Wachimbaji wadogo
Na Hastin Liumba, Nzega
ZAIDI ya wachimbaji wadogo 2,500 katika mgodi mdogo wa dhahabu wa Mwanshina uliopo wilayani Nzega Mkoani Tabora wamehofia kufukuzwa mara baada ya uchaguzi mkuu.
Wamesema baada ya uchaguzi kufanyika kwani wanachodai kuwa mgodi huo umefunguliwa kisiasa ili viongozi husika wapate kura kupitia wachimbaji hao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wachimbaji walisema wamekuwa wakipata taarifa baada ya kumalizika kwa shuguli ya kupiga kura mwezi Octoba 25, mwaka huu kwa kuwapata Diwani,Mbunge na Rais mgodi huo utafungwa .
Juma Ramadhani mchimbaji alisema kuna kila sababu ya wachimbaji hao kuwaeleza ukweli ili wajue jinsi ya uwekezaji wao kutokana na kutimuliwa mara mbili mgodini hapo hali iliyopelekea kupata hasara kubwa ya mali zao.
Alisema taarifa wanazoendelea kuzipata nikuwa pindi uchagugi utakapo malizika jeshi la polisi litapewa jukumu la kuwafukuza wachimbaji hao na kuongeza serikali inapaswa kuwaangalia watu hao kwa jicho la kuwasaidia ili waweze kupata ridhiki.
Joseph Ngullumwa ni mtaalam wa miamba akizungumza na wachimbaji hao walipowatembelea alisema mgodi huo unatambulika kupitia Ressein ya Tumain Group na kuwatoa hofu wachimbaji hao uhai wa Ressein hiyo ni miaka saba.
Alisema kuwa mgodi huo haupo kisiasa bali unatambulika kisheria na serikali na kuwataka kufanya kazi kwa kujituma ili kujikwamua na umasikini na kuongeza kuwa serikali imewekeza kwa wachimbaji wadogo.
Ngassa Kagune mtaalam wa miamba aliwataka wachimbaji hao kuzingatia utunzaji wa mazingira katika mgodi huo kulipa kodi kama ilivyo ada ilikuweza kukidhi vigezo vya ressein hiyo ambayo itadumu kwa muda wa miaka saba.
Katibu wa Mgodi huo Samweli Nhindilo aliwatoa hofu wachimbaji hao kuwa Ressein hiyo ina uhai wa miaka saba na kuongeza kuwa miaka saba ikiisha kuna uwezekano mkubwa wakuihuisha ili kazi ziendelee kama kawaida.
Aliwataka wachimbaji hao kufanya kazi kwa bidii kwa kujituma na kujiamini kutokana na uwekezaji huo kuwa ni mkubwa na unatambulika na serikali.
No comments:
Post a Comment