Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 20 September 2014

TAMWA KUENDELEA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO


Na Mwandishi Wetu

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimesema kitajikita kutoa elimu na kuendelea na utafiti kuhusu ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwenye maeneo ambayo elimu hiyo haijawafikia wananchi na kuifanya Tanzania bila ukatili inawezekana.

Mwenyekiti wa Tamwa, Rose Ruben, alisema hayo wakati akizindua

ripoti ya utafiti kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kijinsia mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Rose alisema ripoti inaonyesha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto vimepungua kwa kiasi kikubwa, tofauti na mwaka jana walipozindua ripoti kama hiyo.

Alisema utafiti huo uliofanywa Mei 18 na 27, mwaka huu, ulilenga masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar ambapo uliwashirikisha wanahabari kutoka NIPASHE, Mwananchi, Majira, Uhuru, Jamhuri, Zanzibar Leo, Habari Leo na ZBC-Radio.

Alisema tofauti na mwaka jana taarifa zilikusanywa bila kuwa na takwimu, wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa mwongozo wa ukusanyaji wa takwimu ambapo wilaya ya Ilala katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2014 matukio ya ukatili wa kijinsia yalikuwa 393, takwimu zinaonyesha kuwa wanawake waliofanyiwa ukatili kwa mwaka 2013/2014 walikuwa 2,108.

Aliongeza kuwa vitendo vya ubakaji katika Wilaya ya Kinondoni ni vya kiwango kikubwa kwani utafiti unaonyesha kuwa watoto hubakwa na kulawitiwa kwa wakati mmoja hususani wanafunzi wa shule za msingi.

Taarifa zilizotolewa na Dawati la Kijinsia mkoa wa Ilala na Prisca Komba, zinaonyesha kuwa matukio ya ubakaji yanaonyesha kupungua kutoka 288 na kufikia 97, wakati ya ulawiti yamepungua kutoka 15 hadi 12.

Aidha, utafiti unaonyesha kesi nyingi za ubakaji na ulawiti zinatokea Mwenge, Kinondoni Shamba, Msasani nyingine zinatokana na wananchi kutofautiana kwa mambo mengine na kutungiana kesi za ubakaji kwa lengo la kukomoana ambapo huishia hewani kwa kukosekana kwa ushahidi.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment