Wachimbaji wadogo wakiwa kwenye mkutano
Na Hastin Liumba, Nzega
OFISI ya Afisa Madini Mkazi Tabora imewataka wafanyabiashara wa madini Mgodi mdogo wa dhahabu wa Mwanshina uliopo wilayani Nzega Mkoani Tabora kukata Leseni za Biashara hiyo ili waweze kuwa na sifa na kukidhi mahitaji ya sheria mpya ya madini ya mwaka 2010.
Mgodi huo una zaidi ya wafanya Biashara 60 wa dhahabu ambao hawana Leseni na hawatambuliki na wizara ya Nishati na Madini hali inayopelekea serikali kuu na wilaya kushindwa kukusanya mapato ambayo yanegeweza kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza na uongozi wa mgodi huo Mtaalam wa miamba ya madini Joseph Ngullumwa aliwataka viongozi hao kuhakikisha wafanya biashara wanao nunu dhahabu katika mgodi huo wasajiliwe na kutambulika na wizara ya madini ilikuweza kupata stahiki zao.
Alisema kitendo cha kukwepa kusajiliwa na wizara ya madini ni kuisababishia hasara serikali ya kutokusanya mapato ambayo yangeweza kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Masumbuliko Jumanne meneja mkuu wa mgodi huo alisema jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha wafanya Biashara wanapatiwa Elimu ya kusajiliwa na kupata Leseni ambayo itawasaidia kufanya kazi zao kwa uhuru mkubwa tofauti na sasa wanafanya kazi kwa kificho.
Hata hivyo wafanya biashara hao hawakuweza kupatikana kwa muda huo na kuonogeza kuwa zaoezi hilo litafanyiwa kazi na uongozi wa mgodi iliwapatikane na kusajiliwa haraka kama maagizo ya sheria mpya ya madini ya mwaka 2010 inavyowataka wafanya biashara hao.
Samweli Nhindilo katibu wa mgodi huo alisema endapo wafanya biashara wataitikia wito huo na kufuata masharti ya serikali mgodi huo utakuwa umetimiza mmoja ya vigezo vikubwa na kuweza kujua kiasi gani cha dhahabau kimepatikana kwa muda tangu uchimbaji ulipoanza.
Alisema serikali ya wilaya na serikali kuu zitapata mapato kupitia wafanya biashara hao endapo watakata Leseni jamii itanufaika kupitia mapato hayo.
Hata hivyo Ngassa Gakune mtaalam wa miamba ya madini aliwatahadharisha viongozi hao kuhakikisha usalama wa mashimo ya wachimbaji ambayo yanapaswa kukaguliwa kwa nyakati tofauti tofauti ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
No comments:
Post a Comment