Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 29 September 2015

WALIMU KENYA WAKAIDI AMRI YA MAHAKAMA


Mgomo wa walimu washika kasi Kenya
Masomo katika shule za umma nchini Kenya yamekwama licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu warejee shuleni jana Jumatatu.

Mgomo wa walimu kote nchini Kenya umeingia wiki yake ya tano.
Vyama vya walimu nchini Kenya vimesema havitatekeleza amri ya mahakama iliyowataka kusitisha mgomo huo kwa siku tisini kuanzia leo.
Image captionWalimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha
Badala yake vyama hivyo vimerejea mahakamani leo kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi huo.
Hata hivyo kesi yao iliahirishwa hadi alhamisi wiki hii.
Walimu walijitokeza kwa wingi wakiandamana na viongozi wao wa vyama vya walimu mwendo wa saa nane unusu.
Walimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha hapo awali mgomo ulipochacha.
Image copyright
Walimu wamegoma wakidai serikali iwalipe nyongeza ya mishahara yao
Kesi hiyo imeahirishwa hadi alhamisi saa nane u nusu kwa sababu jaji aliyekuwa akisikiza kesi hiyo aliomba radhi iliapokee matibabu.
Jijini Nairobi hii leo shule ya Msingi ya Moi Avenue na Shule ya Msingi ya Nairobi hazikuwa na wanafunzi.
Wanafunzi wamesalia nyumbani huku walimu pia wakikosa kurejea shuleni kama walivyoagizwa na mahakama.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment