Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 1 September 2015

NICHAGUENI NIKAMALIZE UBADHIRIFU MANISPAA TABORA-NTIMIZI

Mussa Ntimizi


Na Hastin Liumba, Tabora 
MGOMBEA udiwani wa kata mpya ya Mwinyi halmashauri ya manispaa Tabora kwa tiketi (CHADEMA) Musa Martini amewataka wananchi wa kata hiyo kumchagua ili akamalize ubadhirifu uliopo katika Manispaa hiyo.

Martini alisema hayo kwenye mkutano a hadhara wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Alisema akiwa katibu wa CHADEMA wilaya ya Tabora mjini amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na uongozi wa halmashauri ya manispaa Tabora na dhahiri amegundua ubadhirifu na uzembe mkubwa uliopo hivyo anaomba ridhaa ya kuchaguliwa ili akamalize hali hiyo.

Alisema moja ya ubadhirifu huo ni kuwepo kwa fedha zilizokopeshwa kwa vikundi hewa ambavyo vingi havina usajili na havijukalikani tu vilipo wala ofisi zao.

Martini aliongeza ubadhirifu mwingine ni ule uliopo idara ya ardhi kwani kuna watumishi wengi wamejilimbikizia viwanja huku maeneo menngi ya wazi yakiuzwa kinyemela.

alidai kingine ni makusanyo ya fedha ambayo hayalingani na vyanzo vya mapato ya halmashauri hiyo huku kukiwqa na mashaka fedha nyingi kuingia kwenye mifuko ya watu

Aliongeza ameamua kuombea nafasi ya udiwani ili aweze kumaliza kero za kata hiyo ikiwemo kukosekana kwa barabara za uhakika,mitaro hali ambayo inaleta kero kipindi masika,kata kukosa zahanati wala kituo cha afya na wakazi wa kata hiyo kutosomewa mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka mitano.

Katika hatua nyingine mgombea huyo alionya taarifa za kuwepo watu wanaomba wananchi vipalata vya kupigia kura na kuorodhesha majina yao na namba zao za simu.

Kwa upande wake katibu wa BAVICHA wilaya ya Tabora mjini Josephine John alisema aliomba wakazi wa kata hiyo kwa kuchagua kiongozi aliye mbumbumbu.

Alisema wakazi hao wachague mtu sahihi na siyo mgombea yule wa CCM ambaye hajafanya kitu akijitetea kuwa kata ni kubwa ndiyo maana ameshindwa kutimiza ahadi zake.

Alisema hakuna sababu kuichagua CCM tena hali ambayo umasikini umezidi ikiwemo watoto watano kulala kitanda kimoja,kushindwa hata kunywa chai ya uhakika na wajawaito hospitali ya Rufaa kitete ambayo bado haina hadhi ya kuwa Rufaa.

No comments:

Post a Comment