Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 29 September 2015

VYUO VIKUU WAFURAHIA SERA YA UKAWA YA ELIMU BURE

Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini wa chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa.

Na Hastin Liumba, Tabora

BAADHI ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu wameonyeshwa dhahiri kufurahishwa na sera ya elimu bure kwa wanafunzi wa vyuo vikuu iliyomo katika ilani ya uchaguzi ya vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi, UKAWA.

Wakizugumza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walisema sera hiyo itakuwa mwarobaini wa manyanyaso na kero za upatikanaji mikopo hiyo kwani muda mwingi wamekuwa wakiutumia kuhangaikia hela hizo.

Aidha walisema kitendo cha serikali kuanzisha bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kililenga kumaliza kero za upatikanaji mikopo hiyo ikiwemo kuwezesha wanafunzi wengi zaidi wenye sifa za kujiunga vyuo vikuu lakini hawana uwezo kupata fursa hiyo.

"Hali imekuwa tofauti, wanafunzi wengi wanahangaika, uwezo wa bodi kugharamia wanafunzi wote haupo, badala yake tunabaguliwa kwa visingizio vya kipaumbele cha masomo tunayosoma, wanaopata asilimia 100 hata robo haifiki, wengine watapata wapi hela hizo?" walihoji wanafunzi hao.

Keneth Athuman mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino tawi la Tabora alieleza wazi kuwa sera hiyo ya UKAWA ndio mwarobaini wa wanafunzi wengi zaidi wenye sifa za kujiunga vyuo vikuu kupata elimu hiyo.

Alisema gharama za chuo kikuu ni kubwa, wazazi wengi hasa wale wa vijijini ambapo wanafunzi wengi zaidi wanatoka hawana uwezo wa kuzimudu, na bodi hiyo imeweka utaratibu wa kutoa mikopo kwa asilimia kadhaa jambo ambalo linawapa mazingira magumu ya kupata elimu wanafunzi wengi zaidi.

Underson Mkono mhitimu wa shahada ya kwanza ya ualimu alisema sera ya UKAWA ya kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu inawezekana kwani nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi zinazoweza kuongeza mapato ya serikali na kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kupata elimu hadi ngazi hiyo.

Alitoa mfano wa rasilimali zilizopo hapa nchini za madini ya dhahabu, almasi, tanzanite, nickel, makaa ya mawe na vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, maeneo ya kihistoria, ardhi nzuri na misitu kuwa zingetosha kuongeza pato la nchi kama yangesimamiwa ipasavyo.

Fikiri Richard mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu SAUT alisema sio kweli kwamba serikali imeshindwa kuiwezesha bodi ya mikopo ili wanafunzi wote wanaodahiliwa vyuoni wapate mikopo hiyo, tatizo lililopo ni mfumo mbovu wa usimamizi wa rasilimali za nchi na serikali kutokuwa na dhamira ya dhati.

Alisema kitendo cha bodi ya mikopo kutoa asilimia 100 kwa baadhi ya wanafunzi na wengine kupata asilimia kidogo huku wengine wakikosa kabisa kimefanya baadhi yao washindwe kuendelea na masomo hayo kwa umaskini wa wazazi.

Mwanafunzi Vincent Tricus alibainisha wazi kuwa tatizo lililopo ni mfumo wa utendaji wa serikali na usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi ambao unawanufaisha wachache pasipo kuchukuliwa hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment