pistorious
Mawakili wa mwanariadha mlemavu wa Afrika kusini Oscar Pistorius anayehudumia kifungo jela wamepoteza kesi ya rufaa kuhusu hatua ya mahakama ya kumuondolea mashtaka ya mauaji.
GAVANA WA KENYA ANUSURIKA KUUAWA NA AL SHABAAB
Gavana Ali Roba wa Kaunti ya Mandera
Mwanasiasa mmoja wa Kenya amenusurika shambulizi lililotekelezwa na kundi la Al shabaab.
Ali Roba ,ambaye ni gavana wa mji ulio mpakani wa Mandera alikuwa akisafiri kuelekea mjini humo wakati msafara wake ulipovamiwa.UNYANYAPAA WADAIWA KUKIMBIZA WENYE VVU HOSPITALI
Na Hastin Liumba,Tabora
HALI ya Unyanyapaa miongoni mwa jamii kumesababisha baadhi ya wagonjwa wa maambukizi ya VVU kujificha na kukatisha tiba hali inayopelekea wengi wao kupoteza maisha, imeelezwa.
CHIKAWE AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI 900 WILAYA YA NACHINGWEA KUJENGA MAABARA SHULE ZA SEKONDARI
SKIMU YA MPUNGA KIROKA YAPATA UGENI MKUBWA
Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla, akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi walipofanya ziara ya kugagua miradi yao ya maendeleo mkoani Morogoro.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)
IT'S FRIDAY AND ITS ON #TGIF, SKYLIGHT BAND KUKINUKISHA THAI VILLAGE USIKU WA LEO
MWALIMU MKUU AJIGEUZA MTENDAJI, MGAMBO
Na Hastin Liumba, Kaliua
WANANCHI wa kata ya Zugimlole wilaya ya Kaliua mkoani Tabora
wamemkataa mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Zugimlole Azbert Kamala kwa hatua
yake ya kujigeuza afisa mtendaji wa kata na askari mgambo na kushirikiana na
askari mgambo wengine kukamata wahalifu.
SAKAYA APANGA KUMNG`OA KAPUYA
Na Hastin
Liumba,Usinge
MBUNGE wa viti maalumu chama cha wananchi (CUF) Magdalena
Sakaya amesema atachukua fomu kugombea jimbo la Urambo Magharibi wilayani
Kaliua mkoa wa Tabora.
LEADING TEA PACKING COMPANY PROMISES GREAT TEA
CHAI BORA the leading Tea packing company in Tanzania, with over 300 employee operating countrywide distribution from head office based in Dar-es-Salaam, Companies factory is based in Mafinga Irringa region the main Tea growing area, CHAI BORA is happy to pack the Tea growing region to keep the freshness of Taste and aroma. Company Brands are known to public, accepted with ISO quality certification and TBS standards.
BARAKA SHELUKINDO ATOA TAHADHARI JUU YA MATAPELI WA MITANDAONI
Dear Friends
Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na tapeli mmoja ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook accounts kwa majina mbali mbali kama Justin Stan, James Brown, Onesmo, Felister Julius, Anthony Yohana au Yohana Anthony na mengineyo mengi.
Mtu huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
JAPAN YACHANGIA SH. MILIONI 160 SHULE YA MSINGI KAKUNI
Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga akisoma risala fupi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Tuesday, 10 March 2015
JUMUIYA YA BANGO SANGHO WATOA HUDUMA ZA AFYA BURE KIBUGUMU
SIMBA, YANGA ZAINGIZA MIL 436
UNESCO, TIE NA OUT WAFADHILI KOZI KUBORESHA MITAALA YA ELIMU AFRIKA
Ofisa mwakilishi wa Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala.
BASATA YATOA ELIMU KWA WASANII KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Na
Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) kupitia programu yake ya Jukwaa la Sanaa wiki hii limetoa elimu kwa
wasanii kuhusu maudhui ya katiba inayopendekezwa hasa ibara ya 59 ya katiba hiyo
inayohusu sekta ya Sanaa.
EU, UN WAFAGILIA JUHUDI ZA KUBORESHA HALI ZA WANAWAKE TANZANIA
Wednesday, 28 January 2015
POLISI: HATUKUMPIGA RISASI PONDA
Khadija Ahmad, mke wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa akiondoka katika Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro jana baada ya kesi inayomkabili mumewe kuahirishwa hadi Februari mwaka huu. Picha na Juma Mtanda
Na Hamida Shariff, Mwananchi
Morogoro. Shahidi wa pili katika kesi inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kuwa, hawakuhusika kumpiga risasi mtuhumiwa huyo na kwamba alikamatwa katika Hospitali ya Muhimbili akitibiwa jeraha alilodai lilitokana na risasi.
RIPOTI YA WIZARA YAZIDI KUIWEKA PABAYA IMTU

Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Dar es Salaam. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) hakitafunguliwa mpaka pale upungufu ulioainishwa utakapofanyiwa kazi.
WANASAYANSI ‘BONGO’ KUSAFISHA MAJI YA KINYESI KUWA YA KUNYWA
Na Florence Majani, Mwananchi
Dar es salaam. Umeshikwa na kiu? Unaingia katika duka lililo jirani na kununua maji ya chupa kwa ajili ya kunywa. Lakini ukapatwa na udadisi kutaka kujua maji hayo yametengenezwa na nini. Unaposoma kilichotumika kutengeneza maji hayo, unagundua kuwa yametengenezwa kwa kinyesi.
BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KUKAMATWA KWA PROFESA LIPUMBA DAR
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, akiwa chini ya ulinzi wa Polisi Dar es Salaam jana, baada ya kukamatwa kwa yeye na wafusi 36 wa Chama hicho 32 madai ya kuandamana bila kibali cha polisi, kukumbuka mauaji ya wafuasi 22 wa Chama hicho huko Pemba, Januari 26 na 27 , 2001 baada ya polisi kupambana na waandamanaji. Picha na Saidi Khamis
Kikao cha Pili cha Mkutano wa 18 wa Bunge la 10 kimeahirishwa muda huu mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka shughuli zote za serikali ziahirishwe mara moja ili kulishughulikia suala la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
NSSF, REAL MADRID KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA TANZANIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja. (Na Mpigapicha Wetu).
Subscribe to:
Posts (Atom)




