Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday, 31 August 2016
NMB YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE USONJI, YAWAPA MSAADA WA VIFAA VYA MASOMO
Pamoja na kuwa bora utoaji wa huduma za kibenki lakini pia benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora katika kusaidia jamii na katika kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa vya kutumia darasani na vya michezo kwa watoto walio na usonji (autism) ambao wanasoma katika shule ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Tuesday, 30 August 2016
TTCL YAJITOSA MISS HIGHER LEARNING INSTITUTIONS 2016
Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. Nyuma yake ni washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016.
TANESCO KUBORESHA KITUO KIKUU CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA ILALA, MAENEO KADHAA KUATHIRIKA NA UPATIKANAJI UMEME JIJINI DAR ES SALAAM
NA
K-VIS MEDIA
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuuarifu umma kuwa kutakuwepo na katizo
la umeme KUANZIA Septemba 3, 2016 kwenye maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kutokana
na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoza
na kusambaza cha Msongo wa Kilovolti 132 cha Ubungo-Ilala.
SHUKRANI ZA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED MTATURU MKONONGO
Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo enzi za uhai wake
Familia ya
marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura
pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na
Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa
upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika
kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo
(pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi,
kwa ajali ya gari.
TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA
DC NDEJEMBI AJIONEA KITUO CHA AFYA KILICHOJENGWA CHINI YA KIWANGO
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya.
RC SINGIDA AKABIDHI MADAWATI 630 KWA WAKURUGENZI WA WILAYA NA MANISPAA
Na
Mathias Canal, Singida
Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa
Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa
adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati
akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.
Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka
madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya
kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa
chini wakiwa darasani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa
makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na
Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali
ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba
na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe
amesema
kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa
ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na
wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500
hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo
hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika
Halmashauri za Singida na Manyoni.
Monday, 29 August 2016
WAZIRI WA FEDHA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA KIGOMA
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu, akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao.
RAIS MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNISHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Kipa wa Young Africans na timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Deogratius Munishi kutokana na kifo cha Baba yake mzazi, Mzee Boniventur Munishi kilichotokea jana Agosti 28, 2016.
MCHEZO WA LIGI KUU YOUNG AFRICANS V JKT RUVU
Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imethibitisha kuwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na JKT Ruvu ya Pwani, ulipangwa kufanyika Jumatano Agosti 31, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeahirishwa mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine.
KIPAO AMBADILI MUNISHI TAIFA STARS
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
DALADALA LAGONGA MAGARI MATATU MAJI MATITU TEMEKE JIJINI DAR
Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN.
Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.
Na Dotto Mwaibale
MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.
Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.
Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.
" Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema Juma.
Alisema baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.
Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.
MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM
Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUDHURIA KIKAO CHA SADC TROIKA MJINI MBABANE SWAZILAND
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Balozi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shio (katikati) kulia ni Waziri Mambo ya Njena ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika
Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
WAKAZI WA MULEBA WALIPOKEA KWA SHANGWE TAMASHA LA TIGO FIESTA USIKU WA JANA
WATANZANIA WAASA KUHIFADHI LUGHA ZA ASILI ILI KUONGEZA MISAMIATI YA KISWAHILI.
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dar es Salaam
Serikali inathamini jitihada za wadau katika kuhifadhi, kutunza na kusambaza lugha za makabila mbalimbali nchini ambazo ndio msingi wa lugha aushi ya Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa.
DC MTATURU AWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI KUHAMA NDANI YA MWEZI MMOJA
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.
KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA
Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.
NI HESHIMA UKICHINJIWA MBUZI WA SUPU MKOANI MARA.
Kuna Sherehe za aina mbalimbali mkoani Mara. Leo BMG inakujuza juu ya Shereze ya kuchinjiwa supu ya mbuzi. Hii hufanywa zaidi kwa wanajamii wa kabila la Wakurya mkoani humo.
KAMPUNI YA MABIBO YAWAANDALIA BONANZA WASHIRIKI MISS KINONDONI 2016 ILI KUWAWEKA FITI
Wanyange wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 wakionesha moja ya shoo katika Bonanza walioandaliwa na Mdhamini wao Mkuu Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd lililofanyika ufukwe wa Jangwani Sea Breeze Mbezi jijini Dar es Salaam jana lenye lengo la kuwaweka fiti kabla ya shindano lao litakalofanyikaa Septemba mbili Hoteli ya Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.
Sunday, 28 August 2016
ASASI YA FEDHA YAWAKUMBUSHA WANACHUO UMUHIMU WA KUWEKA AKIBA
Mkurungezi
mtendaji wa Asasi ya Fedha Jafari Selemani akisitiza jambo wakati wa
ufunguzi wa warsha iliyofanyika katika Chuo cha Kilimanjaro Insitute college na
kuwakutanisha wanavyuo zaidi ya mia 2 hapa jijini Dar es salaam ambapo
alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa na tabia ya kuweka akiba na
kujiandaa na maisha ya uzee ambapo Moto wa asasi hiyo ni "UHURU WA
KIFEDHA NI WAJIBU WAKO " kulia kwake ni mtaalamu wa biashara na
mhamasishaji wa vijana Fasili Boniface mapema mwishoni wa wiki
iliyopita.
RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUBILEI YA DHAHABU (MIAKA 50) YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA
Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe wakati akiwasili kuhudhuria Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016.
KAMANDA SIRRO ATANGAZA KIAMA KWA WANANCHI WATAKAO ANDAMANA SEPTEMBA MOSI JIJINI DAR
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUFANYA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIPYA NA LA KISASA.
TIGO FIESTA YATIKISA MJI WA KAHAMA
WAFANYAKAZI WA NMB TAWI LA NELSON MANDELA WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI MJINI MOSHI LEO.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo la njia mbili maarufu kama Double Road mjini Moshi leo.
Saturday, 27 August 2016
WATANZANIA WALIOSOMA CHINA KUPATA UONGOZI MPYA
By LEAH MUSHI
Chama
cha watanzania waliosoma China- China Allumni Association of Tanzania
(CAAT) hii leo tarehe 27 August, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu
kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.
Friday, 26 August 2016
KAMPUNI YA UDALALI YA YONO YAINGIA MKATABA WA KIMATAIFA NA KAMPUNI YA BIDDERS CHOICE YA AFRIKA KUSINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scholastika Christian Kevela (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo (hawapo pichani), mkataba wa kimataifa walioingia na Kampuni ya Bidders Choice ya Afrika Kusini wa ushirikiano kwa ajili ya kufanya mnada wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela.
KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YATEMBELEA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
Thursday, 25 August 2016
KESHO NI KESHO TANZANIA V IVORY COAST
Mchezo wa kwanza wa mpira wa miguu wa ufukweni, kati ya Tanzania na Ivory Coast unatarajiwa kufanyika kesho kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja uliotengenezwa maalumu kwa ajili ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza
wakati wa kuaga miili ya askari
waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada
hiyo ya kuaga ilifanyika katika Viwanja
vya Polisi vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI BUNDA AMSIMAMISHA KAZI MTHAMINI ARDHI KWA RUSHWA
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth Mayanja akiwa ofisini
kwake.
Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth Mayanja amemsimamisha kazi mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
MFUKO WA PSPF WATOA ELIMU YA KUJIUNGA KATIKA MFUKO WA KUJICHANGIA KWA HIARI KWA WANANCHI WASIO KATIKA SEKTA RASMIN ZANZIBAR
Afisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Fadhila akizungumza wakati wa Mkutano Taasisi zisizo rasmin za Wavuvi, Madereva wa gari za mchanga, Kifusi na Wakulima wa mbogamboga kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ya Mfuko wa PSPF uliofanyika katika ukumbi wa Betilyamin Malindi Zanzibar.
TATIZO LA CHADEMA WANAPIMA HOMA KWA KIGANJA!
Na Daniel Mbega
NILIWAHI
kuandika wakati fulani kwamba “UKWELI WA MWANASIASA NI JINA LAKE TU” lakini wakatokea watu wengi kunikosoa, wakipinga uchambuzi wangu huo na wengine
wakinitisha kwa maneno kwa sababu tu nilikuwa nimekisema kile ambacho wao ama
wapendwa wao hawakupenda kisemwe hata kama kiko wazi.
Ilikuwa ni
wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu 2015 wakati nilipozichambua kauli
za mawaziri wakuu wa zamani – Edward Lowassa na Frederick Sumaye – waliokwenda kutafuta
hifadhi Chadema baada ya kuona ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hawana nafasi
ya kwenda Ikulu tena kama wakuu wa nchi.
Nilisema kwamba
wanasiasa hao wamefuzu katika sanaa. Bora Lowassa tunajua alisomea sanaa, lakini
Sumaye alisomea kilimo!
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(katikati), katika kikao
cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao
ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali
kwa asilimia kumi ifikapo mwezi
Februari, mwakani.Wa kwanza mkono wa kulia kwa Naibu Waziri ni Katibu Mtendaji wa baraza ambae pia ni Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani , Mohamed Mpinga.
Kikao kilifanyika katika ukumbi wa
wizara,jijini Dar es Salaam.
RC SIMIYU ATOA UFAFANUZI SAHIHI WA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi
wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo
lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na
Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na
mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Wednesday, 24 August 2016
TAIFA STARS YA KUIVAA NIGERIA HII HAPA
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Subscribe to:
Posts (Atom)