Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 1 September 2014

VYUO VYATAKIWA KUFUNDISHA UJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha: VYUO vya elimu hapa  nchini vimetakiwakufundisha masomo ya ujasiriamali mashuleni ili kuwawezesha wanafunzi wanaohiotimu katika vyuo hivyo kuweza kujiajiri wenyewe  badala ya kusubiria ajira kutoka serikalini.
Aidha baadhi ya vyuov imekuwa vikifundisha tu masomo ya kawaida hali ambayo inawafanya wahitimu wanapohitimu masomo yao kujikuta hawana ujuzi wa aina yeyeote wa kuwafanya waweze kujiingizia kipato.
Hayo yalielezwa na mkuu wa chuo cha habari maalum kilichopo Ngaramtoni Jackson Kaluzi alipokuwa akizungumza katika mahafali ya chuo hicho ambapo wahitimu 21 wa kozi ya uhandishi wa habari pamoja wahitimu 12 wa ngazi ya diploma ya uongozi  bora walitunukiwa vyeti vyao.
Aidha Kaluzi alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa vyuo kuanzisha kozi za ujasiriamali katika vyuo vyao ili kuweza kuwapatia wanafunzi ujuzi wa kujiajiri wenyewe  hali ambayo itawafanya kuachana na changamoto ya kusubiria ajira.
“Kwa sasa swala la ajira kwa vijana wetu ni kubwa sana ila ili tuweze kupambana na halii hii lazima wamiliki wenye vyuo waangalie jinsi gani ya kuwawezesha hawa vijana wetu waweze kujiajiri wenyewe kwa kuwafundisha masomo ya ujasiriamali ambayo yatawasaidia katika kujiingizia viapato vyao,” aliongeza Kaluzi.
Alieleza kuwa katika kuhakikisha kuwa vijana wanaohitimu chuoni hapo wanajiajri wenyewe chuo hicho kimefanikiwa kufundisha somo la ujasiriamali ambapo baadhi ya wahitimu hao wataweza kutumia ujuzi walioupata kujiajiri wenyewe na kuachana na tabia ya kusubiria ajira kutoka serikalini.
Aliongeza kuwa ni vema vyuo vikajipanga kuwaandaa vijana watakaokuwa bora katika maeneo muhimu kwenye jamii inayowazungua na kuacha kufundisha masomo ambayo hayana umuhimu kwenye jamii.
Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo mkurugenzi wa kampuni ya Feeder International kutoka Kenya,  Ari Joensuu, aliwataka wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanatumia elimu waliyoipata kwa kuibadilisha jamii
inayowazunguka.

No comments:

Post a Comment